Wadukuzi wa Korea Kaskazini wadaiwa kudukua kampuni ya Urusi inayozalisha makombora ya hypersonic

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Habari za udukuzi huo zilikuja muda mfupi baada ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu kusafiri hadi Pyongyang mwezi Julai kuadhimisha mwaka wa 70 wa kumalizika kwa Vita vya Korea.

Kwa takriban miezi mitano hivi , kundi moja la wadukuzi wa Korea Kaskazini wamekuwa wakidukua kwa siri mtandao wa kompyuta za jeshi la Urusi , linalohusika na uundaji wa silaha nyingi zikiwemo zile za masafa marefu na zile za hypersonic kwa takriban miezi mitano kulingana na chombo cha habari cha reuters.

Watafiti katika kampuni ya uchanganuzi wa usalama wa mtandao ya SentinelOne walichunguza data zao na kuhitimisha kuwa vikundi vya wadukuzi wa ScarCruft na Lazarus, vinavyoaminika kuwa na uhusiano na Korea Kaskazini, vilikuwa vikisakinisha kwa siri kile kinachoitwa milango ya nyuma kwenye mifumo ya NPO Mashinostroeniya ambayo kupitia hiyo wangeweza kupata data nyeti.

Reuters haikuweza kujua ni data gani hasa wadukuzi waliweza kufikia. Miezi michache baada ya udukuzi huo, Pyongyang ilitangaza mabadiliko fulani kwenye programu yake ya makombora ya masafa marefu, lakini haijabainika ikiwa hii ni kutokana na vitendo vya wadukuzi hao na taarifa walizopokea.

Udukuzi huo ulianza mwishoni mwa 2021 na uliendelea hadi Mei 2022, wakati, kulingana na ripoti za ndani za kampuni, wahandisi wake wa masuala ya teknolojia waligundua shughuli za kutiliwa shaka.

Timu ya wachambuzi wa SentinelOne ilifahamu udukuzi huo baada ya kugundua kwamba mfanyakazi wa NGO (aliyekataa kutoa maoni yake kama ilivyoombwa na Reuters) alivujisha kwa bahati mbaya mawasiliano ya ndani ya kampuni yake katika jaribio la kuchunguza shambulio la Korea Kaskazini kwa kupakia ushahidi kwenye tovuti ya kibinafsi inayotumiwa na watafiti wa usalama wa mtandao duniani kote.

Wataalamu wawili huru wa usalama wa kompyuta, Nicholas Weaver na Matt Tate, walichambua yaliyomo kwenye barua pepe iliyofunguliwa na kuthibitisha uhalisi wake.

Wachambuzi walithibitisha saini za siri za barua kwa seti ya funguo zinazodhibitiwa na NPO Mashinostroeniya.

"Nina imani kabisa na ukweli wa data hii," Weaver aliiambia Reuters. "Jinsi habari hiyo ilivyofichuliwa ilikuwa matokeo ya kosa la kustaajabisha kabisa."

SentinelOne ilisema wanaamini kuwa Korea Kaskazini ndiyo iliyohusika na udukuzi huo, kwani wavamizi hao walitumia programu hasidi ya hapo awali na miundombinu iliyojengwa kutekeleza udukuzi mwingine unaohusiana na Pyongyang.

Roketi na mafuta

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Roketi ya Korea Kaskazini ya Hwasong-18 inatumia injini dhabiti ya kurusha hewa
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na wataalamu, tukio hili linaonyesha wazi kwamba, katika jitihada za kupata teknolojia muhimu, nchi iliyotengwa inaweza pia kupeleleza washirika - katika mkesi hii, Urusi.

Kulingana na wataalamu katika uwanja wa teknolojia ya roketi, NPO Mashinostroeniya ni mmoja wa watengenezaji wa kwanza wa makombora ya hypersonic, teknolojia ya satelaiti na silaha za kizazi kijacho.

Tangu Korea Kaskazini ianze kuunda kombora la balestiki la mabara lenye uwezo wa kushambulia bara la Marekani, maendeleo ya kampuni ya Urusi yamekuwa ya manufaa kwa Pyongyang.

Mnamo mwaka wa 2019, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kuunda kombora la Zirkon hypersonic, lenye uwezo wa kusafiri kwa takriban mara tisa ya kasi ya sauti. Roketi hiyo ilitengenezwa na NPO Mashinostroeniya.

Lakini, hata iwapo wadukuzi wa Korea Kaskazini wangeweza kupata data kwenye Zircon, hii haimaanishi kwamba Pyongyang itapokea uwezo sawa wa kijeshi mara moja, anasema Markus Schiller, mtaalam wa makombora wa Ulaya ambaye amesoma misaada ya kigeni kwa mpango wa makombora wa Korea Kaskazini, michoro pekee haitoshi, anaamini.