Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Chelsea sasa yamtaka mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo
Chelsea imesitisha mpango wa kumsajili beki wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, licha ya beki huyo wa Uingereza kupatikana kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Express)
Chelsea, hata hivyo, ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Antoine Semenyo na iko tayari kulipa takriban £78m kumpata mshambuliaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 25. (Fichajes - kwa Kihispania)
Beki wa zamani wa Tottenham na Manchester United Sergio Reguilon yuko kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa kushtukiza ili kuungana na Lionel Messi katika klabu ya Ligi Kuu ya Soka (MLS) Inter Miami baada ya mkataba wake na Spurs kumalizika majira ya kiangazi. (Mail)
Juventus ilikataa ofa ya takriban £58m kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz, 20. (TuttoJuve viaTeamtalk)
Arsenal pia hawajakata tamaa katika harakati zao za kumanasa Yildiz na walituma maskauti wao kumfuatilia wakati Juventus ilipocheza na AC Milan katika mechi ya Ligi Kuu ya Italia maarufu Serie A Jumapili. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)
Mshambulizi wa Manchester United Joshua Zirkzee, 24, anafikiria kusalia katika Ligi ya Premia ikiwa ataondoka Old Trafford, huku akipigiwa upatu kujiunga na Everton au West Ham. (Team talk)
James Ward-Prowse, 30, anajiandaa kuhama West Ham katika usajili wa majira ya baridi, baada ya kocha Nuno Espirito Santo kukosa kumtumia. (FootballInsider)
Beki wa Uruguay Ronald Araujo alikataa nafasi ya kuondoka Barcelona msimu wa kiangazi - mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliazifahamisha klabu zinazomuwania ikiw ai pamoja na Chelsea, Liverpool, Tottenham na Juventus kwamba anataka kusalia katika uga wa Santiago Bernabeu (Sport - kwa Kihispania)
Lakini Barcelona huenda wakamuuza Araujo mwezi Januari, baada ya kuweka bei ya takriban £35m kwa mlinzi huyo. (Fichajes - kwa Kihispania,)
West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Endrick kwa mkopo lakini watakabiliwa na ushindani kutoka kwa Valencia na Real Sociedad kuwania saini ya mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 19 mwezi Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)
Arsenal wana matumaini ya kufikia mkataba mpya na Bukayo Saka, 24, wakati wa mapumziko ya kimataifa ili kumbakisha winga huyo wa Uingereza kwa muda mrefu. (TBR Football)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi