Vyakula ambavyo hufai kula unapokuwa katika matibabu

Chanzo cha picha, Getty Images
Moja ya maswali mengi yanayoulizwa mara kwa mara ni iwapo ni hatari kunywa pombe wakati wa kutumia dawa aina ya antibiotics. Lakini kuna vinywaji na vyakula vingine vingi ambavyo tunapaswa kufahamu.
Tunachokula na kunywa kinaweza kuathiri sana dawa. Kwa hiyo, ni muhimu kusoma maelekezo ya kuchukua dawa.
Kama chakula, dawa husagwa ndani ya matumbo na kisha kwenye ini na zinaweza kuingiliana kwa njia ngumu. Baadhi ya vyakula vinaweza kuongeza athari za dawa, na vingine vinaweza kupunguza athari hiyo. Hatua zote mbili ni hatari.
Pombe

Chanzo cha picha, Getty Images
Dawa zingine, kama vile antihistamines na antidepressants, husababisha usingizi, na pombe inaweza kuongeza athari hii.
Lakini, matumizi ya pombe na dawa kwa wakati mmoja husababisha athari kama vile "upele " au "mzio wa disulfiram".
Wakati pombe inaposagwa mwilini , dutu yenye sumu inayoitwa acetaldehyde huundwa, na mwili huondoa dutu hii. Hata hivyo, baadhi ya dawa yanaweza kuzuia kuondolewa kwa simu hiyo mwilini yake na kusababisha mkusanyiko wake katika mwili; husababisha dalili kama vile kutokwa na maji mwilini, shinikizo la damu, mapigo ya moyo na kutapika.
Zabibu
Zabibu zimebainika kuingiliana na dawa zaidi ya 100, ambazo baadhi ni hatari. Kwa mfano, inajulikana kuongeza athari za dawa za kukabiliana na shinikizo la damu mara kadhaa.
Hii ni kutokana na dutu katika zabibu inayoitwa furanocoumarin.
Tunda la zabibu au glasi ya juisi ya balungi inaweza kuongeza athari za dawa zingine za kupunguza cholesterol kwa mara 13. Hii pia ina maana ya ongezeko la madhara.
- Dawa ambazo haziwezi kushirikiana na tunda la zabibu mwilini ni pamoja na
- Baadhi ya statins ambazo hupunguza mafuta (hasa yenye simvastatin);
- Dawa zinazoathiri mapigo ya moyo moyo;
- Dawa zinazotumika katika magonjwa ya akili
- Dawa zinazotumiwa kupunguza kasi ya mfumo wa kinga baada ya upandikizaji wa kiungo
- Dawa zinazoweza kuathiri tatizo la kusimama kwa uume.
Machungwa ya Seville na matunda ya pomelo pia yana furanocoumarin. Chungwa la kawaida halina dutu hii, lakini wakati mwingine linaweza kuathiri dawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mboga za kijani kibichi
Mboga za kijani kibichi kama vile kabichi, brokoli, mchicha, chard, flaxseeds, na baadhi ya mafuta ya mboga yana kiasi kikubwa cha vitamini K. Vitamini hii husaidia katika kuganda kwa damu.
Lakini , ikiwa unatumia diwa zinazozuia mgando wad amu kwa moyo wako na dawa za kupunguza damu kama warfarin , unapaswa kufahamu kuwa vyakula hivi vitapunguza athari za dawa hiyo.
Hali hiyo hiyo ilizingatiwa kwa mgonjwa ambaye alikunywa kiasi kikubwa cha chai ya kijani.
Hata hivyo, madaktari hawapendekezi kuacha mboga za kijani kabisa. Unahitaji tu kuwa mwangalifu usizidi kiwango cha kila siku ili vitamini K isiongezeke ghafla.
Mzizi wa licorice

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mizizi ya licorice nyeusi ina kemikali tamu sana iitwayo glycyrrhizin. Dutu hii inaweza kusababisha kupungua kwa viwango vya potasiamu, ongezeko la shinikizo la damu, na hata kwa watu wenye afya, usumbufu wa mapigo ya moyo.
Ikiwa una shinikizo la damu au ugonjwa wa moyo, unapaswa kuepuka mizizi ya licorice.
Amira, vyakula vya chumvi nyingi vilivyochachushwa, na jibini
Tyramine ni asidi ambayo husaidia kudhibiti shinikizo la damu na husagwa vizuri katika hali ya kawaida.
Hata hivyo, baadhi ya dawa za mfadhaiko zinazoitwa MAOIs (monoamine oxidase inhibitors) zinaweza kusababisha ongezeko la viwango vya tyramine mwilini, shinikizo la damu kuongezeka, mapigo ya moyo, maumivu ya kichwa, na hata kupooza.
Hii ni moja ya athari ambazo madaktari wanaogopa zaidi.
Bidhaa zinazotokana na Hamira kama vile tyramine, marmite, samaki, nyama, jibini , baadhi ya vileo; zinapatikana katika bidhaa nyingi za vodka, ikiwa ni pamoja na vyakula vilivyokaushwa, vilivyochomwa, na vilivyopchachushwa
Ingawa chokoleti, ambayo ina tyramine, pia imeripotiwa kuingiliana na dawa, hakuna ushahidi wa kutosha kuunga mkono hili.
Chai na kahawa
Kwa matibabu ya upungufu wa anemia ya chuma, chai, kahawa, mayai, maziwa na bidhaa za maziwa hazipaswi kutumiwa saa mbili kabla na baada ya kutumia vidonge vya sulfate ya chuma.
Hizi hupunguza unyonyaji wa chuma kwenye matumbo.
Inashauriwa kuchukua dawa hizi kabla ya kula chochote, na juisi ya machungwa au virutubisho vya vitamini C.
Makala hiyo imechukuliwa kutoka kwa mradi wa BBC "Trust Me I'm a Doctor".












