Jinsi maisha ya walemavu wa Senegal yanavyobadilishwa na urekebishaji wa miguu

G

Huku Afrika ikifanya mkutano wake wa kwanza kuhusu kasoro zinazosababishwa kasoro za miguu – takriban mtu mmoja kati ya watu 800 kote duniani anazaliwa na 800 ulemavu wa miguu unaotokea wakat iwa kuzaliwa - BBC imetembelea kiliniki ya afya nchini Senegal kushuhudia tiba yenye kuleta mabadiliko inayobadili maisha

Mapema mwaka huu , Serigne mwenye umri wa miaka 14 , mvulana kutoka Senegal alikuwa anasita nyumbani. Alikuwa anaweza kutembea taratibu sana - alizaliwa huku miguu yake yote miwili iliwa imegeukia ndani – alikuwa anahisi aibu sana . Baadhi ya watu walikuwa wakimcheka kwa jinsi alivyokuwa akitembea , wengine walimuogopa na walikuwa wakimuita majiba ya kejeli.

Lakini sasa, chini ya miezi sita, migu yake imebadilika na ndoto yake ya kuichezea soka timu ya Senegal walau inaonekana inawezekana kwa sasa.

Miguu iliyopinda ya Serigne ina mifupa iliyoingia ndani ,ambayo pia inafahamika kama talipes, na leo ni hatua nyingine katika safari ya kurekebisha ulemavu huu.

 Kulingana na shirika la misaada la MiracleFeet, watu karibu milioni 10 wanaoishi leo walizaliwa na ulemavu huu unaofahamika kama clubfoot, na milioni nane kati yao hawajawahi kupokea matibabu.

Senegal imechelewa kwa kiasi fulani kutumia Ponseti – mbinu ya kwanza ya kurekebisha ulemavu huu iliyopewa jina la daktari Mhispania ambaye aliivumbua. Malawi na Uganda , kwa mfano walikuwa mbele ya nchi nyingi za Afrika katika kutambua uwezo wa tiba hii.

Lakini hii inamaanisha kwamba madaktari wa Senegal wameielewa vyema dhana asilia na sasa wanaitumia kuwatibu vijana wadogo au hata watu wazima ambapo walifikiri kuwa umri wao umekuwa mkubwa zaidi kiasi cha kutotibiwa.

 Mama yake Serigne anafurahia maendeleo ya kijana wake. Anafahamu vyema kuliko mtu yeyote jinsi mwanaye anavyoumia kutokana na ulemavu huu.

"Wakati mmoja alikataa hata kuondoka nyumbani kwa siku tatu. Ilinisababishia machungu sana . Lakini kwa sasa tuna furaha ."

G
Maelezo ya picha, Miguu ya Serigne kabla na baada ya kupata matibabu
G
Maelezo ya picha, Serigne sasa nahitaji mazoezi kidogo ya viungo kuimarisha miguu yake
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kama sehemu yambinu ya Ponseti, bandeji ndogo huwekwa kila wiki ili kurekebisha taratibu mguu na kuuweka katika nafasi nzuri. Kwasababu kisa hiki ni kibaya sana amekuwa akiwekewa bandeji 20 mguuni mwake kwa wiki nyingi, lakini wastani ni vifaa bandeji kati ya tano na nane.

 Kama ilivyo kwa visa vingi, karibu na mwisho wa matibabu yake alifanyiwa mdogo upasuaji unaohitajika wa kulegeza misuli ya miguu.

Tiba hii bado ni ya gharama ya chini, haihitaji kufanywa na mpasuaji mwenye ujuzi wa hali ya juu, n ani ya ufanisi - 90% ya watoto waliopokea usaidizi chini ya umri wa miaka miwili , miguu yao hueza kufanya kazi vyema, ingawa upasuaji unaweza kusababisha matatizo. Mabadiliko kusema kweli yanashangaza wakati unapoona picha za video za ulemavu wa Serigne kabla na baada ya kuanza kwa matibabu.

Siku chache zilizopita , Serigne aliwekewa bandeji ya mwisho. Baada ya hapo , atahitaji tiba ya mazoezi ya viungo kiasi ili kumsaidia awezae kujifunza kuubeba uzito wa miguu yake, na kwanza atahitaji kuvaa miguu badia ili kuiwezesha miguu yake kuwa katika mwelekeo mmoja kiasi, lakini maisha yake yajayo ni yanatia matumaini sana.

 Fatou, mtoto mwingine anayetibiwa katika kliniki ya Dakar amesafiri umbali wa maili 400 (644km) kupata matibabu sawa na haya kwa ajili ya mguu wake. Leo ametimiza umri wa miaka 13 lakini siku yake inaanza kwa kuondolewa kwa bandeji yake ya nne.

G
Maelezo ya picha, Fatou akibadilishiwa bandeji

Fatou anaelezea kwamba kwasbabu anaishi katika eneo la mbali zaidi lisiloweza kufikiwa kwa urahisi, hakuwahi kutarajia kuwa mguu wake utawahi kurekebishwa, kwahiyo ni mgonjwa mwenye furaha.

Imekuwa vigumu kwake kwenda shule – kuwaona wengine wakiruka na kukimbia - wakati Fatou hulazimika kutegemea magongo kutembea.

"Kila kitu nilichokitamani, sikuweza kukifanya. Lakini nitakapopona. Nitaweza kufanya kila kitu ninachokitaka."

 Hii ni pamoja na kufanyia kazi ndoto yake mpya ya kuwa daktari,alipata uzoefu mzuri sana hapa.

Hutembea kwa kuchechemea upande wa mguu wake maumivu yanamfanya asiweza kufika mbali. Maisha yake yamekuwa ya kunyanyapaliwa kutokana na miguu iliyopinda, na anafuta machozi akikumbuka maisha yake ya utotoni.

"Nilikuwa ninamuuliza mama yangu ni kwanini niko hivu? Alikuwa ananijibu ‘Ni mapenzi ya Mungu’ na 'Ulizaliwa hivi.'" Oumou amepitia uzoefu wa kuamini kuwa mambo yalivyo ndivyo yalivyopangwa, uzoefu ambao umezizuia familia nyingi za Wasenegal wengi kutafuta matibabu.

Anasema kipindi chake kigumu zaidi kilikuwa wakati alipokuwa katika umri wa kubalehe, wakati marafiki zake walipoanza kuvaa viatu vyenye visigino virefu, alilazimika kuvaa kandambili. Mwishowe alikatia masomo – kwasababu hakuweza kuendelea kudhalilishwa.

 Hata mbali ya wanafunzi wenzake maisha yalikuwa magumu. Ilimbidi akate tamaa ya kuendelea na kozi ya ushonaji wakati alipogundua kuwa kuendesha machine ya kushona kulikuwa kunamuumiza sana.

Oumou ana mume na watoto wawili kwahivyo maisha yake sio ya upweke kama wengine wengi ambao ulemavu wa aina hii ulivyowafanya, lakini bado anahisi kuwa anashindwa kufanya mambo mengi na ulemavu wake umemfanya asipate ajira. "Sifanyi kitu chochote cha maana ," analia.

Kwa bahati mbaya, kutokana na umri wake na upasuaji ambao haukufanikiwa , Oumou hawezi kupata tiba ya Ponseti. Baadhi ya watu wazima huweza kutibiwa vyema na tiba ya Ponseti, lakini ni vigumu zaidi kwao kutokana na kwamba miguu yao huwa haiwezi kupinda kwa urahisi.

Mara nyingi, sababu hasa ya kuzaliwa mtu akiwa amepinda miguu huwa haieleweki vyema, ingawa wavulana wana uwezekano mara mbili wa kuzaliwa na hali hii kulipo wasichana. Visa vingi vya hali hii duniani hutokea katika nchi zenye kipato cha chini au cha kati, kutokana na viwango vya juu vya uzazi, na ni katika nchi masikini zaidi ambako hali hii huwa hairekebishwi.

Mwanamke mmoja ambaye alijitolea maisha yake kuhakikisha kwamba ni watu wachache wanafikia umri wa utu uzima ndio wakiwa na ulemavu huu ni Aisha Mballo. Wakati tulipokutana naye, alikuwa akitembea katika soko la mji wa Thies, akiwa na kitabu kikubwa cha picha alichokuwa amekibeba chini ya kwapa lake . Kitabu kinafafanua ulemavu wa kupinda kwa miguu-clubfoot na jinsi mbinu ya Ponseti inavyoweza kuurekebisha. Amekuja hapa kutafuta visa vya clubfoot ambavyo vinginevyo haviwezi kugundulika.

Aisha anasema mguu wake mwenyewe "ulikuwa umepinda na kugeuka nyuma kabisa" hadi miaka ya 1990 wakati alipokuwa kijana mdogo, alipopelekwa nchini Marekani kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mgumu. Sasa anajitolea kama balozi wa shirika la msaada la MiracleFeet, linaloongoza juhudi za kuchunguza mapema watoto wachanga wanaozaliwa na hali hii.

G
Maelezo ya picha, Aisha (kulia) hutumia kitabu cha picha kuelezea jinsi ya tiba ya urekebishaji viungo-Ponseti, inavyofanya kazi

"Kama watu watatambua hali na kuwaondoa watoto wao mafichoni, tunaweza kuwapeleka hospitalini kwa ajili ya matibabu."

Rosalind Owen wa shirika la Global Clubfoot Initiative, ambaye amefanya uchunguzi kuhusu mtizamo wa clubfoot barani Africa, anasema kwamba tamaduni za jamii pale ni "matatizo makubwa ya unyanyapaa".

"Watu hufikiria ulilaaniwa, au ulirogwa, au labda wazazi wako walifanya kosa ."Anasema hii inaweza kuwa ni pamoja na madai, kwamba mama yako alizini, na hiyo ni adhabu.

 Bado, ni chini ya 20% ya visa vya clubfoot vinavyopewa matibabu wakati wa kuzaliwa nchini Senegal, kwa hiyo bado kuna mengi ya kufanya kuboresha hali za watu weny ulemavu huo.

 Kabla ya kuondoka, tunatmbelea kliniki nyingine kumuona mtoto mwenye miezi miwili ambaye anawekewa bandeji mpya ya kurekebisha mguu. Madaktari na wauguzi wanakamilisha kumuwekea bandeji kwenye miguu yake midogona kuweka bandeji nyingine laini juu yake.

 Huu ndio muda unaofaa wa kurekebisha ulemavu huu wa miguu - clubfoot.

Katika chumba cha kusubiri daktari, mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili, ambaye huenda akawa mwanasoka, anapiga teke boksi la juisi. Anayumba kiasi – kutokana na kwamba mguu wake mmoja bado umegeuka nyuma – lakini walau anapata matibabu anayohitaji.

Picha na maelezo zaidi ya taarifa na Gabriella O'Donnell na Nick Loomis