Zijue paspoti 10 zenye nguvu Afrika 2024

fdvggf

Chanzo cha picha, Getty Images

Yamkini swali la kwanza litakuwa, pasipoti ama pasi ni nini? Hii ni hati au nyaraka inayotumika kwa ajili ya kumtambulisha mtu anapotaka kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine. Pasipoti ni mali ya nchi inayoitoa.

Ubora wa paspoti huamuliwaje? Kwa mujibu wa ripoti ya Hanley Passport Index, ya 2023 ili kuzijua paspoti zenye nguvu katika nchi za Afrika; wanatumia wingi wa nchi ambazo unaweza kwenda bila ya kuomba visa kabla ya safari, kama kigezo cha kujua paspoti yenye nguvu.

Barani Afrika kuna nchi 54. Makadirio ya mwaka 2023 ya Umoja wa Mataifa, bara hili lina zaidi ya wakaazi bilioni 1.4, ambayo ni sawa na asilimia 17 ya idadi jumla ya watu ulimwenguni.

Je, ni paspoti gani zenye nguvu katika bara hili?

dfffgfg

Chanzo cha picha, AFP

Ushelisheli

Nchi hii inaundwa na visiwa takribani 115, iko katika bahari ya Hindi – Mashariki mwa bara la Afrika. Inajuulikana kwa fukwe za kuvutia, nchi ya kijani na maarufu kwa kutembelewa na watalii wa kimataifa.

Kwa Afrika ni ya kwanza, kidunia ni ya 24. Ukiwa na paspoti ya Seychelles unaweza kusafiri nchi 155 bila ya kuomba viza kabla ya safari. Hii inatokana na nchi hiyo kuwa na uhusiano mzuri wa kidplomasia na makubaliano ya viza na nchi nyingi duniani.

Mauritius

Mauritius, ni nchi ya kisiwa katika bahari ya Hindi – Mashariki mwa bara la Afrika. Ni maarufu kwa fukwe za kuvutia. Nchi hii ina watu wapatao milioni 1.266 hadi mwaka 2021 kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.

Inashika nafasi ya pili barani Afrika kwa kuwa na paspoti yenye nguvu. Ulimwenguni ikishika nafasi ya 29. Raia wa taifa hilo, anao uwezo wa kusafiri katika nchi 148 bila ya uhitaji wa kuomba viza kabla ya safari.

Afrika Kusini

Inatambulika kuwa ni nchi iliyosonga mbele kwa maendeleo barani Afrika, ikiwa na uchumi imara. Afrika Kusini inaakizi eneo ilipo nchi hiyo kijegrafia, iko Kusini mwa Afrika, ikiwa na wakaazi wapatao milioni 60 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Ukiwa na pasopoti ya Afrika Kusini, unaweza kusafiri katika nchi 106 bila ya uhitaji wa kuomba viza kabla ya safari. Inashika nafasi ya 51 ulimwenguni miongoni mwa nchi zenye paspoti zenye nguvu.

Botswana

Nnchi isiyo na bahari – ipo kusini mwa bara la Afrika. Ina watu takribani milioni. Ni nchi ya tambarare, inapakana na Afrika Kusini upande wa Kusini na Kusini Mashariki, Namibia upande wa Magharibi na Kaskazini, Zimbabwe upande wa Kaskazini Mashariki. Na ule mpaka mdogo unaoiunganisha na Zambia katika daraja la Kazungula.

Ukiwa na viza ya nchi hiyo utapata kutembelea nchi 89 bila ya kutakiwa kuomba viza kabla ya safari. Uliwenguni iko nafasi ya 58. Sekta yake ya utalii inakuwa, kwa sababu ya utajiri wa mbuga za wanyama, mito na milima ya Tsodilo ambayo ni urithi wa dunia.

Namibia

Namibia iko kusini-magharibi mwa Afrika. Jangwa lililo pembeni ya bahari ya Atlantiki linapatikana katika nchi hii. Ni nchi yenye makovu ya ukoloni – majengo ya Wajerumani, katika mji mkuu Windhoek na mji wa wa pwani wa Swakopmund.

Paspoti yake itakuwezesha kusaifirisha nchi 81 bila ya kuomba viza kabla ya kuondoka. Ulimwenguni ina shika nafasi ya 62 Katika bara la Afrika, Namibia ni nchi ya tano miongoni mwa nchi zenye paspoti yenye nguvu.

Lesotho

Lesotho nchi ndogo isiyo na bahari na imezungukwa na taifa la Afrika Kusini katika mipaka yake yote. Kwa sehemu kubwa uchumi wake unategemea nchi ya Afrika Kusini. Ni nchi ya tatu kwa ukubwa miongoni mwa nchi zilizozungukwa na nchi nyingine.

Paspoti ya Lesotho ni ya 64 ulimwenguni. Katika bara la Afrika inashika nafasi ya sita. Raia wa nchi hiyo wanaweza kutembea katika nchi 79 bila ya kuhitaji kufanya mchakato wa kuomba viza wakati wanajiandaa na safari.

eSwatini

eSwatini nchi ndogo isiyo na bahari. Inafanana na na Lesotho. Awali ikijuulikana kama Swaziland. Inapakana na Mozambique kaskazini mashariki na mipaka iliyobakia imezungukwa na Afrika Kusini.

Eswahitini ni mwanachama wa nchi za jumuiya ya madola. Paspoti yake inashika nafasi ya 66 kwa nguvu ulimwenguni. Ukiwa na paspoti hiyo utakwenda katika nchi 77 bila kuomba viza kabla ya safari.

Malawi

Nchi inayopatikana Kusini Mashariki mwa bara la Afrika. Bonde kubwa la ufa (Great Rift Valley), limepita katikati ya nchi hiyo. Malawi ina utajiri wa wanyama pori, mito na mbuga za wanyama.

Ukiwa na paspoti ya Malawi utatembea katika nchi 75 bila kuhitaji kuomba viza kabla ya kusafiri. Paspoti ya nchi hiyo inashika nafasi 68 ulimwenguni.

Morocco

Morocco inapatikana kasakazini mwa Afrika.

Pasipoti ya Morocco inashikilia nafasi ya 73 duniani kulingana data ya kipekee kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA) - hifadhidata kubwa zaidi ya habari za usafiri kwa ushirikiano na shirika la utafiti ya Henley & Partners.

Ukiwa na pasipoti ya Morocco unaweza kusafiri nchi na maeneo 71 bila ya visa.

Tunisia

Kufikia Mei 2024, watu milioni 11.8 walio na pasipoti za Tunisia sasa wanaweza kusafiri hadi nchi 87.