Fahamu miji 10 bora zaidi ya kuishi duniani 2022

Vienna

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vienna

Vienna kwa mara nyingine tena imeorodheshwa nambari moja kuwa jiji bora zaidi duniani kuishi, kulingana na ripoti inayotolewa kila mwaka na jarida la Uingereza la The Economist.

Mji mkuu wa Austria ulijishindia taji hilo kutoka Auckland huko New Zealand, ambayo ilishuka hadi nafasi ya 34, kwa sababu ya hatua kali ilizoweka kukabiliana na janga la corona kulingana na ripoti hiyo.

Vienna ilikuwa imepoteza nafasi yake mwaka uliopita kutokana na kufungwa kwa majumba yake ya makumbusho na migahawa kutokana na janga la corona lakini ufunguzi wa Maisha yake ya kitamaduni iliurudisha katika nafasi iliyokuwanayo miaka 2018 na 2019.

Katika nafasi ya pili ilikuwa mji wa Copenhagen Denmark , nafasi ya tatu ulikuwa mji wa Zurich Switzerland nafasi ya nne na ya tano ukaiweka miji miwili ya Canada , Calgary na Vancouver mtawalia.

Miji 10 bora kuishi duniani

  • Vienna (Austria)
  • Copenhagen (Denmark)
  • Zürich (Switzerland)
  • Calgary (Canada)
  • Vancouver (Canada)
  • Geneva, Switzerland)
  • Frankfurt (Germany)
  • Toronto Canada)
  • Amsterdam (Netherlands)

Osaka (Japan) na Melbourne (Australia)

Chanzo: The Economist

Miji hiyo imepewa hadhi hiyo kwasababu ya uthabiti wake, uwezo wake wa kukabiliana na matatizo ya Kiafya, kitamaduni , kimazingira, kielimu na miundombinu

Lakini ni nini kinachoufanya mji wa Vienna kuwa mji bora wa kuishi?

Miji wa Auckland ulitoka katika nafasi ya kwanza hadi nafasi ya 34 mwaka huu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miji wa Auckland ulitoka katika nafasi ya kwanza hadi nafasi ya 34 mwaka huu

Kulingana na waandishi wa ripoti hiyo , uthabiti, na miondombinu mizuri ndio sababu kuu ya wakazi kuishi katika mji huo ikiwemo vituo vizuri vya kiafya na fursa nyingi za burudani na utamaduni.

Masuala mengine muhimu

Ukitaka kujua ni miji gani muhimu ya watu kuishi , ripoti hiyo inaorodhesha miji 10 mibaya zaidi kuishi.

Kutoka chini (miji mibaya zaidi) hadi juu ni: Damascus (Syria), Lagos (Nigeria), Tripoli (Libya), Algiers (Algeria), Karachi (Pakistan), Port Moresby (Papua New Guinea), Dhaka (Bangladesh), Harare ( Zimbabwe), Douala (Cameroon) na Tehran (Iran).

Katika orodha hiyo mji wa London, upo katika nafasi ya 3, Paris katika nafasi ya 19, New York nafasi ya 51, Barcelona na Madrid zikiwa katika nafasi ya 35 na nafasi ya 43 mtawalia.