Vita vya Ukraine: Mwanzo wa mwisho wa Rais Putin umeanza kuhesabiwa - Afisa wa Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Tahadhari katika mji mkuu wa Ukraine imeelekezwa kabisa kwenye uasi wa Kundi la Wagner, kiongozi wake Yevgeny Prigozhin, na matokeo yake kwa Vladimir Putin pamoja na mwenendo wa vita nchini Ukraine.
Mjadala kuhusu Urusi umefanya mtazamo kuwa mgumu mjini Kyiv kwamba muda wa Bw Putin kama rais wa Urusi unakaribia kumalizika.
"Nadhani muda wa kuhesabu mwisho wake umeanza," alisema Andriy Yermak, mshauri wa karibu wa Rais Zelensky.
Katika mkutano wa mjini Kyiv, alitazama nyuma mwaka ambao Urusi ilivamia Ukraine kwa mara ya kwanza, na kuiteka Rasi ya Crimea.
"Yale ambayo Ukraine imeona tangu 2014 yamedhihirika kwa ulimwengu mzima," alisema Bw Yermak.
Hii [Urusi] ni nchi ya kigaidi ambayo kiongozi wake si mtu aliyesawa na amepoteza uhusiano na ukweli. Ulimwengu lazima uhitimishe kwamba haiwezekani kuwa na uhusiano wa aina yoyote na nchi hiyo."
Maafisa wakuu wa Ukraine waliozungumza na BBC hapa mjini Kyiv wote walihoji kuwa Rais Putin hangeweza kuondokana na janga la kupoteza mamlaka yake.
Picha:
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ilianza, walisema, na uamuzi wake mbaya wa kuanzisha uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari mwaka jana.
Uasi wa Wagner, na kukashifu kwa Bw Prigozhin kwa uhalali wa Kremlin kwa vita hivyo, walisema, vimeondoa kile kilichokuwa kimesalia kwa Bw Putin kuendelea kuwepo.
"Utawala wa Putin" mmoja wao alisisitiza, "hauwezi kunusuriwa."
Ni muhimu kukumbuka kwamba chochote Waukraine, hasa wale wanaoendesha nchi, wanasema juu ya adui wao Urusi, kinatokea wakati wa mapigano ambayo wanayashuhudia, kwa usahihi, kama changamoto ya kuendelea kuwepo kwa kitaifa lao.
Waukraine wamepigana vita vya ujanja vya vyombo vya habari, na wamekuwa wakitoa ujumbe kila mara kwa watu wao na washirika wao wa Magharibi, pamoja na maadui zao huko Moscow.
Mawazo ya kutamani lazima yachukue sehemu katika tathmini wanazoshirikisha waandishi wa habari.
Lakini bado ni muhimu kutumia muda kupata maoni yao juu ya mzozo ambao umekumba urais wa adui yao mbaya Vladimir Putin.
Bila shaka, anakabiliwa na changamoto kubwa zaidi kwa mamlaka yake tangu alipokuwa rais kwa mara ya kwanza mwaka wa 2000.
Maafisa wengine wakuu mjini Kyiv wanasema wana hakika kwamba Bw Putin anapingwa na mitandao isiyo rasmi lakini iliyopangwa ya watu wa ndani waliokata tamaa.
Ofisini kwake, Oleksiy Danilov, katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa la Ukraine, aliiambia BBC kwamba "Prigozhin sio mkuu zaidi. Wanaweza kuwa wasomi wapya wa kisiasa".
Bw Danilov alisema ni pamoja na vikosi vya usalama, maafisa na wawakilishi wa matajiri wa Urusi, ambao wanaamini kuwa uamuzi wa Bw Putin kuanzisha uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari mwaka jana umekuwa maafa ya kibinafsi kwao na vile vile tishio kwa Urusi.
Bw Danilov, mwanamume mwenye umri wa miaka sitini akiwa amevalia vazi jeusi la mtindo wa kijeshi na jina lake la ukoo kwenye beji kifuani mwake, alishangaa kwa muda nilipouliza kama ana uthibitisho wa kuunga mkono uchambuzi wake.
"Sibashiri," alisisitiza."Tunajua watu hawa ni akina nani, tunajua kuhusu maisha yao."

Mykhailo Podolyak, mshauri mwingine wa karibu wa Rais Zelensky, alikubali kulikuwa na "makundi kadhaa ya watu wanaotaka kuchukua mamlaka nchini Urusi".
Mfumo alioujenga Bw Putin, wa juu kwenda chini na wa kimabavu, alidai, ulibadilishwa na kukaribia pengo katikati ya mamlaka.
Afisa mwingine mkuu ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajwa, alifafanua zaidi, akipendekeza kuwa Rais Putin atalazimika kuwafuta kazi Waziri wake wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Valery Gerasimov, labda kama jibu la kizuizi kingine kijeshi.
Kuwafuta kazi watu hao wawili lilikuwa hitaji kuu la Yevgeny Prigozhin na waasi wake wa Wagner.
"Prigozhin atapata alichotaka," afisa huyo alitabiri. "Maisha yake ya kisiasa hayajakamilika. Hatasalia uhamishoni Belarus."
Kuhusu mashambulizi ya Ukraine, Bw Podolyak alisema maasi ya Wagner hayakudumu kwa muda wa kutosha kushawishi mapigano kwenye eneo la kilomita 1,800, ambalo ni refu zaidi - alisema - katika vita vyovyote tangu 1945.
Ni wazi kwamba Ukraine inapaswa kupigana kwa bidii sana, na kuchukua majeruhi katika wanajeshi wake na vifaa, ikiwa ni pamoja na silaha zinazotolewa na Nato.
Nilipomuuliza afisa huyo ambaye alitaka kutotajwa jina lake kuhusu mafanikio ya hivi majuzi ya kimbinu huko mashariki, ikiwa ni pamoja na vijiji vidogo vidogo, aliinua mkono wake huku kidole gumba kikibana hewa labda umbali wa nusu inchi.
Ujumbe wake ulikuwa kwamba maendeleo yamekuwa ya polepole, yenye uchungu na yenye mipaka, ingawa alionyesha matumaini ambayo yanaweza kubadilika.
Maafisa wakuu wa Ukraine bado wanafanya kila wawezalo kudhibiti matarajio kuhusu mashambulizi ya majira ya kiangazi.
Wanaamini baadhi ya washirika wao wa Magharibi, pamoja na wafuasi katika vyombo vya habari, wamefurahishwa sana na jeshi la Ukraine na zana zake za Nato.
Baadhi ya maafisa wa Ukraine walikiri hofu inayowafanya viongozi wa nchi za Magharibi kukosa usingizi, kwamba kuanguka hadharani kwa utawala wa Rais Putin kunaweza kusababisha hatari ya kweli kwani warithi wake watakuwa wakigombea madaraka katika jimbo lenye hazina kubwa zaidi ya silaha za nyuklia duniani.
Matarajio hayo ni hakika kwamba yatakuwa juu kwenye ajenda ya mkutano wa kilele wa Nato, watakapokutana huko Lithuania mwezi ujao.
Rais Zelensky na washauri wake wanataka mkutano huo kuwapa njia thabiti na isiyo na shaka ya uanachama wa Nato.
Wanaamini kuwa jibu bora kwa kukosekana kwa utulivu nchini Urusi ni kuwasilisha vikwazo kwa Moscow.
Lakini hali ya kutokuwa na uhakika inayomzunguka Rais Putin na serikali yake, karibu mwaka mmoja na nusu katika vita vibaya na baada ya kilichotokea kutoka kundi la Wagner, inaweza kuengeza wasiwasi wa nchi hizo za Nato ambazo wangependelea vita kumalizika kwa kuwa na meza ya mazungumzo, wala sio kwenye uwanja wa vita.















