Vita vya Gaza: "Kundi la WhatsApp la familia yangu lipo kimya na kila mtu amekufa"

ggg

Chanzo cha picha, AHMED ALNAOUQ

Maelezo ya picha, Kati ya watoto wote kwenye picha hii, ni wawili tu ambao bado wapo hai

Majira ya saa kumi alfajiri Ahmed aliamka akiwa katika hali isiyo ya kawaida, japokuwa alitakiwa kulala usingizi mzito.

Ahmed alikuwa akiangalia hali ya baba yake na kaka zake katika eneo la Ukanda wa Gaza kupitia kikundi cha WhatsApp, licha ya ugumu wa kufanya hivyo kutoka katika eneo lake huko London, ambako anaishi.

Siku mbili zilizopita kulikuwa na ujumbe kutoka kwa dada yake, Aya.

Bomu liliharibu nyumba yake, na aliandika kwenye kikundi: "Milango na madirisha yamevunjwa." Aliongeza: "Jambo muhimu zaidi ni kwamba Mwenyezi Mungu ametuokoa sote."

Ahmed alimjibu, akisema: “Jambo muhimu ni kwamba upo salama. Kila kitu kinaweza kurekebishwa.”

Aya na watoto wake wanne walihamia kwenye nyumba ya babake huko Deir al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Ahmed alipoamka alfajiri, kundi hilo la Whatsapp lilikuwa kimya kabisa, jambo ambalo halikuwa la kawaida, isipokuwa baadhi ya ujumbe zilizokuwa zimefutika.

Ahmed alimpigia simu rafiki yake huko Gaza, na ndipo akapata habari kwamba familia yake yote ilikuwa imekufa.

ggg

Chanzo cha picha, ALNAOUQ FAMILY

Maelezo ya picha, Ahmed akiwa na familia yake

Tangu kuanza kwa vita, Ahmed na wenzake kutoka Gaza waliokuwa wakiishi naye walikuwa wakiteseka sana.

Simu zao zilishuhudia kiwango cha uharibifu na vifo kila siku, na kuwajulisha vifo vya jamaa na marafiki zao kila siku.

Lakini Ahmed hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angesoma kupitia simu yake habari za kifo cha familia yake yote. Nyumba yao huko Deir al-Balah haikuwahi kulengwa hapo awali.

"Nilifikiri ulikuwa wakati mbaya, wa kutisha kwao, lakini wangekuwa sawa mwisho wake," anasema. "Hivyo ndivyo nilivyofikiria."

Watu 21 wa familia yake wameuawa, ikiwemo watoto 15, dada zake watatu, na baba yake, wakati wa shambulio la anga la Israeli lililoharibu nyumba yao.

ggg

Chanzo cha picha, ALNAOUQ FAMILY

Maelezo ya picha, Ahmed na mtoto wa dada yake Abdullah 2019

Orodha ya waathirika ni ndefu, na inajumuisha watoto wengi, ambapo mkubwa kati yao anaitwa Islam, mtoto wa dada yake, ambaye alikuwa na umri wa miaka 13.

Alizaliwa wakati Ahmed alipokuwa kijana, na aliishi katika nyumba hii hii. Mama yake alikuwa akimtunza dada yake alipoenda kazini, na Ahmed alikuwa akimsaidia kumlisha.

Islam alitamani kuwa kama mjomba wake akiwa mkubwa, na alikuwa akijifunza Kiingereza kwa umakini, ili aweze kwenda Uingereza na kufanya kazi huko.

Ama Tala, ambaye alikuwa na umri wa miaka 9, na Nour, ambaye alikuwa na umri wa miaka 10, wao pia waliuawa pamoja na Islam wakati wa shambulio la bomu la Israeli katika nyumba ya Deir al-Balah, pamoja na dada zao Dima na Nasma, ambaye alikuwa na miaka miwili tu

ggg

Chanzo cha picha, ALNAOUQ FAMILY

Maelezo ya picha, Abdullah alifariki akiwa na umri wa miaka 6

Siku moja baada ya uvamizi wa Israel, Ahmed alichapisha picha ya kila mwathirika kutoka katika familia yake, wakiongozwa na Omar, ambaye alikuwa na umri wa miaka 3. Kisha dada yake akampigia simu kumwambia kwamba Omar bado yu hai. Ahmed anasema: "Huu ulikuwa wakati wa furaha zaidi maishani mwangu."

Omar alikuwa kitandani na wazazi wake, Shaima na Muhammad, wakati uvamizi wa Israeli ulipotokea. Muhammad aliuawa, lakini Shaima na Omar walinusurika kimiujiza.

Kwa upande wa Malak, ambaye ana umri wa miaka 11, alinusurika katika shambulio la bomu la Israel, na kuungua vibaya mwilini mwake, baada ya kuvutwa akiwa hai kutoka chini ya vifusi vya nyumba.

ggg

Chanzo cha picha, ALNAOUQ FAMILY

Maelezo ya picha, Malak alitolewa akiwa hai kutoka chini ya vifusi vya nyumba

Nilipokutana na Ahmed, alinionyesha moja kwa moja picha ya Malak, akipokea matibabu hospitalini, mwili wake wote ukiwa umefungwa bandeji. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni mvulana, kwa sababu nywele zake zilikuwa fupi, lakini alinielezea kuwa nywele zake zilikuwa ndefu kabla ya shambulio hilo, lakini zilichomwa moto.

Baba yake Malak hakuwepo nyumbani wakati wa uvamizi wa Waisraeli, lakini mke wake na watoto wake wawili walikuwepo.

Baada ya siku mbili za kukatika kwa mawasiliano huko Gaza, Ahmed aliweza kuwasiliana na familia yake tena na kujua kwamba Malak alifariki hospitalini kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu.

ggg

Chanzo cha picha, 4ALNAJJAR FAMILY

Maelezo ya picha, Uvamizi wa Israel ulimuua Yousef akiwa na umri wa miaka

Kabla ya mawasilianokukatwa huko Gaza, Ahmed alijua kwamba nyumba ya mmoja wa wajomba zake pia ilikuwa imepigwa bomu, na hakuweza kutambua waathirika.

Wengi wamepoteza jamaa zao huko Gaza, na familia nzima imeangamizwa. Familia zilipoteza ndugu 20, na wengine 44 walipoteza ndugu zao.

Yara Sharif, mbunifu wa mitindo wa Kipalestina anayeishi London, alinitumia picha za familia ya shangazi yake na nyumba yake, ambayo iliharibiwa katika shambulio la bomu la Israeli.

Alisema, "Ilikuwa nyumba nzuri sana, jumba la kifahari lenye ua mpana, na bustani kubwa nyuma."

ggg

Chanzo cha picha, ALNAJJAR FAMILY

Maelezo ya picha, Fatima, mwenye umri wa miaka 5, na Anas, mwenye umri wa miaka 3, wakiwa kwenye bustani ya nyumba yao kabla ya kuuawa katika shambulio la bomu la Israeli nyumbani kwao.

Watu 20 waliuawa katika shambulizi la bomu la Israel lililoharibu nyumba ya shangazi yake Yara, wakiwemo watoto 10.

Miili hiyo ilitolewa chini ya vifusi.

Wanafamilia wanaishi katika maeneo tofauti katika Ukanda huo, hawawezi kuhudhuria shughuli za mazishi wala kufanya mazishi yanayofaa kwa waliouawa.

Yara alipokea ujumbe kutoka kwa mmoja wa jamaa zake akisema: "Miili ya Muhammad na mama yangu bado ipo chini ya vifusi."

ggg

Chanzo cha picha, ALNAJJAR FAMILY

Maelezo ya picha, Abdul Rahman na pacha wake Omar

Hakuna mafuta ya kutosha katika Ukanda wa Gaza kuendesha mashine za kuchimba visima, kutafuta manusura au kutoa miili kutoka chini ya vifusi.

Nilipokuwa nikikutana na Ahmed Al-Jumaa, na tulikuwa tunatazama taarifa ya habari pamoja, na wakati tunapitia orodha ya waathirika, nilimuuliza ikiwa amepata majina ya ukoo wake, akajibu akisema: "Ni 12 tu. wao,” huku majina ya wengine 9 hayakutajwa, kwa sababu miili yao ilikuwa bado haijafukuliwa.

Wiki iliyopita, dadake mkubwa, anayeishi katika nyumba tofauti, alikwenda kwenye eneo la mabaki ya nyumba ya familia hiyo na kumwambia Ahmed kwamba hakukaa kwa muda mrefu kwa sababu hakuweza kuvumilia harufu ya miili iliyooza iliyokuwa ikitoka.

Tangu Ijumaa iliyopita, Ahmed hajaweza kuzungumza na dada yake yeyote. Simu hizo hazifanyi kazi, kwa hivyo hajui ni nini kilitokea na hawezi kupata maneno ya Kiingereza ya kutosha kuelezea jinsi alivyo na huzuni, anasema.

ggg

Chanzo cha picha, ALNAOUQ FAMILY

Maelezo ya picha, Islma, Abdullah, Raghad pamoja na Sarah

Miongoni mwa waliouawa ni mdogo wa Ahmed, ambaye jina lake ni Mahmoud.

Mahmoud alikuwa ametoka tu kupokea udhamini wa shahada ya uzamili huko Australia, na wiki moja baada ya kuanza kwa vita, alimwambia Ahmed kwamba hataki kwenda, kwa sababu ya hasira yake juu ya jinsi nchi za Magharibi zinavyoshughulikia suala la Palestina.

Aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter: “Moyo wangu hauwezi kuvumilia zaidi. Tunafanyiwa mauaji,” lakini aliuawa wiki moja baadaye.