Kwanini sisi hufa?

ggg

Kati ya viumbe wote wa ajabu wa majini ambao huzunguka katika bahari na mito yetu,bila shaka ungestaajabu kwa kumtizama sana kiumbe aitwaje hydra.

Alipewa jina hili lililotokana na nyoka wa kale wa Kigiriki wa mitholojia ambaye angeweza kukua tena vichwa vyake, ni jamii ya viumbe wengine kama jellyfish, anemones na matumbawe.

Ni mdogo kama mbegu ya mmea wa dandelion, akiwa na mwili mrefu na kizimba cha hema upande mmoja, hakuna mengi ya kuyaona. 

Lakini wana mali ya ajabu ambayo inawafanya kuwa na udadisi wa biolojia, wanaweza kuzaliwa upya. Ikiwa utawahitaji hydra katika vipande vingi, kila kidogo kitakua tena kuwa kiumbe kamili kipya. 

Tabia zao za kuzaliwa upya zimevutia shauku ya wanabiolojia kutafuta ushahidi wa kutokufa kwa asili. Kwa nini spishi hizi zinaonekana kutokufa kwa sababu za asili? Na je, kifo hakiepukiki? 

Uzee ulielezewa katikati ya Karne ya 20 kama biashara kati ya uzazi na matengenezo ya seli. Kwa kawaida, miili ya viumbe hai hutumia rasilimali zilizopo kwenye miili yao kukua na kutuweka tukiwa na afya njema kudumisha seli zetu.

 Kupitia utoto na ujana, mkazo ni juu ya kubaki hai na kuwa na nguvu na afya bora kadri iwezekanavyo. Baada ya ukomavu wa kijinsia, kipaumbele hubadilika kwa kuzaliana. Kwa sababu, kwa viumbe vingi, rasilimali ni ndogo, kutanguliza kuzaa watoto kunaweza kugharimu kudumisha afya. 

Chukua samoni ambaye ameogelea juu ya mto ili kuzaa na hufa mara moja baadaye. Kila kitu kinatumiwa ili kutoa nafasi nzuri zaidi ya kuifanya kwenye ardhi ya kuzaa, na mara moja huko hutengeneza fursa zaidi.

Uwezekano wa samoni kuogelea kurudi chini ya mto, kunusurika mwaka mwingine baharini, kufanya safari ile ile ya kurudi na kuzaa tena kwa mafanikio ni mbali sana hivi kwamba uteuzi wa asili hautawapendelea viumbe hawa. Na kwa hali yoyote, tayari wamepitisha jeni zao kwa mafanikio mara moja. 

Lakini ufahamu wa sasa wa kwa nini vitu hufa ni maalum zaidi. Viumbe vinapofikia ukomavu wa kijinsia, nguvu ya asili hudhoofika, na mchakato wa kuzeeka huanza, na kusababisha kifo. Lakini sio kuchukua nafasi kwa kizazi kijacho, ambacho kinaweza "kuvutia kutoka kwa mtazamo wa kujitolea", anasema Alexei Maklakov, profesa wa biolojia ya mabadiliko na biogerontology katika Chuo Kikuu cha Anglia Mashariki nchini Uingereza. 

Natural

Chanzo cha picha, NATURAL VISION/ALAMY

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika kipindi cha maisha yetu, jeni zetu hukusanya mabadiliko. Baadhi hutokea bila mpangilio kabisa, wengine ni matokeo ya milo yetu au mambo ya nje kama vile mwanga wa jua nk. Wengi hawafanyi chochote au wana madhara, wachache sana watakuwa na manufaa.

Kabla ya ukomavu wa kijinsia, "badiliko lolote la jeni ambalo linapunguza uwezekano wa kiumbe kuzaliana, au hata kuua kiumbe kabla ya kuzaliana, litachaguliwa kwa nguvu dhidi yake," anasema Gabriella Kountourides, mwanabiolojia wa mageuzi katika idara ya anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Oxford.

Mara tu kiumbe kinapofikia ukomavu wa kijinsia, hata hivyo, kinaweza kupitisha jeni zake kwa kizazi kijacho. Katika hatua hii, nguvu ya uteuzi wa asili hudhoofika. 

Kwa kuangalia utaratibu wetu wa kuzaa. Hufanya vizuri sana kuwafanya kuwa watu wazima na kuzaliana. Wazao wake watakuwa na nafasi ya kupigana ya kuzaa pia. Iwapo mabadiliko ya jeni yalitokea kwenye samoni yetu baada ya kuzaa ambayo iliongeza muda wake wa kuishi bila mpangilio na kumaanisha kuwa ilidumu mwaka mwingine (hata hivyo haitawezekana sana), watoto hao hawangekuwa na manufaa makubwa zaidi ya ndugu zao. Samaki wetu tayari ana kizazi kimoja (bila mabadiliko) huko alipo. 

Kuna faida kidogo, kutoka kwa mtazamo wa uteuzi wa asili, katika kuendelea na juhudi zinazohitajika ili kuwa na afya baada ya kuzaliana. Kwa hivyo, jeni zozote zinazowezesha suala hili haziko chini ya shinikizo la uteuzi ambalo lingesababisha kuwa kawaida zaidi. "kwa kawaida mtuu yeyote angependa kubaki hai. Lakini katika hatua hiyo, uteuzi wa asili haufanyi kazi kwa bidii juu yake, kwa sababu hakuna kitu zaidi cha kuendelea kutoa ili kuupa mwili uwezo wa kuendelea kuishi," anasema Kountourides. 

Mabadiliko mengi ya DNA yetu yatakuwa na matokeo mabaya au hayana matokeo yoyote. Miili yetu inaweza kurekebisha baadhi ya uharibifu huu wa DNA, lakini uwezo wetu wa kufanya hivyo huzorota kadiri umri unavyoongezeka kwa sababu ya kupungua nguvu ya asili. 

Lakini kuzeeka na kifo hutokea kwa njia mbili - mkusanyiko wa mabadiliko hasi kwa sababu ya uteuzi dhaifu wa asili na mabadiliko ambayo yanaweza kuwa ya manufaa kwa uzazi lakini ambayo yanakuwa mabaya kwa maisha marefu. 

Mfano mmoja wa mwisho unaweza kuwa mabadiliko ya jeni ya BRCA. Hizi zinajulikana kuongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya saratani ya matiti na ovari, lakini pia zimehusishwa na uzazi wa juu kwa wanawake wanaobeba mabadiliko. Kwa hivyo, inaweza kuwa kwamba mabadiliko ya jeni ya BRCA hutoa faida ya uzazi mapema maishani, ikifuatiwa na hatari kubwa ya afya baadaye maishani. Lakini kwa sababu uteuzi wa asili hudhoofisha baada ya ukomavu wa kijinsia, faida ya uzazi inazidi hasara. 

Pale ambapo seli huacha kugawanyika, kunaweza kuwa mfano mwingine wa faida ya maisha ya mapema ambayo ina hasara mwishoni. Senescence hutulinda dhidi ya saratani kwa sababu inaweza kuzuia seli iliyo na uharibifu wa DNA kuendelea kufanya kazi. Hata hivyo, seli za senescent zinaweza kujilimbikiza katika tishu, na kusababisha uharibifu na kuvimba, na ni watangulizi wa magonjwa yanayohusiana na umri. 

Arch

Chanzo cha picha, ARCH WHITE/ALAMY

Pia kuna maelezo kwamba baadhi ya spishi hufaulu zaidi kadiri umri unavyosonga - inajulikana kama "senescence hasi" - lakini ushahidi wa hili ni hafifu sana, anasema Maklakov. 

"Kama ikolojia ya spishi ni kwamba uzazi kwa sababu fulani kwa ujumla ni mdogo au huwezi kuzaliana mapema maishani hata kidogo, hii inabadilisha jinsi uteuzi unavyofanya kazi," anasema Maklakov. Mifano inaweza kupatikana kwa wanyama wanaozaa katika nyumba za wanyama - kwa mfano walrus au kulungu. Mwanaume mmoja anaweza kudhibiti kundi zima la wanawake. Ukubwa wa kundi hilo, na kwa hiyo idadi ya watoto anayoweza kuwa nayo, inaweza kuongezeka kwa umri na ukubwa wake. Kwa hiyo, uzazi unaendelea kuongezeka. 

Ingawa ni kweli kwamba baadhi ya spishi zinaweza kuhifadhi uwezo wao wa uzazi kulingana na umri, sio mifano ya kweli wakati mwingine, na tafiti ambazo zimedai kuwa nyingi zinaweza kuwa na dosari, anasema Maklakov. 

Lakini ngono inaweza kuchukua jukumu la kujua jinsi tunavyozeeka. Wanawake wanaofanya mapenzi mara kwa mara hucelewa kukoma hedhi, kulingana na utafiti wa Megan Arnot na Ruth Mace kutoka Chuo Kikuu cha London London. Wanapendekeza kwamba hii ni mfano wa biashara kwamba nguvu inayotumiwa wakati wa hedhi inaweza kutumika vyema na mwili wote ikiwa hakuna nafasi ya mimba. 

Kisha kuna aina ambazo muda wa maisha hutofautiana sana kati ya jinsia. Kwa kawaida, mchwa, nyuki na mchwa wana mfalme au malkia ambaye anaweza kuwa na nguvu nyingi na kuishi muda mrefu ikilinganishwa na wafanyakazi wao tasa. Kwa upande wao, kwa nini gharama ya uzazi haipunguzi maisha yao? Jibu linaweza kuwa kwamba mfalme au malkia amekingwa dhidi ya vitisho vingi vinavyowakabili wafanyakazi, na kuna tofauti kubwa katika mitindo yao miwili ya maisha hivi kwamba nadharia za kuzeeka hazitumiki kwao kwa usawa. 

Kwa hiyo ikiwa uzazi una uvutano mkubwa sana juu ya muda wetu wa kuishi, kwa nini wanadamu huishi kwa muda mrefu baada ya wengi wetu kuacha kuzaa? 

Dhana ya kuwa bibi inapendekeza kwamba ni muhimu kwa jamaa wakubwa kusalia hai kwa sababu uzazi ni biashara ya gharama kubwa na hatari. Bibi anaweza kuhakikisha uhai wa baadhi ya vizazi vyake mwenyewe kwa kuwekeza kwa wajukuu zake, na hivyo maisha marefu yanaweza kuleta manufaa kutokana na mtazamo wa uteuzi wa asili. "Familia ambazo zina bibi karibu zina uwezo wa juu zaidi wa uzazi, labda kwa sababu mama anaweza kuzingatia kupata watoto zaidi na bibi husaidia kulea watoto ambao tayari wapo," anasema Kountourides. 

Lakini kwa vile wajukuu wanashiriki 25% tu ya jeni zao na bibi yao, wana uhusiano naye sawa na yeye na wapwa zake. 

"Inaweza pia kuwa katika siku za nyuma wanawake hawakuwa wa kutosha kuweza kuzaa wakiwa na umri wa miaka 50. Na hivyo uteuzi wa kile kinachotokea kwa uzazi wa wanawake katika umri wa miaka 50 ulikuwa mdogo sana," anasema Maklakov. kurudi kwenye kanuni ya msingi ya kuzeeka ni kwamba baada ya kuzaliana nguvu ama uwezo wa asili huanza kudhoofu. Mengi ya yanayotokia katika maisha ya baadaye yanaweza yasiwe ya kufurahisha, lakini hakuna nguvu yoyote ya mageuzi kusaidia kutulinda dhidi yake.