'Kifo au ndoa': Hadithi za wanawake walioolewa kwa lazima

g
Maelezo ya picha, Ruby Marie alikuwa na umri wa miaka 15 alipolazimishwa kuolewa na mwanamume ambaye hakuwahi kumuona hapo awali ambaye alikuwa na umri mara mbili ya umri wake

Ruby Marie alikuwa na umri wa miaka 15 alipolazimishwa kuolewa na mwanamume ambaye hakuwahi kumuona hapo awali ambaye alikuwa na umri mara mbili ya umri wake.

Nchini Uingereza, ndoa ya kulazimishwa ilikuwa kosa la jinai mnamo 2014. Na wenye hatia wanakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela. Mnamo 2023, umri wa ndoa nchini Uingereza na Wales uliongezwa kutoka miaka 16 hadi 18.

Hata hivyo, walionusurika katika ndoa za kulazimishwa, pamoja na wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu, wanahofia kwamba hatua zilizoongezeka zitasababisha tu waathiriwa kuwa chini ya shinikizo zaidi kutoka kwa jamaa na kushindwa kutafuta msaada.

Ndoa ya kulazimishwa chini ya sheria ya Uingereza inachukuliwa kuwa ndo ya aina hiyo wakati "mtu mmoja au wawili hawakubali au hawawezi kuidhinisha."

Sheria inachukulia ndoa ya kulazimisha kuwa ni mojawapo ya aina za unyanyasaji wa nyumbani, ambao mara nyingi huambatana na uhalifu mwingine, kama vile ubakaji.

Kulingana na takwimu za serikali, mahakama za Uingereza zinakubali hadi maombi matano kwa wiki ya watu wanaotaka kulindwa dhidi ya ndoa ya kulazimishwa.

Kulingana na takwimu za mwaka wa 2022, Kitengo cha Ndoa ya Kulazimishwa (FMU), shirika la serikali ambalo hutoa ushauri na usaidizi nchini Uingereza na nje ya nchi, lilishughulikia kesi 297 za uhalifu kama huo.

Kati ya kesi hizo :

  • Katika visa 88 (29%) waathiriwa walikuwa chini ya umri wa miaka 17
  • Katika kesi 119 (39%) waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka 18 na 25
  • Katika kesi 62 (19%) waathirika walikuwa watu wenye matatizo ya ukuaji wa akili
  • Katika kesi 235 (78%) wanawake waliathiriwa, na katika 67 (22%) - wanaume
  • Mara nyingi, zilihusu familia kutoka Pakistan, Bangladesh, India, Afghanistan na Iraq.
g
Maelezo ya picha, Foziya Rasheed kutoka Nottingham alikubali kuolewa na binamu yake nchini Pakistani kwa mtutu wa bunduki
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Profesa wa makosa ya jinai katika Chuo Kikuu cha Bristol, Aisha Gill, anasema kwamba sheria iliyoongezeka umri wa kuolewa imekuwa upanga wenye makali pande mbili: "Kwa upande mmoja, inasaidia kuzuia ndoa za kulazimishwa na kuwalinda waathiriwa, lakini wakati huo huo huongeza hatari ya ukatili wa heshima, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara, ukatili wa kimwili na ubakaji."

Wakati huo huo, wafanyakazi wa FMU wenyewe wanakubali kwamba ndoa ya kulazimishwa ni uhalifu uliofichwa kwa macho ya jamii na maafisa wa kutekeleza sheria, na waathirika mara nyingi hawawezi au hawataki kuripoti.

Kesi zinazoshughulikiwa na idara labda ni sehemu ndogo tu , na kwa kweli kuna nyingi zaidi.

Uhalifu huu mara nyingi hufanyika London na eneo la kati Magharibi, ambayo mji mkuu wake ni Birmingham.

Shirika hisani la Karma Nirvana (ambaye mwanzilishi wake, Yaswinder Sangera, mwenyewe alinusurika na ndoa ya kulazimishwa akiwa na umri wa miaka 15) aliripoti kuwa watu 9,616 walipiga simu yao ya msaada mnamo 2022-2023.

Katika kipindi hichohicho, shirika linaloshughulikia kile kinachoitwa uhalifu wa heshima liliwasaidia watu 2,346, 417 kmiongoni mwao wakiwemo wale waliotishiwa kuolewa kwa kulazimishwa.

Wanawake wawili walionusurika na ndoa za kulazimishwa wamezungumza na BBC kuhusu matukio yao ya kuhuzunisha.

Ndoa kwa mtutu wa bunduki

g

Chanzo cha picha, FOZIA RASHID

Maelezo ya picha, Foziya Rashid ana umri wa miaka 16

Kwa Fozia Rashid mwenye umri wa miaka 16 kutoka Nottingham, safari ya kuwatembelea jamaa zake nchini Pakistani iliisha kuwa jinamizi.

Mara tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, aliambiwa kwamba bibi babu yake, ambao walibaki Pakistani, walikuwa wagonjwa sana na ilimbidi "kuwaona kwa mara ya mwisho".

"Nilienda Pakistani na baada ya wiki mbili nilikuwa tayari nimeolewa," anasema. "Babu na nyanya yangu walikuwa hai na wanaendelea vizuri, hakuna mtu ambaye angekufa."

Fozia alisema kuwa mjomba wake alimnyooshea bunduki na kusema kwamba angemuua ikiwa hatamuoa mwanawe.

Wakati huohuo, wazazi wake wenyewe hawakujua kwamba binti yao alikuwa akitishwa na waliamini kwamba hiyo ilikuwa ndoa ya kawaida.

Ndugu zake wa nchini Pakistani alionya: ikiwa atajaribu kukwepa harusi, watamuua sio yeye tu, bali pia familia yake yote.

"Nilikubali kwa sababu niliogopa," anakumbuka Fozia. "Nilikabiliwa na chaguo: kifo au ndoa. Sikutaka, sikupanga, hakuna mtu aliyeniuliza, nilikuwa mtoto tu."

Baada ya kuozwa kwa lazima, alielekezwa jinsi ya kujiendesha ili mume wake apate viza ya kuhamia Uingereza.

g

Chanzo cha picha, Fozia Rashid

Maelezo ya picha, Fozia akiwa na mama yake. Wazazi wake walimuunga mkono aliposema anataka talaka

“Mwanaume niliyemuoa alinifanya nijitambue kuwa mimi ni kitu tu, nilikuwa kitu tu kwake, nilimsikia mjomba akimwambia shangazi kwamba sasa wana visa, hawanihitaji tena na kwamba wanaweza kuniua na kuwaambia wazazi wangu kwamba nilitoroka," anaendelea hadithi yake.

Kwa bahati nzuri, alifanikiwa kurudi nyumbani. Aliwaambia wazazi wake kilichompata, nao walimuunga mkono kwa kumruhusu ataliki.

Lakini msisimko uliosababishwa na mtihani huu mgumu kwa msichana wa miaka 16 ulijidhihirisha. Ulimsababishia vurugu za maono, jambo ambalo anasema yalikuwa "matokeo ya moja kwa moja ya kile kilichotokea."

g

Chanzo cha picha, FOZIA RASHID

Anaamini kuongezwa kwa muda wa kuolewa kutoka umri wa miaka 16 hadi 18 ni jambo sahihi, lakini anadhani umri unapaswa kuongezwa zaidi.

"Ndoa ya kulazimishwa haijui dini, hakuna rangi, hakuna historia," anaelezea.

Sheria ya Uingereza inasema nini kuhusu ndoa za mapema

h

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Kuanzia tarehe 27 Februari 2023, ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuchukua hatua yoyote ya kulamzimisha mtu kuoa au kuolewa kabla ya umri wa miaka 18, hata kama amekubali harusi kwa hiari na bila kushurutishwa;
  • Hapo awali, watu wangeweza kuoana wakiwa na miaka 16 au 17 iwapo wangekuwa na kibali cha wazazi;
  • Wale wanaopatikana na hatia ya kuandaa ndoa za utotoni wanakabiliwa na kifungo cha miaka 7 jela;
  • Ikiwa mtoto mdogo ameolewa nje ya Uingereza, wahalifu bado wanaweza kufunguliwa mashtaka;
  • Sheria hiyo pia inatumika kwa sherehe za "kijadi", ambazo hazina athari za kisheria nchini Uingereza.