Fujian: Meli ya kubeba ndege ya China inayoweza kuibua ushindani wa silaha baharini na Marekani

.

Chanzo cha picha, CCTV

Maelezo ya picha, Sehemu tambarare ya Fujian yenye manati za sumakuumeme huiruhusu kurusha ndege nzito zaidi, zinazobeba mafuta zaidi - na silaha.
Muda wa kusoma: Dakika 4

Chombo cha tatu cha kubeba ndege cha China, ambacho kilianza kuhudumu mnamo Novemba 2025, kitapita watangulizi wake wawili, wataalam wanasema, na kuifanya Beijing kukaribia kuafikia lengo lake la changamoto ya kutawala kwa Marekani katika eneo la magharibi la Pasifiki.

Meli hiyo kwa jina Fujian yenye uzito wa tani 80,000, iliyopewa jina la jimbo lililo karibu zaidi na Taiwan, inaweza kubeba hadi ndege 70, zikiwemo za kivita, helikopta na ndege za upelelezi - silaha zenye uwezo wa kugundua vitisho kutoka mbali, kuratibu ulinzi wa anga na kufanya mashambulizi ya uhakika.

Lakini zaidi ya kulipa jeshi la wanamaji la China kiwango kipya kabisa cha anuwai na kubadilika, mbeba ndege huyu pia hutoa taarifa ya dhamira ya kimkakati.

Ni meli ya kwanza ya China ilio na sumakuumeme, inayowezesha kurusha ndege nzito zaidi na kubeba mafuta zaidi - na silaha.

Kando na China, Marekani ndio nchi pekee ambayo ina uwezo huu.

"Hii inaziweka meli nyengine zinazobeba ndege nchini China katika kiwango kipya, ," Dk William C. Chung wa Taasisi ya Mafunzo ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama ya Taiwan aliiambia BBC News China.

"Bila shaka, muundo wake huboresha sana uwezo wa kupaa na kutua kwa ndege.

Vyombo vya habari vya serikali viliipongeza Fujian kama "hatua muhimu" katika maendeleo ya jeshi la wanamaji la China.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chombo cha pili cha kubeba ndege cha China, Shandong, bado kinategemea muundo wa kitamaduni wa "ski-jump" kwa ajili ya kupaa na kutua kwa ndege.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Dkt. Chung aliiambia BBC News China kwamba nchi hiyo sasa inaweza kushiriki katika "diplomasia ya vita vya maboti" sambamba na Marekani, baada ya kubadilisha, kwa maneno ya New York Times, kutoka "kujilinda kisasa" hadi "kuimarisha misuli yake katika safu ya mashambulizi".

Na kauli ya Rais Xi Jinping wa China, kwamba "Bahari ya Pasifiki ni kubwa ya kutosha Marekani na China," inahitimisha msukumo huu kuelekea kuleta usawa.

China imepanua jeshi lake la wanamaji kwa mwendo wa kasi chini ya Xi Jinping - na sasa ina meli nyingi kuliko nchi nyingine yoyote, na kuweka shinikizo kwa Marekani na washirika wake.

Bw Xi "aliamua kibinafsi" kwamba Fujian ilihitaji kutumia manati ya sumakuumeme, vyombo vya habari vya serikali vilisema.

Na aliongoza hafla ya kifahari ya uzinduzi katika kisiwa cha kusini cha Hainan, akikagua ndege na kuwasifu marubani kuwa mashujaa.

Akiwa amevalia sare ya kijeshi ya kijani kibichi, Xi Jinping alitoa hotuba kutoka kwenye sitaha kwa wanajeshi waliokuwa wakishangilia, akiimba: "Tii Chama, pigania ushindi na udumishe tabia njema ya maadili!"

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Taasisi ya Sera ya Mikakati ya Australia inaita Fujian "kizuizi cha haraka", chenye uwezo wa kusafirisha ndege za kivita na meli za kutua kwa uvamizi.

"Wakati wa amani, Fujian hutoa kizuizi sawa na wabebaji wa ndege za Marekani. Kwa muda mrefu, inaruhusu ufikiaji wa kimataifa, uwezekano wa kupelekwa Mashariki ya Kati, Afrika au Ulaya," Dk Chung aliiambia BBC News China.

Beijing kwa muda mrefu imekuwa ikiichukulia Taiwan inayojitawala kuwa sehemu ya eneo lake, na kuahidi "kuungana tena" na kisiwa hicho siku moja bila kupinga matumizi ya nguvu.

Dakta Satoru Nagao, wa Taasisi ya Hudson, taasisi yenye makao yake makuu mjini Washington, pia alidokeza kwamba meli ya Fujian ina uwezo wa kutishia ulinzi wa mashariki wa Taiwan kutoka kwa Pasifiki.

"Kutumwa kwa Fujian kutasaidia mashambulizi kwenye safu hizi za ulinzi," aliiambia BBC News Kichina.

Bado, vikosi vya Marekani katika vituo vya jeshi la majini huko Okinawa, Japan, Korea Kusini, Guam na hata Ufilipino vinaweza kushambulia kwa urahisi.

Bila kusahau meli 11 zinazobeba ndege za nyuklia za Marekani, zote zikiwa na hadi tani 100,000.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kinyume chake, Dkt. Chung alidokeza kwamba matumizi ya injini za dizeli za meli hiyo, pamoja na ukosefu wa bandari kubwa za ng'ambo, ina maana kwamba itahitaji ugavi wa mara kwa mara kutoka kwa meli za usaidizi - hatua inayopunguza uwezo wake wa makabiliano na meli nyengine .

Katika tathmini ya Fujian iliyochapishwa Oktoba 2025, Aita Moriki wa Taasisi ya Kitaifa ya Mafunzo ya Ulinzi ya Japan aliandika: "Bado kuna changamoto nyingi katika masuala ya teknolojia na wanajeshi ."

"Kwa maneno mengine," Dk. Chung aliiambia BBC News China, "uwezo wa jumla wa mapambano na uzoefu wa Fujian na wabeba ndege wengine wa China bado ni tofauti suna tofauti kubwa sana na ule wa jeshi la Marekani, ambalo limepigana vita."

"Wana meli tatu za kubeba ndege za kivita ilhali, tuna 11 - na tumedumisha hilo kwa miongo kadhaa," Admirali wa zamani wa Marekani Brett Mietus aliambia Washington Post mnamo Septemba 2025.

.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Chombo kikubwa zaidi cha kubeba ndege cha Jeshi la Wanamaji la Marekani, USS Gerald R Ford, kimesalia kuwa chombo kilichopiga hatua za juu zaidi duniani.

Hatahivyo uundaji wa makombora ya hali ya juu unaweza kuwa umepunguza umuhimu wa kijeshi wa meli za kubeba ndege za kivita.

Na hata kukiwa na manati za sumakuumeme, marubani bado wanalazimika kupaa na kutua kwa hatari kwenye sitaha ya meli iliyotikiswa na mawimbi.

"Iwapo teknolojia ya ndege zisizo na rubani za AI itakomaa, ndege hizo zitakuwa na umuhimu mkubwa na kuwa nguvu kuu," Dk. Nagao aliiambia BBC News Kichina.

Bado, picha za satelaiti zinaonyesha China imeanza kuunda chombo cha nne cha kubeba ndege za kivita.

Mipango ya kupanua zaidi meli hiyo inaendelea na, kulingana na wataalam, China itachukua hatua ya kuunda meli za kubeba ndege zinazotumia nyuklia.

Wataalamu pia wanatabiri ushindani wa silaha baharini kati ya Marekani na China.