Mauna Loa: Nini hutokea kwenye volkano kubwa zaidi duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mauna Loa, volkano hai kubwa zaidi duniani, inalipuka kwa mara ya kwanza tangu 1984.
Lava hutiririka chini ya kando ya volcano kwa joto la 1,000 ° C, lakini wataalamu wanasema hii bado haileti tishio kubwa kwa wenyeji.
Mauna Loa ina ukubwa gani?
Mauna Loa, ambayo ina maana ya "mlima mrefu" katika Kihawai, ni volkano kubwa zaidi duniani. uko kwenye maili za mraba 2,035 (kilomita za mraba 5,271) na ni moja ya msururu wa volkano tano zinazounda kisiwa kikubwa cha Hawaii.
Kilele cha Mauna Loa kiko mita 4,170 juu ya usawa wa bahari, lakini msingi wake uko chini ya bahari. Kutoka hapo hadi juu kuna mita 9,170, ambayo inafanya kuwa juu zaidi ya Mlima Everest.

Kwa nini Mauna Loa inalipuka?
Magma zimekuwa zikibubujika chini ya Mauna Loa na volkano za jirani kutoka "mahali penye moto" ndani kabisa ya Dunia. "Hakuna anayejua haswa kwa nini kuna sehemu hii ya joto," anasema Carmen Solana, mtaalamu wa volkano katika Chuo Kikuu cha Portsmouth nchini Uingereza.
"Lakini inaweza kusababishwa na kuoza kwa nyenzo za mionzi ndani ya vazi la Dunia." "Safu hizi za magma ziliunda jumla ya Visiwa vya Hawaii," anaongeza. Kama Solana anavyoeleza, Mauna Loa inapolipuka, magma hulipuka kwanza kwenye caldera, shimo lenye umbo la bakuli lililo juu ya volkano. Inaitwa Mokuaweoweo, ni eneo la kilomita za mraba 15 na kina cha mita 180.
Kisha magma hutoka kwenye "nyufa," kwenye mwamba, kando ya volkano na kutiririka chini ya mlima kama kioevu kinachoitwa lava. Ina nyuzi joto 1,000 na huwasha kila kitu kwenye njia yake.
Wakati volkano hulipuka, pia hutoa vitu vinavyopoa na kuunda vipande vya kioo vinavyoitwa "nywele za Pele." "Pele lilikuwa jina la mungu wa kike ambaye alidhaniwa kuishi Mauna Loa, na vipande hivyo ni vya rangi ya dhahabu," Solana alisema. "Alikuwa mwenye hasira," anaongeza.
Kwa nini mlipuko wa Mauna Loa ni muhimu?
Mauna Loa imelipuka mara 33 tangu 1843, ambayo ni tarehe ya mlipuko wa kwanza uliorekodiwa.
Kwa wastani, ni mlipuko kila baada ya miaka 5 na nusu. Hatahivyo, mlipuko wa mwisho ulikuwa karibu miaka 40 iliyopita.
"Kumekuwa na baadhi ya dalili za magma kulipuka katika miaka 10 iliyopita," anaeleza Andrew Hooper, Profesa wa Jiofizikia katika Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza, lakini hakujawa na mlipuko wowote kufikia sasa." Mlipuko wa sasa huko Mauna Loa unawapa kizazi kipya cha wanasayansi nafasi ya kusoma jinsi volkano hiyo inavyofanya kazi, anasema Profesa Hooper.

Chanzo cha picha, US GEOLOGICAL SURVEY
Je, mlipuko wa Mauna Loa ni hatari?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tofauti na volkano nyingi, Mauna Loa kwa kawaida haitoi milipuko inayolipuka , ambayo lava hurushwa hewani pamoja na majivu na gesi.
Badala yake, lava hutiririka polepole."Mitiririko ya lava sio hatari kwa maisha," anasema Prof Hooper, "kwa sababu unaweza kujiepusha nayo." "Pia, lava kutoka kwenye volcano haielekei magharibi kuelekea miji ya karibu, lakini kaskazini-mashariki.
Hulazimika kusafiri umbali mrefu kuelekea huko kabla ya kusababisha uharibifu mkubwa wa mali," alisema. Hata hivyo, wakazi wa eneo hilo wanaweza kukabiliwa zaidi na gesi zinazotolewa na Mauna Loa.
"Gesi za volkano, ikiwa ni pamoja na dioksidi ya salfa na klorini, hutoka ikiwa na unyevu hewani kutoa 'vog', ambayo ni ukungu wa volkano" kwa Kiingereza, anaelezea Solana.
“Hii inaweza kusababisha tatizo kwa watu kuwashwa macho na kusababisha matatizo ya kupumua,” anaongeza. Mamlaka ya afya ya Hawaii inasema ubora wa hewa unabaki kuwa mzuri lakini unaweza kuwa mbaya wakati wowote.
Ikiwa ndivyo, wakazi wa eneo hilo wanashauriwa kuepuka shughuli za nje na kukaa ndani na milango na madirisha kufungwa.













