Kutumia "mkono wa kushoto" haimaanishi ni mkono tu, bali pia viungo vingine

h

Chanzo cha picha, iStock

Muda wa kusoma: Dakika 7

Agosti 13 ni Siku ya Kimataifa ya Watu wa Kushoto, na bado haijafahamika ni kwa nini watu wanaotumia mkono wa kushoto wana uwezekano mdogo wa kutumia mkono wa kulia.

Hata hivyo, utafiti wa kisayansi wa jambo la " matumizi ya mkono wa kushoto," ambapo mkono wa kushoto hutumiwa zaidi ya mkono wa kulia, unaonyesha ukweli wa kuvutia juu ya wanadamu; kuanzia jinsi unaweza kubadilisha jinsi tunavyofikiria, kwa ukweli kwamba kuna wale kati yetu ambao wanaweza kuwa wanatumia "mkono wa kushoto," lakini mara hii kwa maana ya kusikia, na sio kwa mkono.

h

Chanzo cha picha, THINKSTOCK

Iwapo mtu ni mtumiaji wa mkono wa kushoto au la huwa wazi tangu utotoni , hasa kwakati anapoanza , huanza kushikilia kushika kalamu kuandika kwenye karatasi.

Lakini nini hufanya mkono mmoja kutawala juu ya mwingine, na kwa nini watu wanaotumia mkono wa kushoto huwa ni ni wachache?

Katika ripoti hii, tunajaribu kuchunguza sababu za jambo hili kisayansi na kihistoria ili kujifunza habari zaidi juu yake, na tuligundua haraka kuwa maelezo yanayohusiana na mada hii ni zaidi ya tulivyofikiria. Kwa mfano, hatukutambua hapo awali kwamba utegemezi wa mtu kwa mkono mmoja zaidi kuliko mwingine ni jambo ambalo pia linaenea kwa viungo vingine, pamoja na macho, kwa mfano.

Kila mmoja wetu anaweza kutambua kama yeye ni mtumiaji wa mkono wa kushoto kupitia majaribio yafuatayo:

Nyoosha mkono mmoja na ushikilie kidole gumba mbele yako. Kisha angalia kwa macho yote mawili na kisha kwa kila jicho kando wakati wa kufunika jicho lingine. Jicho lako lenye nguvu litakuwa lile linalokuruhusu kuona kidole karibu na muundo wake wa asili zaidi.

Unaweza pia kujaribu masikio yako ili kuona ni lipi unalotumia mara moja na kwa urahisi zaidi wakati wa kujibu simu.

Ni jambo la kushangaza kuona jambo hili likitokea katika maisha halisi. Mara nyingi, mimi hujikuta nikishikilia simu kwenye mkono wangu wa kushoto na kuiweka kwa shida kwa sikio langu la kulia, wakati ninaandika haraka maneno kwa na mkono wangu wa kulia.

f

Chanzo cha picha, THINKSTOCK

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa ujumla, asilimia 40 ya binadamu husikia vizuri kwa sikio letu la kushoto, asilimia 30 wanaona vizuri kwa jicho letu la kushoto, na asilimia 20 wana mguu wa kushoto wenye nguvu kuliko wa kulia.

Jambo la kushangaza ni kwamba asilimia ni ya chini sana linapokuja suala la wale ambao "wanatumia mkono wa kushoto", kwani asilimia yao haizidi 10% ya idadi ya watu. Sababu ya hii ni nini? Na kwa nini wao ni wachache miongoni mwetu?

Katika nyakati za kale, walifukuzwa kwa sauti kubwa na aibu kutoka kutoka kwenye safu za wanafunzi, kama watu walio kinyume na "njia ya asili." Kwa kweli, maelezo mabaya ya kushangaza yanayohusiana na mkono wa kushoto bado yanaendelea katika lugha zingine.

Neno la Kiingereza "kushoto" linatokana na neno la Anglo-Saxon ambalo liliandikwa kama lyft na lilimaanisha "dhaifu." Neno kinyume cha "kushoto" katika Kilatini ni dexter, maana yake "mkono wa kulia" na lilihusishwa na ustadi, uadilifu, uchamungu, na haki.

Kwa hivyo ni nini kinachoamua kuwa mtu atakuwa anatumia zaidi mkono wa kushoto? Kwa mtazamo wa mabadiliko, ni rahisi zaidi kufahamu sababu za kutumia mkono mmoja kuliko mwingine. Nyani huwa na uwezo wa kugawa kazi fulani kwa mkono mmoja.

Hebu tuchukue mfano hapa na wa nyani wanaowinda. Sokwe huchagua "mkono" ambao anaona unafaa zaidi kati ya viungo vyake, na kuuingiza kwenye shimo ambapo wadudu wanaishi, kwani hisia ya kugusa humpa habari nyingi juu ya kina na upana wa shimo na jinsi lilivyo na mchwa ambao wana ladha kwa aina hii ya tumbili.

Kisha sokwe huvuta "mkono" wake kwa urahisi, akifunua mawindo yake, ambapo hujaribu kulazimisha taya zake ndani ya shimo.

Kwa kutumia mkono huo huo kufanya kazi hii kila wakati humfanya sokwe kuwa na ujuzi zaidi na kumuwezesha kula idadi kubwa ya mchwa wakati huo pia.

Lakini utafiti uliofanywa na wanasayansi wa nyani na sokwe wa porini umeonyesha kuwa matumizi yao ya viungo vyao ni tofauti kabisa na yetu.

g

Chanzo cha picha, THINKSTOCK

Katika kila kazi ambayo watafiti waliifanya kuwahusu sokwe, ilionyesha kuwa nusu ya sokwe hawa walitumia "mkono wao wa kulia" kuifanya, wakati nusu nyingine walitumia mkono wao wa kushoto, yaani, uwiano wa asilimia 50 kwa 50, ambayo inatufanya tujiulize: Katika hatua gani katika mageuzi yetu wale wanaotumia mkono wa kulia kimsingi walionekana kuwa wengi zaidi kuliko wenzao wa mkono wa kushoto, Je, mtu mmoja kati ya kumi anatumia mkono wa kushoto?

Meno ya binadamu wa kale aina ya Neanderthals ni kiashiria muhimu katika suala hili. Inaonekana kuwa mtu huyu wa mapema alikuwa mwenye akili na mwenye busara kwa wakati mmoja.

Mababu zetu walitumia meno yao kushikilia vipande vya nyama ili waweze kuzikata kwa kisu kilichoshikiliwa katika mkono wao wa kulia.

Alama hii ya kushoto kwenye meno inayojulikana kama incisors ya mbele, na kwa kuchunguza alama hizi, wanasayansi waliweza kuamua ni mkono gani ulioshikilia kisu na ambao ulishikilia nyama.

La kushangaza, uchunguzi huu ulifunua kuwa uwiano wa mkono wa kushoto na mkono wa kulia kati ya wanadamu hawa wa zamani ulikuwa sawa na uwiano kati yetu leo: mmoja hadi kumi.

Hata hivyo, inajulikana kwamba kuna msingi wa maumbile. Hata hivyo, wanasayansi katika uwanja huu bado wanajaribu kutambua sehemu maalum za DNA zinazohusika na hili, na idadi ya jeni zinazoaminika kuwa na jukumu katika suala hili kufikia jeni 40 tofauti.

Kwa kuzingatia data ya sasa, hatuwezi kujua sababu maalum kwa nini watu wengine huwa wanatumia mkono mmoja zaidi kuliko mwingine, wala hatuna maelezo ya ni kwa nini "watu wa wanaotumia mkono wa kushoto" ni wachache, kwa hivyo jibu la swali lolote katika suala hili linabaki kuwa "hatujui kuhusu hilo."

Lakini je, kutumia mkono wa kushoto kuna athari yoyote kwa maisha ya mtu, isipokuwa ugumu - hata kidogo - katika kutafuta mkasi ambao umeundwa vizuri kwa matumizi na mkono wa kushoto wa mtu, au zipu ambayo mtu hawezi kufunga, au kalamu ambayo ni vizuri kwa moja?

f

Chanzo cha picha, THINKSTOCK

Kwa muda mrefu kumekuwa na mjadala juu ya ikiwa mkono wa kushoto huathiri ubongo kwa kwa namna yoyote au la.

Upande wa kulia wa ubongo hudhibiti mkono wa kushoto na kinyume chake. Kwa hivyo kutumia mkono wa kushoto zaidi kunaweza kuwa na athari zisizo za moja kwa moja-lakini zisizoepukika kwa njia ambayo ubongo umeratibiwa.

Katika muktadha huu, mwanasaikolojia Chris McManus wa Chuo Kikuu cha London, anayeandika kwa kutumia mkono wa kulia, na mkono wa kushoto, anasema: "Jinsi ubongo wa mtu anayetumia mkono wa kushoto unalivyopangwa ni tofauti sana."

Siku ya Kimataifa ya Watetezi wa Matumiazi ya Mkono wa Kushoto: Rozana Jamal aelezea uzoefu wake.

"Kitendo changu cha kibinafsi ni kwamba washikadau wa kushoto wana vipawa zaidi na wenye upungufu zaidi," McManus anaongeza. ‘’ Iwapo ni wewe, unaweza kujikuta na njia tofauti kidogo ya kuandaa ubongo wako, ambayo inaweza kukupa ujuzi ambao watu wengine hawana."

Lakini kuna wale ambao hawakubaliani. Miongoni mwao ni Dorothy Bishop, profesa wa saikolojia ya maendeleo ya ubongo katika Chuo Kikuu cha Oxford. Ana maslahi binafsi katika suala hilo: yeye pia ni hutumia mkono wa kushoto, jambo ambaloo anasema daima limemfanya ajiulize ni nini kilichomfanya kuwa tofauti.

"Kwa miaka mingi, kumekuwa na kila aina ya madai kwamba kuwa na mkono wa kushoto kunahusishwa na ulemavu kama vile dyslexia au autism," Bishop anaendelea. "Kwa upande mwingine, kumekuwa na uhusiano na sifa nzuri, na wasanifu na wanamuziki wanasemekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na matumizi ya mkono wa kushoto."

Lakini madai kama hayo yalionekana kutomridhisha Askofu baada ya kuangalia takwimu husika. Anasema mengi ya mawazo haya yanatokana na kile anachokiita "upendeleo katika kurekodi data fulani na sio za wengine."

Hapa anatoa mfano kwa kusema: Ikiwa mtafiti anafanya utafiti juu ya asili ya uvumbuzi, kwa mfano, na unajumuisha swali kuhusu uhusiano kati ya vigezo vya uvumbuzi, atahisi msisimko ikiwa atapata kisa kinachothibitisha kuwepo kwa uhusiano huo, bila kutaja visa vingine ambavyo havijathibitisha uhusiano wowote kati ya vigezo hivi viwili.

Bishop anaamini kwamba kutumia mkono wa kushoto kunaweza kuwa ni dalili badala ya sababu. "Udhaifu wa mkono wa kushoto wenyewe hauleti matatizo, inaweza kuwa dalili ya hali ya ugonjwa," anasema. Ukakamavu wa kushoto "hauna athari yoyote kwa maendeleo ya utambuzi kwa watu wengi," anasema.

Hata hivyo, mjadala bado unaendelea juu ya suala hili, na bado tunahitaji kujifunza mengi kuhusu asili ya ubongo wa mtu anayetumia mkono wa kushoto.

Sehemu ya tatizo ni kwamba wanasayansi wa neva, ambao hujifunza mambo mbalimbali ya tabia ya binadamu, hufanya masomo ya MRI tu juu ya watu ambao wana mkono wa kulia zaidi, katika jitihada za kupunguza tofauti kati ya masomo.

Kwa hivyo, mtu aliye mkono wa kushoto hastahili utafiti wowote wa kisayansi isipokuwa utafiti huu unapohusika naudhaifu wa kimatibabu.

Maarifa haya yaliwezekana kutokana na tafiti za kipaji zilizofanywa na Peter Huber, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Queen cha Belfast, kuchunguza harakati za kijusi ndani ya tumbo kwa kutumia kipimo cha ultrasound.

Uchunguzi huu ulifunua kuwa vijusi tisa kati ya kumi vilipendelea kunyonya kidole gumba cha mkono wao wa kulia, idadi ambayo ni sawa na asilimia ya watu ambao huwa wanatumia mkono sawa kwa idadi ya watu.

Mtafiti alipofuatilia hali ya vijusi hivi miaka mingi baada ya kuzaliwa kwake, aligundua kuwa wale walionyonya kidole gumba cha kulia tumboni walianza kupendelea kutumia mkono huo huo wakati wa maisha yao nje ya tumbo hilo, huku wale waliopendelea kunyonya kidole gumba chao cha kushoto walikuwa walitumia mkono wa kushoto katika maisha yao baada ya kuzaliwa.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi