Korea Kaskazini ina silaha ngapi na inafanyia majaribio makombora gani

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kombora la Korea kaskazini

Korea Kaskazini ilirusha kombora kuelekea Japan, ambalo lilisafiri takriban kilomita 4,500 (maili 2,800) kabla ya kuanguka katika Bahari ya Pasifiki, jambo ambalo haijafanya tangu 2017.

Wakati huo huo, katika miezi ya hivi karibuni, imejaribu kombora la masafa marefu lililopigwa marufuku mwaka 2017 kwa mara ya kwanza, kulingana na Korea Kusini na Japan.

Umoja wa Mataifa umepiga marufuku Korea Kaskazini kufanyia majaribio ya silaha za kinyuklia na zile za masafa marefu , na umeiwekea vikwazo vikali baada ya majaribio ya hapo awali.

Mnamo mwaka wa 2018, Kim Jong-un alitangaza kusitishwa kwa majaribio ya nyuklia na makombora ya masafa marefu baada ya kukutana na Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.

Hatahivyo, kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alitangaza mnamo 2020 kwamba hafungwi tena na masharti hayo.

Je Korea kaskazini imefanyia majaribio makombora gani

Korea kaskazini imefanya majaribio makombora 30 mwaka huu , miongoni mwao yakiwa makombora yenye uwezo wa kuruka hadi Marekani. Haya ni pamoja na makombora ya masafa marefu, pamoja na makombora ya hypersonic.

Mwaka 2017, Korea kaskazini ilifanyia majaribio kombora la ICBM, Hwasaong 12 ambalo liliruka urefu wa kilomita elfu nne mia tano.

Pia imekuwa ikifanyia majaribio Hwasong 14, ambalo lina uwezo mkubwa zaidi na uwezo wa kusafiri kwa takriban kilomita 8000, hata ijapokuwa baadhi ya tafiti zinasema kwamba linaweza kufikia hadi kilomita 10,000, umbali wa kusafiri hadi mjini New York. Ni mataifa ya Marekani , Urusi na China yalio na silaha inayoweza kuruka umbali huo.

Makombora aina ya Hypersonic husafiri kwa mwendo wa kasi na chinichini ili kuweza kukwepa kutambulika na rada.

Silaha ya hivi karibuni iliofanyiwa majaribio juu ya anga ya Japan inaaminika kuwa ile ya Hwasong-12, ambayo ina uwezo wa kusafiri kilomita elfu nne mia tano likiwa na uwezo wa kushambulia kisiwa cha marekani cha Guam kutoka Korea kaskazini.

.

Chanzo cha picha, NORTH KOREA STATE AVERAGE

Maelezo ya picha, Hwasong-17 ndilo kombora kubwa zaidi lililojaribiwa kufikia sasa na Korea Kaskazini.

Katika uzinduzi wa awali, Machi mwaka huu, maafisa wa Japan walikadiria kuwa kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja jingine (ICBM) liliruka kilomita 1,100 kwa zaidi ya saa moja. Inaweza kubeba mzigo wa tani 2.5, hivyo kinadharia lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia.

Wachambuzi katika Kituo cha James Martin cha Mafunzo ya Kuzuia Uenezaji wa silaha Ulimwengu waliambia Reuters kuwa inaonekana kuwa "kombora lililoboreshwa" la kombora lililojaribiwa hapo awali, la KN-23.

Marekani na Korea Kusini zilionya wakati huo kwamba Korea Kaskazini inaweza kuwa inajiandaa kufanyia majaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza tangu 2017.

Chati inayoonesha aina tofauti ya silaha

.
Maelezo ya picha, Makombora ya Korea kaskazini na umbali yanayoweza kurukM

"Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio makombora yenye masafa marefu," anasema Joseph Byrne, mtafiti mwenza katika Taasisi ya Huduma za Kifalme Marekani.

"Hili ndilo kombora la masafa marefu zaidi kuwahi kurushwa juu ya Japan. Linaweza kuwa utangulizi wa majaribio ya aina nyingine ya makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia, jambo ambalo limetabiriwa kutokea."

Kwa upande wa kombora la Hwasong-15, linafikiriwa kuwa na umbali wa kilomita 13,000, na kuliweka bara zima la Marekani katika njia panda.

Mnamo Oktoba 2020, Korea Kaskazini ilizindua makombora yake mapya zaidi: Hwasong-17, lenye uwezekano wa masafa ya kilomita 15,000 au zaidi. Li naweza kubeba vichwa vitatu au vinne vya nyuklia, badala ya moja tu, na kufanya iwe vigumu kwa taifa kujilindadhidi yake.

Kuzinduliwa kwa makombora hayo mapya kulionekana kuwa ujumbe kwa utawala wa Biden kuhusu kuongezeka kwa uwezo wa kijeshi wa Kaskazini, wataalam wanasema.

Je Korea Kaskazini ina aina gani ya silaha za kinyuklia?

Mara ya mwisho Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la nyuklia ilikuwa mwaka wa 2017. Mlipuko wa jaribio hilo huko Punggye-ri ulikuwa na nguvu.

Bomu la kiloton 100 lina nguvu mara sita zaidi ya lile ambalo Marekani ilidondosha huko Hiroshima mwaka 1945.

Korea Kaskazini ilidai kuwa hiki kilikuwa kifaa chake cha kwanza cha nyuklia, chenye nguvu zaidi ya aina zote za silaha za atomiki.

Hata hivyo, huenda Korea Kaskazini sasa inalenga kufanyia majaribio aina ndogo ya vichwa vya nyuklia kwa kutumia vilipuzi sawa na hivyo, kulingana na Byrne.

.
Maelezo ya picha, Idadi ya silaha zilizofanyiwa majaribio na viongozi hawa wawili

Chati inayoonesha silaha zilizofanyiwa majaribio katika miaka kadhaa na Kim Jong - il na kim jong Un

"Inaonekana kwamba sasa wanajaribu uwezo mpya: kichwa kidogo cha kivita ambacho kinaweza kuwekwa kwenye aina mbalimbali za makombora, ikiwa ni pamoja na makombora ya masafa mafupi," anasema.

Je ni wapi ambapo majaribio ya kinyuklia yanaweza kufanyika

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Majaribio sita ya chinichini yamefanywa hapo awali huko Punggye-ri. Walakini, mnamo 2018, Korea Kaskazini ilisema italifunga eneo hilo kwa sababu "limethibitisha" uwezo wake wa nyuklia.

Baadaye, walilipua baadhi ya mahandaki yanayoelekea kwenye eneo hilo mbele ya waandishi wa habari wa kigeni. Hata hivyo, Korea Kaskazini haikualika wataalamu wa kimataifa kuangalia ikiwa imewacha kulitumia eneo hilo.

Picha za satelaiti zilizotolewa mapema mwaka huu zinaonyesha kazi ya ukarabati wa Punggye-ri ilikuwa imeanza.

Majaribio yoyote ya nyuklia yajayo kwenye tovuti yatakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mnamo mwaka wa 2018, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alimuahidi Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump kwamba Korea Kaskazini itaharibu vituo vyake vyote vya kurutubisha nyuklia.

Hata hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa la atomiki linasema kuwa picha za satelaiti zinaonyesha kuwa Korea Kaskazini ilikuwa imeanzisha upya kinu ambacho kinazalisha silaha za kiwango cha plutonium.

Shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) pia limesema mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini umepiga hatu na kazi ya kutenganisha plutonium, kurutubisha uranium na shughuli zingine.