F-35 hadi KAAN: Kwanini Uturuki inawekeza kwenye ndege tofauti za kivita?

Birlikte uçan bir F-16 ve iki Eurofighter

Chanzo cha picha, Damian Lemanski/Bloomberg / Getty Images

    • Author, Onur Erem
    • Nafasi, BBC News Türkçe
    • Akiripoti kutoka, Londra
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Balozi wa Marekani nchini Uturuki ambaye pia ni Mwakilishi maalum wa Syria, Tom Barrack, alieleza kuwa msimamo wa nchi yake kuhusu nia ya Uturuki ya kurejea katika mpango wa ndege ya kivita ya F-35 na kumiliki mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 uliotengenezwa na Urusi haujabadilika.

Tom Barrack alisema katika chapisho la Novemba 9 kupitia mtandao wa X: "Kwa mujibu wa sheria za Marekani, Uturuki lazima isiendelee kutekeleza au kumiliki mfumo wa S-400 ili kurejea katika mpango wa F-35. Uhusiano mzuri kati ya Rais Trump na Rais Erdoğan umetengeneza mazingira mapya ya ushirikiano na umetuwezesha kufanya mazungumzo yenye tija zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita."

Sehemu ya kushangaza zaidi katika taarifa hiyo ilikuwa ni msisitizo wa Barrack kwamba Uturuki "haipaswi kumiliki" mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400 uliotengenezwa na Urusi.

Uturuki imekuwa ikifanya juhudi nyingi na kwa muda mrefu za kupata ndege mpya za kivita.

Wakati mazungumzo yakiendelea na Marekani kuhusu ndege za kivita za F-35 na F-16, tayari makubaliano yamesainiwa kati ya Uturuki na Uingereza kwa ajili ya ununuzi wa ndege zingine 20 aina ya Eurofighter. Awamu ya kwanza ya ndege hizi zitawasilishwa miaka mitano ijayo.

Lakini mazungumzo yanafanyika na nchi za Qatar na Oman kwa ajili ya ununuzi wa ndege zilizotumika aina ya Eurofighter

Uturuki pia inafanya kazi ya kuendeleza ndege yake ya kivita ya ndani, KAAN.

Mfumo wa anga wa Uturuki umepitwa na wakati

Katika mahojiano na BBC Turkish, mwanadiplomasia wa zamani na Mkurugenzi wa Kituo cha tafiti za uchumi na sera za sigeni (EDAM), Sinan Ülgen, alisema kuwa sababu kuu inayofanya Uturuki ihangaike na kununu ndege nyingi za kivita kwa wakati mmoja ni kuzeeka kwa mfumo wake anga upange wa Jeshi

Mara ya mwisho Uturuki ilinunua ndege 30 za F-16 mwaka 2012. F-16 zilizobaki kwenye orodha yake ni ndege za kizazi cha nne zilizonunuliwa mapema miaka ya 2000 au kati ya 1987 na 2000.

Mbali na F-16, Uturuki pia ina ndege za F-4. Hizi ni ndege za kivita za kizazi cha pili na cha tatu zilizoingia kwenye jeshi kuanzia miaka ya 1970.

Baadhi ya ndege za zamani zinaweza kuboreshwa. Kwa mfano, baadhi ya F-4 ziliboreshwa nchini Israel mwaka 1997.

Uturuki iliiomba Marekani mwaka 2021 kuboresha F-16 70, lakini iliacha mpango huo miaka mitatu baadaye, ikitangaza kwamba maboresho yatafanywa kwa kutumia rasilimali za ndani.

Mipango ilibadilika baada ya kuondolewa kwenye mpango wa F-35

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hatua hii inamaanisha nini kwa mkakati wa jeshi la anga la Uturuki?

Katika mahojiano na BBC , Dk. Aaron Stein, mtaalamu wa masuala ya Uturuki na rais wa taasisi ya Marekani ya Foreign Policy Research Institute (FPRI), alielezea hali ya sasa kama "kushindwa kwa utawala" na "vurugu":

"Nguzo kuu ya Jeshi la Anga la Uturuki ilikuwa ndege za F-35. Lakini Uturuki ilipoteza F-35. Tangu wakati huo, haijakuwa na mpango wazi na thabiti."

Stein anadai kuwa ingawa mipango ya ulinzi wa anga ya Uturuki inaonekana kuwa imara kwa mtazamo wa uhandisi, kukosa mpangilio kunafanya iwe "ya vurugu na isiyoeleweka" kwa jicho la usimamizi wa mipango.

Kwa mujibu wa Sinan Ülgen, hali hii inatokana na serikali kushindwa kupima ipasavyo matokeo ya ununuzi wa mfumo wa ulinzi wa anga wa S-400.

Uturuki ilikuwa imeweka mpango wake wa muda mrefu wa jeshi la anga kwenye ndege za F-35, ndege za kivita za kizazi cha tano. Ilitaka kuongeza zaidi ya ndege hizo 100 kwenye jeshi lake na pia ilikuwa mtengenezaji wa sehemu zake.

Hata hivyo, pale ilipoamua kununua ndege za S-400 licha ya onyo la Marekani, ushiriki wa Uturuki katika mpango wa F-35 ulisimamishwa mwaka 2019. Mwaka 2021, iliondolewa rasmi kwenye mpango.

Üz

Chanzo cha picha, Atilgan Ozdil/Anadolu Agency/Getty Images

Maelezo ya picha, Mwaka In 2018, marubani wa ndege wa Uturuki walipelekwa Marekani kujifunza namna ya kutumia ndege za F-35s

Aaron Stein anasema, "Ni taswira mbaya sana kujitoa kwenye mnyororo wa uzalishaji wa F-35 halafu kuomba kununua ndege hizi kutoka nje," na anaamini kuwa Uturuki haitaruhusiwa tena kununua F-35.

Sinan Ülgen anasema, "Binafsi, nilikosoa sana uamuzi wa kununua S-400 hata wakati huo, lakini pia nafikiri matokeo ya uamuzi huu hayakufanyiwa tathmini ya kina katika ngazi za juu."

Kwa mujibu wa Ülgen, kuzorota kwa uhusiano na Marekani pia ni sababu ya uamuzi wa Ututurik kununua Eurofighter.

Kwa kuwa F-16 zinapatikana, je Eurofighter ilikuwa ya lazima?

Aaron Stein anasema kwamba rada kwenye Eurofighter ambazo Uturuki itanunua ni bora zaidi kuliko zile zilizo kwenye F-16 zake za sasa.

Jambo jingine alilosisitiza Stein ni kwamba Eurofighter zina faida nyigni na kubwa kuliko F-16, katika ulinzi na pia mashambulizi.

Kwa mujibu wa Sinan Ülgen, faida nyingine ya Eurofighter ukilinganisha na F-16 ni kwamba hailazimishwi kupata risasi zake kutoka Marekani.

Uturuki itaweza kuzalisha risasi za ndani kwa ajili ya ndege za Eurofighter.

Uvamizi wa Urusi huko Ukraine umebadilisha mitazamo

Kwa mujibu wa Barın Kayaoğlu, msomi na mchambuzi wa mahusiano ya Uturuki na Marekani, kinachoendelea sasa duniani pia kimeathiri mazungumzo yanayoendelea ya ununuzi wa ndege za Eurofighter na F-16.

Akizungumza na BBC, Kayaoğlu anasema kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine mwaka 2022 umefanya nchi za Magharibi kutambua kuwa Uturuki ndiyo nchi muhimu zaidi iliyo pwani ya Bahari nyeusi.

Kwa mujibu wa Kayaoğlu, ununuzi wa ndege za Eurofighter na F-16 umeibuka tena kwenye ajenda baada ya washirika wa NATO kutambua tena umuhimu wao kwa Turuki.

Je Uturuki haiiamini NATO?

Swali linaulizwa kwa nini Uturuki haikutegemea ulinzi wa Kifungu cha 5 cha NATO hadi ndege yake ya kivita ya KAAN iingie rasmi kwenye matumizi miaka ya 2030

Kifungu hicho kinaasema kama nchi mwanachama wa NATO itashambuliwa, nchi zote wanachama watachukulia shambulio hilo kama shambulio dhidi yao wote, na hivyo kuja kuitetea.

Kwa mujibu wa wataalamu, swali hili lina majibu matatu: kutokuaminiana na NATO, ukosefu wa madhumuni ya ulinzi wa kipekee, na ushindani na mwanachama mwenzake wa NATO, Ugiriki.

Sinan Ülgen anasema yapo mashaka Ankara kuhusu kama NATO ingeweza kutoa msaada wa kutosha endapo ungehitajika.

"Hii shaka ipo sio tu Uturuki, bali pia katika nchi nyingi za Ulaya. Sababu ni msimamo wa sasa wa Marekani."

Ülgen anasisitiza kuwa ingawa NATO ingetarajiwa kutoa msaada waziwazi ikiwa Uturuki ingeshambuliwa na Urusi, haiwezi kusemwa hivyo kwa shambulio la Israel linaloweza kutokea.

Kwa mujibu wa Ülgen, Uturuki inahitaji ndege hizi si kwa ulinzi pekee, bali pia kuonyesha nguvu katika nchi za eneo lake kama Syria, Iraq na Libya.

"Uturuki imerekebisha mkakati wake kwa njia hii katika miaka 10 iliyopita. Kwa hiyo, inahitaji ndege hizi sio tu kwa kuzuia mashambulizi bali pia kujipa nafasi ya kiufundi katika matumizi ya nguvu", anasema Aaron Stein.

Kifungu cha 5 cha NATO kinatoa ulinzi tu dhidi ya mashambulizi kutoka nje ya muungano huo wa NATO.

Uturuki pia haitaki Ugiriki, mwanachama mwingine wa NATO, kuanzisha ubabe katika eneo la Bahari ya Aegean kutokana na ndege zake za kizazi cha 4.5 za Rafale na F-35 za kizazi cha tano.

Hivyo uturuki imeazimia kukidhi hitaji lake la ndege za kivita. Kwa mujibu wa Aaron Stein, ombi la Uturuki la kuboresha F-16 na ununuzi wa F-16 mpya linatokana na ushindani na Ugiriki katika Bahari ya Aegean.

Ukweli kwamba muda wa KAAN umekuwa ukicheleweshwa kwa miaka na kwamba bado haijaingia kwenye uzalishaji, pamoja na ukweli kwamba injini itakayotumika inapangwa kuanza kuzalishwa miaka ya 2030, unaongeza hitaji la Uturuki kununua ndege kutoka nchi nyingine.

Sinan Ülgen anasema kuwa mustakabali wa mpango wa ulinzi wa anga wa uturuki unategemea kama KAAN itaingia kwenye uzalishaji kwa wakati.

Ülgen pia anasema kwamba wakati Uturuki itaanza kutumia ndege za kivita za kizazi cha tano, dunia itakuwa tayari imehamia kwenye ndege za kizazi cha sita.