Kwa nini Putin amepeleka silaha za nyuklia katika nchi hii?

Kiongozi wa Belarus aliye uhamishoni Svetlana Tikhanovskaya ameonya dhidi ya hatari ya Urusi kutoa silaha za nyuklia kwa Belarus.

Hivi karibuni, Alexander Lukashenko amethibitisha kuwa makombora na mabomu ya kwanza ya nyuklia ya nchi hiyo yaliyobeba silaha za nyuklia yamefika Belarus.

Muda mfupi baadaye, Svetlana alisema kuwa ilikuwa hatari kuacha silaha za nyuklia kutoka Urusi huko Belarus 'mikononi mwa dikteta wazimu'.

Akizungumza na BBC mjini Warsaw, Svetlana aliwashutumu wanasiasa wa nchi za Magharibi kwa kuwa "kimya" kuhusu kutumwa kwa silaha za nyuklia nje ya Urusi kwa mara ya kwanza tangu kuvunjika kwa Muungano wa Sovieti mwaka 1991.

Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko alitangaza kukabidhiwa kwa silaha hizo katika mazungumzo na mtangazaji rasmi wa TV wa Urusi katika eneo lisilojulikana nchini humo.

Malori ya kijeshi na vifaa vya kijeshi vinaonekana nyuma ya mazungumzo haya.

Wakati mtangazaji alimwuliza afafanue kwamba Belarus imepokea silaha mapema kuliko ilivyotarajiwa, hii inamaanisha nini? Lukashenko alisema kwa tabasamu, 'Si mara moja lakini polepole.'

Lukasjenko ameonekana kama mshirika mkuu wa Urusi na Belarus ilisaidia uzinduzi wa shambulio la Rais wa Urusi Putin Februari 2022 dhidi ya Ukraine.

Kwa nini Lukashenko ana furaha?

Inaonekana ni kwa nia ya kukasirisha washirika wa Magharibi wa Ukraine. Alisisitiza zaidi kwamba mabomu ya nyuklia ya Urusi ni "nguvu mara tatu zaidi" kuliko yale yaliyorushwa na Amerika huko Nagasaki na Hiroshima wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Lukashenko alidai kwamba aliwahitaji kujilinda dhidi ya uchokozi wa nje.

Hata hivyo, hiki ni kitisho cha uongo, ambacho amekuwa akitumia kuhalalisha kuwakandamiza wapinzani wake wote wa kisiasa.

Lukashenko amekuwa madarakani tangu mwaka 1994 na kudai ushindi katika matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyozozaniwa mwaka 2020, ambapo maandamano makubwa yalizuka.

Ili kuwakandamiza, shirika la Ujasusi KGB na polisi wa kutuliza ghasia wa Belarus waliwakandamiza kikatili waandamanaji.

Kama Ukraine na Kazakhstan, Belarus pia ilitoa silaha zake za nyuklia kwa Urusi katika miaka ya 1990 badala ya dhamana ya ulinzi na Urusi ya baada ya Usoviet na nchi za Magharibi.

Tena kupelekwa kwa silaha za nyuklia huko Belarus ni kinyume na sera hiyo, ndiyo maana pia ni habari kubwa.

Hata hivyo, bado hakuna ushahidi kamili kwamba silaha za Kirusi zimekabidhiwa kwa Belarus.

Ni aina gani ya silaha zilizopokelewa na Belarus?

Putin alikuwa ametangaza kupeleka silaha za nyuklia kwa mara ya kwanza mwezi Machi na kusema kuwa Marekani imepeleka silaha hizo barani Ulaya.

Baadaye alisema kuwa uhamishaji wa silaha ungetokea tu wakati mahali pa kuzihifadhi ni tayari, lakini Alexander Lukashenko sasa anasema kuwa Belarus ina maeneo mengi na mengi yamekarabatiwa.

Moscow inasema kwamba udhibiti wa makombora utabaki kwao. Haya ni makombora ya kimbinu na sio silaha za kimkakati za masafa marefu.

Alexander Lukashenko alisema, "Sina mpango wa kupigana na Amerika, ni silaha za kimbinu pekee zinazofaa kwetu."

Roketi ya Iskander ina uwezo wa kufika kilomita 500 au zaidi, alisema.

Svetlana anasema, "Hakuna tishio jipya kwa nchi za NATO kutokana na kutumwa huku, kwa hivyo hazichukulii kwa uzito."

Nyuma ya mantiki yao ni kuelewa kwao kwamba haijalishi kwa nchi za Magharibi ikiwa kombora hilo linarushwa kutoka Urusi au Belarus.

Urusi inapeleka silaha za nyuklia katika eneo la Kaliningrad magharibi ya mbali, karibu na Poland na nchi za Baltic.

Svetlana alisema, "Lakini Belarus ni nchi yetu na hatutaki silaha za nyuklia. Hii ni kama nafasi ya mwisho ya kuokoa uhuru wako. Lakini nchi za Magharibi hazisemi chochote."

Mpango wa Putin ni upi?

Hatua ya Urusi kunyakua rasi ya Crimea mwaka 2014 na uungwaji mkono kwa wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine kumeibua shaka kuhusu Putin nchini Belarus. Putin amekuwa madarakani nchini Urusi kwa miongo miwili iliyopita. Muda huu pia utabaki hadi 2024.

Hata baada ya haya, hakuna uwezekano wa kung’atuka madarakani kwa sababu amechukua hatua ya kujiuzulu kwa baraza zima la mawaziri akiwemo Waziri Mkuu kubadilisha katiba. Mashaka juu ya Putin yanaongezeka huko Belarus.

Mwezi uliopita tarehe 8 Desemba, viongozi hao wote wawili walisherehekea kumbukumbu ya miaka ishirini ya 'Jimbo la Muungano wa Urusi na Belarus'. Mkataba huu ulitiwa saini kati ya nchi hizo mbili mnamo Desemba 8, 1999.

'Jimbo la Muungano wa Urusi na Belarus' ina maana kwamba kulikuwa na mazungumzo ya kujiunga na Belarus nchini Urusi lakini yalibaki kwenye karatasi tu.

Maoni ya Rais Alexander Lukashenko yamekuwa yakibadilika kuhusiana na muungano na Urusi. Kabla ya kukutana na Rais Putin huko Sochi, Rais wa Belarus alikuwa amesema kwamba serikali yake haitaki kuwa sehemu ya nchi yoyote, hata Dada wa Urusi.

Ingawa Rais Alexander Lukashenko alikuwa akifikiria kitu kingine juu yake hapo awali. Katika miaka ya 1990, Rais Alexander Lukashenko amekuwa mchangiaji mkubwa wa ushirikiano wa Moscow na Minsk.