Huw Edwards atajwa kama mtangazaji katika tuhuma za malipo ya picha za utupu

th

Vicky Flind, mke wa mtangazaji wa habari Huw Edwards, amemtaja kama mtangazaji wa BBC anayekabiliwa na tuhuma za malipo ya picha chafu za utupu katika taarifa iliyotolewa kwa niaba yake.

Hii hapa taarifa kamili ya Vicky Find

"Kwa kuzingatia ripoti ya hivi majuzi kuhusu 'Mtangazaji wa BBC' ninatoa taarifa hii kwa niaba ya mume wangu Huw Edwards, baada ya siku tano ngumu sana kwa familia yetu.

"Ninafanya hivi kimsingi kwa kujali hali yake ya kiakili na kuwalinda watoto wetu.

"Huw anasumbuliwa na matatizo makubwa ya afya ya akili. Kama inavyothibitishwa, amekuwa akitibiwa kutokana na mfadhaiko mkubwa katika miaka ya hivi karibuni.

"Matukio ya siku chache zilizopita yamezidisha hali na kuwa mbaya, amepata tukio lingine mbaya na sasa anapokea huduma ya hospitali ya wagonjwa ambapo atakaa hospitali kwa siku zijazo.

"Mara tu ya atakapokuwa katika hali nzuri ya kufanya hivyo, anakusudia kujibu taarifa ambazo zimechapishwa.

"Ili kuwa wazi Huw aliambiwa kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na tuhuma zinazotolewa dhidi yake Alhamisi iliyopita.

"Katika hali hiyo na kutokana na hali yake ya sasa , ningependa kuuliza kupewa faragha ya familia yangu na kila mtu mwingine aliyepatikana katika matukio haya ya kukasirisha iheshimiwe.

"Ninajua kwamba Huw anasikitika sana kwamba wenzake wengi wameathiriwa na uvumi wa hivi majuzi wa vyombo vya habari. Tunatumai taarifa hii itamaliza hilo."

Huw Edwards ni nani?

Huw Edwards, 61, ni mmoja wa watangazaji maarufu wa BBC.

  • Amefanya kazi na BBC kwa miongo minne, ikiwa ni pamoja na miongo miwili kama mtangazaji mkuu wa habari za BBC saa kumi kamili.
  • Ametangaza matukio mengi muhimu, ikiwa ni pamoja na kifo na mazishi ya Malkia Elizabeth II, harusi ya Prince William na Kate na Prince Harry na Meghan, Sherehe za Diamond na Platinum Jubilee za Malkia na kuapishwa kwa Rais wa Marekani Barack Obama na kifo cha Nelson. Mandela
  • Alilelewa Wales na alisoma katika Chuo Kikuu cha Cardiff ambapo sasa ni profesa wa heshima wa uandishi wa habari.
  • Yeye ni mmoja wa wafanyikazi wanaolipwa zaidi BBC, akipata kati ya £435,000 na £439,999 kwa 2022/23.
  • Anaishi London na mke wake na watoto watano
  • Edwards amezungumza siku za nyuma kuhusu mapambano yake na msongo wa mawazo

BBC 'kusonga mbele' na uchunguzi

BBC imetoa taarifa yake kufuatia idara ya polisi ya Met kusema hakuna ushahidi wa kosa la jinai:

“Tumeona taarifa ya polisi ikithibitisha kuwa wamekamilisha tathmini yao na hawachukui hatua zaidi. Tunawashukuru kwa kukamilisha kazi hii kwa kasi.

"Polisi walikuwa wametuomba hapo awali kusitisha uchunguzi wetu na sasa tutaendelea na kazi hiyo, kuhakikisha mchakato unaofaa na tathmini ya kina ya ukweli, huku tukiendelea kuzingatia jukumu letu la kutoa huduma kwa wote wanaohusika."