Hivi ndivyo ubongo unavyofanya kazi tunapokuwa wagonjwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Tunapoambiwa kwamba tutapata mafua, jambo la kwanza tunalofikiria ni dalili za kimwili: maumivu ya misuli, kikohozi na homa. Lakini, kinachotufanya tuhisi uchovu ni uchovu mwingi, muwasho wa pua na uchovu ambao unaonekana kama utakaa nasi milele.
Dalili hizi hujulikana kama tabia ya ugonjwa, na ingawa haifurahishi, ni muhimu.
Tabia ya ugonjwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Imegunduliwa kwamba dalili tunazopata wakati wa maambukizo ya virusi au bakteria sio tu athari za ugonjwa huo, lakini zinafanya kazi nzuri: zinaruhusu mwili wetu kuelekeza nguvu zake kwa kupambana na vimelea ambavyo vimetuvamia . Kwa maneno mengine, tunahisi vibaya ili kujisikia vizuri.
Lakini, tabia ya ugonjwa inaweza pia kuwa athari isiyohitajika kwa wagonjwa walio na saratani au magonjwa ya autoimmune (Ugonjwa wa ambao hutokea wakati mfumo wa ulinzi wa asili wa mwili hauwezi kutofautisha seli zako na seli za kigeni, na hivyo kusababisha mwili kushambulia seli za kawaida kimakosa)
Watu wenye magonjwa haya hutibiwa kwa dawa zinazojumuisha molekuli za kinga zinazojulikana kama interferon. Interferon huzalishwa na kutolewa na seli zetu za mfumo wa kinga wakati tunapopata maambukizi, lakini matumizi yake ya matibabu yanaweza kusababisha dalili hizi zisizofurahisha.
Kizuizi cha damu- ubongo

Chanzo cha picha, Getty Images
Ugonjwa huo unaathirije kazi ya ubongo na hali yetu ya kiakili?
Ili kujaribu kujibu swali la awali, lazima kwanza tuanzishe kizuizi cha damu-ubongo, muundo tata ambao kazi yake kuu ni kulinda seli za ubongo.
Kizuizi cha damu-ubongo ni mfumo wa kinga ambao huzuia vimelea vingi vya magonjwa na molekuli za kinga kuingia kwenye ubongo.
Imekuwa ikifikiriwa kwa muda mrefu kuwa kizuizi hiki pia huzuia ishara kutoka kwa mfumo wa kinga. Hata hivyo, leo tunajua kuwepo kwa mfululizo mzima wa taratibu zinazoruhusu maumivu fulani kuvuka kizuizi na kuathiri tabia ya ugonjwa.
Majaribio yaliyofanwa kwa panya hutuambia nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ili kufafanua jinsi maambukizi yanavyoweza kusababisha tabia ya ugonjwa huo, kikundi cha utafiti cha Ujerumani kilifanya utafiti ambapo waliweka panya kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa kwa muda mfupi.
Kisha wakatathmini athari za vimelea wanaosabaisha magonjwa kwa tabia ya ugonjwa kwa kutumia kipimo cha kawaida ili kugundua vinavyofanya kazi katika panya. Jaribio hili, linalojulikana kama Morris water, linajumuisha kuwaweka wanyama kwenye chombo cha maji ambapo lazima waogelee hadi wapate jukwaa linalowaruhusu kutoka.
Panya wenye afya kawaida hupigana hadi kufaulu, lakini wasio na afya hukata tamaa haraka na kuelea. Hapa inakuja jambo la kuvutia zaidi: panya zilizoambukizwa na virusi zilitumia karibu mara mbili wakati wa kuelea, na kupendekeza kuwa virusi vinabadilisha tabia zao ; Yaani walipokuwa wagonjwa walivunjika moyo sana.
Katika utafiti huu, iligunduliwa kuwa virusi viliwashawishi panya kutoa aina ya interferon-β, au kinga ambayo, kwa upande wake, huchochea molekuli zingine za vipokezi ambazo ziko katika miundo ambayo ni sehemu ya kizuizi cha ubongo-damu.
Jeni za urithi na tabia ya ugonjwa
Ili kubaini ikiwa vipokezi hivi vilivyo kwenye kizuizi cha damu-ubongo huchochea tabia ya ugonjwa, watafiti walilinganisha panya wa kawaida na panya ambao waliobadilishiwa vinasaba ambao hawakuwa na vipokezi hivi.
Kisha waliamilisha majibu ya kinga sawa na virusi kwenye panya na kuwafanyia majaribio ya kuelea. Ndani yake, panya waliorekebishiwa vinasaba walichukua takriban muda wa 50% chini wa kufikia jukwaa kuliko panya wa kawaida, na kuonyesha kuwa wale wa zamani hawawezi kukabiliwa na uchovu kwa vile hawakubeba vipokezi.
Jukumu la CXCL10 kwenye ubongo

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama tulivyosema, watafiti waliweza kutambua sehemu mbili za utaratibu ambao hupitisha ishara za kinga kupitia kizuizi cha ubongo-damu: interferon-β na vipokezi vinavyochochea. Lakini bado ilikuwa muhimu kuamua ni molekuli gani, katika mtiririko huu , uliosababisha mabadiliko katika ubongo.
Waligundua kwamba, kwa kukabiliana na interferon-β, seli za mishipa ya damu huzalisha molekuli nyingine: CXCL10, ambayo ina shughuli inayojulikana ya uchochezi katika magonjwa ya mishipa ya arthritis ya rheumatoid .
Kwa hivyo, waliweza kuelezea katika kiwango cha seli na msingi wenyewe wa tabia ya ugonjwa.
Maana muhimu ya kazi hii ni kwamba inafungua milango ya kutafuta njia za kuzuia tabia ya ugonjwa kwa wagonjwa wenye saratani au magonjwa ya autoimmune ambao hutibiwa na tiba ya interferon.
Hata hivyo, lililo wazi kwetu ni kwamba hisia ya kuwa mgonjwa si kero tu isiyo na kusudi. Dalili tunazopata ni sehemu muhimu ya mwitikio wa mwili wetu kwa maambukizo, ikiruhusu mfumo wa kinga kupambana na wavamizi.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












