Reece Nyawira: 'Watu hushangaa kwamba natumia mkono wa kushoto'
Je wajua kuwa ni karibu asilimia kumi ya watu duniani hutumia mkono wa kushoto kwa zaidi ya kulia.
Hivi leo kila mwaka huwa ni siku ya kusheherekea watu wanaotumia mkono wa kushoto.
Hata hivyo hali ina changamoto zake kwa watu wa aina hii ingawa wanajiona kuwa wa kipekee.
Mwandishi wa BBC jijini Nairobi Victor Kenani alizungumza na Reece Nyawira anayetumia mkono wa kushoto ambaye anaamini watu wanaotumia mkono wa kushoto ni watu wakipekee.
Anasema alikuwa na bahati kwamba wazazi wake hawakumzuia kuandika kwa mkono wa kushoto, ingawa anasema watu wengi hushangaa yeye huwezaje kuandika hivyo na kumuuliza iwapo hutembea kwa mguu wa kushoto pia.
Na salamu je, huwasalimia watu kwa mkono wa kushoto?