Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Tuko pale tunapotaka kuwa' - Arsenal baada ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Mnamo Machi 9, 2010, Nicklas Bendtner alifunga penati na kuhitimisha hat-trick yake katika ushindi wa 5-0 wa Arsenal dhidi ya Porto kwenye Ligi ya Mabingwa, huku The Gunners wakithibitisha kufuzu kwa robo fainali kwa kubadili upungufu wa mkondo wa kwanza.
Imechukua miaka 14 na siku tatu, lakini Arsenal wamerejea katika hatua ya nane bora ya Ligi ya Mabingwa - wakiwa na Porto, mikwaju ya penati na mechi ya mkondo wa pili kwa mara nyingine tena kwenye hati.
Safari hii, si mfungaji wa penati aliyegongwa vichwa vya habari bali ni mlinda lango, David Raya aliyewanyima Porto nafasi ymara mbili katika ushindi wa 4-2.
Arsenal waliponea baada ya kufungwa bao 1-0 nchini Ureno katika dakika za mwisho, huku bao la Leandro Trossard likilazimisha muda wa ziada katika mchuano mkali ingawa ubora wa mchezo ulikuwa chini.
Lakini Raya aliporuka upande wake wa kushoto kushika mkwaju wa penati wa Galeno, mashabiki katika uwanja wa Emirates walishangilia kwa vifijo na nderemo, baada ya kusubiri kwa karibu muongo mmoja na nusu kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
"Imekuwa miaka 14, ambayo ni muda mrefu kwa klabu kama Arsenal na inaonyesha jinsi ilivyokuwa ngumu," kocha wa Arsenal Mikel Arteta aliiambia TNT Sports.
"Kwa kweli tulilazimika kuongeza juhudi ili kufikia ushindi huu. Hatimaye tunaanza kuwa na nguvu ya kushangaza kwenye uwanja, sote tulikuwa tulijisukuma ili kufikia lengo letu na kwa pamoja tumefaulu."
Kampeni ya Arsenal ya 2009-10 katika Ligi ya Mabingwa iliashiria mwisho wa hadhi yao kama nguvu ya soka Uropa.
Baada ya kuwasambaratisha Porto katika hatua ya 16 bora, walikumbana na hali kama hiyo mikononi mwa Barcelona kwenye robo fainali - ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa mabao 4-1 katika mkondo wa pili ambapo Lionel Messi alifunga mabao yote manne.
Kurejea kwa Arsenal katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siku chache baada ya kukwea kileleni mwa Ligi ya Premia, kunaongeza matumaini kuwa The Gunners watajiimarisha tena kama kikosi cha mabara wakiwa na nia ya kushinda mechi ngumu kwenye hatua kubwa zaidi.
'Matokeo mazuri, changamoto inayofuata '
"Ndiyo matokeo haya yenyewe ni makubwa, lakini hatari ya kushindwa ni makubwa zaidi," mlinzi wa zamani wa Arsenal Matthew Upson aliiambia BBC 5 Live.
"Kwenye Premier League na katika mashindano mengine yaliyosalia, kuna mambo mengi mazuri ambayo Arsenal imejifunza.
"Uzoefu huu, kushinda mikwaju ya penati dhidi ya wapinzani wakali, wajanja kama Porto ni wa kupigiwa mfano, bila shaka watakuwa wamejifunza mengi kutokana na mechi hii."
Wakati furaha wanapofurahia, huu haukuwa mchuano wa kuvutia wa Ligi ya Mabingwa. Kulikuwa na majeruhi 74 - zaidi katika mechi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa tangu 2015-16.
Lakini Arsenal wamemaliza - wameumizwa na kujeruhiwa, lakini wameimarika zaidi.
"Uzoefu wa kufika kwenye mikwaju ya penati katika kiwango hiki, na kushinda, ni jambo ambalo wachezaji watakumbuka na kujifunza mengi," alisema winga wa zamani wa Gunners Theo Walcott kwenye 5 Live.
" Sasa wanajua wanahitaji kufanya nini ili kufikia ushindi.
"Walichanganywa na Porto wakati fulani, lakini walikabiliana nayo vilivyo."
Baada ya kuifunga Porto mwaka wa 2010, Arsenal ilitolewa mara saba katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa katika misimu saba mfululizo.
Mchezo huo ulijumuisha fedheha mbaya, ikiwa ni pamoja na mechi yao ya mwisho katika hatua hii mwaka wa 2017 walipofungwa jumla ya mabao 10-2 na Bayern Munich.