Ndege inyotumia gesi ya hidrojeni yafanyiwa majaribio

.

Chanzo cha picha, WRIGHT ELECTRIC

Maelezo ya picha, Ndege ambayo ya siku zijazo ambayo haichafui mazingira

Katika kona yenye upepo mkali katika kambi moja ya kijeshi huko Salisbury , injini ndogo ya ndege inafanyiwa majaribio ambayo siku moja yanaweza kusababisha mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga.

Injini yenyewe ni ya kawaida kabisaa. Ni turbine ya gesi ya Rolls-Royce AE-2100A, muundo unaotumiwa sana kwenye ndege za safari fupi kote ulimwenguni.

Jambo lisilo la kawaida kabisa juu yake ni mafuta yanayotumiwa. Hii ni mara ya kwanza kwa injini ya kisasa ya ndege kuwahi kuendeshwa kwa gesi ya hidrojeni.

Huku nyaya zake na bomba zikiwa wazi, mashine hiyo imefungwa kwa usalama kwenye rigi thabiti ya majaribio, huku wahandisi wakikusanyika kuzunguka eneo la skrini kwenye chumba cha kudhibiti, usalama.

Majaribio hayo yanafanywa na kampuni ya Rolls-Royce, kwa ushirikiano na shirika la ndege la easyJet

.

Chanzo cha picha, Roll Royce

Maelezo ya picha, Hadi sasa injini inaendesha kwa kasi ya chini kwa kutumia hidrojeni

Kampuni hiyo inaamini kuwa nishati ya hidrojeni inatoa nafasi bora zaidi ya kupunguza hewa chafu kutoka kwa usafiri wa muda mfupi wa angani.

"Tulianza miaka michache iliyopita kuangalia kile ambacho kinaweza kuendesha ndege za siku zijazo," anaelezea David Morgan, afisa mkuu wa uendeshaji wa easyJet.

"Tuliangalia teknolojia ya betri, na ilikuwa wazi kuwa teknolojia ya betri labda haitafanya hivyo kwa ndege kubwa ya kibiashara ambayo tunaendesha.

"Tumefikia hitimisho kwamba hidrojeni ni pendekezo lenye matumaini sana kwetu."

Faida ya hidrojeni ikilinganishwa na betri ni kwamba hutoa nguvu zaidi kwa kilo. Betri nzito zaidi zinahitajika kuwasha ndege kubwa.

Huku usafiri wa anga wa ktumia hidrojeni ukiwa uko mbali kuafikiwa. Majaribio yaliyofanywa hadi sasa yameonyesha tu kwamba injini ya ndege inayotumia haidrojeni inaweza kuwashwa na kukimbia kwa kasi ya chini.

.

Chanzo cha picha, Roll Royce

Maelezo ya picha, Mafuta ya haidrojeni ni pendekezo "la kusisimua" anasema David Morgan, afisa mkuu wa operesheni wa easyJet

Lakini kutoka hapo hadi kujenga injini mpya kabisa, yenye uwezo wa kuwezesha ndege ya abiria kusafiri kwa kwa usalama itahitaji utafiti mkubwa zaidi - na uwekezaji mkubwa.

Ndege yenyewe pia itahitaji kuundwa upya. Haidrojeni, hata ikiwa katika hali ya kumiminika, huchukua nafasi mara nne zaidi ya mafuta ya taa yanayohitajika kuruka umbali sawa.

Hali hiyo italazimu gesi hiyo kupozwa hadi -253C. Kisha, kabla ya kuchomwa moto, lazima igeuzwe tena kuwa gesi.

"Kuna mabadiliko makubwa kutoka kwa mtazamo wa ndege," anasema Alan Newby katika Rolls-Royce.

"Watalazimika kuwa na tanki iliyo na hidrojeni itakayohifadhiwa katika baridi kali.

"Halafu kuna suala la jinsi ya kuipeleka gesi hiyo kwa injini pia."Alan Newby, Head of Future Aerospace, Rolls Royce

.

Chanzo cha picha, Roll Royce

Maelezo ya picha, Hidrojeni inahitaji hifadhi na nafasi zaidi kuliko mafuta ya ndege
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Swali lingine muhimu ni wapi hidrojeni yenyewe inatoka, kwa sababu hiyo itakuwa na athari kubwa juu ya faida za mazingira inayoweza kutoa.

Mafuta yaliyotumiwa katika majaribio hayo yanaitwa hidrojeni ya kijani inayozalishwa katika Kituo cha Nishati ya Bahari ya Ulaya katika Visiwa vya Orkney.

Inapatika kwa kutumia umeme unaogawanya maji katika vipengele vyake, hidrojeni na oksijeni. Umeme unaohitajika hutolewa kwa kutumia nguvu ya mawimbi na upepo. Hii inayafanya kuwa mafuta safi kabisa.

Lakini hidrojeni nyingi zinazozalishwa kwa ajili ya matumizi ya viwanda siku hizi zinapatikana kutokana na mchakato unaohusisha kuchanganywa kwa mvuke wa joto la juu na gesi asilia chini ya shinikizo la juu.

Hatahivyo, hii hutoa kiasi kikubwa cha hewa ya kaboni, ambayo huachiliwa angani. Pia inahitaji kiasi kikubwa cha nishati - ambayo mara nyingi hutolewa kwa kuchoma mafuta.

Njia moja mbadala ni ile inayojulikana kama hidrojeni ya bluu. Hii inazalishwa kwa njia ile ile, lakini kaboni dioksidi inachukuliwa na kuhifadhiwa au kutumika tena.

.

Chanzo cha picha, Roll Royce

Maelezo ya picha, Shida nyingi za uhandisi zinapaswa kutatuliwa ili kufanya hidrojeni kufanya kazi kama mafuta, anasema Alan Newby kutoka Rolls-Royce.

Hii inapaswa kuifanya gesi hiyo kuwa safi, mafuta yalio na kaboni ya kiwango cha chini. Lakini mtazamo huo ulipingwa na watafiti katika vyuo vikuu vya Cornell na Stanford mwaka jana.

Walipendekeza kwamba kwa kweli, kutumia hidrojeni ya bluu bado kunaweza kuwa na madhara zaidi kwa sayari kuliko kuchoma mafuta.

"Kwa sasa kuna sifa nyingi za hidrojeni," anasema Matt Finch, mkurugenzi wa sera ya Uingereza kuhusu kikundi cha kampeni ya Usafiri na Mazingira.

“Watu wengi wanasema ‘tunaweza kutumia haidrojeni, tunahitaji hidrojeni’ unasikia kwa magari, kwa malori, kwa meli, kwa ndege, kwa kupasha joto nyumbani, kwa kemikali.

"Kwa sasa Uingereza inazalisha haidrojeni ya kijani kibichi isio na uchafuzi wowote wa mazingira. Ili kutimiza mahitaji yote ambayo kila mtu anataka haiwezekani kabisa."

Bw Finch anaamini kuwa hii ina maana kwamba ugavi wa hidrojeni ya kijani huenda ukafanyika miongo kadhaa ijayo, na anasema usafiri wa anga hauwezi kuwa kipaumbele kwa serikali.

Haya yote yanamaanisha kuwa kupatikana kwa ndege zitakazotumia gesi ya kaboni isio na uchafuzi wowote wa mazingira kutachukua miongo kadhaa .

Hata ifikiapo wakati huo kutakuwa na masoko machache, angalau kwa kuanzia. Katika njia za masafa marefu, mafuta yaliyotengenezwa yanatarajiwa sana kutoa suluhisho.

Majaribio haya ya kwanza Salisbury Plain siku moja yanaweza kuonekana kama hatua za kwanza, kuelekea mapinduzi ya kiteknolojia katika tasnia ya usafiri wa angani.