Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maisha ya Papa Francis katika Picha
Papa Francis amefariki dunia baada ya kuongoza Kanisa Katoliki kwa zaidi ya muongo mmoja.
Mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa kwenye kibaraza cha juu cha Kanisa kuu la Vatican la Mtakatifu Peter's Basilica ili kuwatakia "Pasaka Njema" maelfu ya waumini.
Papa, akiwa katika kiti cha magurudumu, alipungia mkono kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia katika Uwanja wa mtakatifu St Peter's kwa chini.
Papa alidhamiria kuwa na Kanisa jumuishi zaidi, hizi hapa ni baadhi ya picha za kushangaza za maisha yake na upapa mpaka anafariki akiwa na umri wa miaka 88.
Alizaliwa kama Jorge Mario Bergoglio huko Buenos Aires, Argentina, tarehe 17 Desemba 1936 , akiwa ndiye mkubwa katika watoto watano. Wazazi wake walikuwa wamekimbia nchi yao ya asili ya Italia ili kuepuka ufashisti.
Alikua katika familia ya wafanya kazi, maisha yake ya utotoni yaliwekwa alama ya urahisi na kujitolea kwa imani yake
Akiwa kijana Bergoglio alifanya kazi kama mlinzi (bouncer) katika klabu ya usiku na aliwahi kuwa mfanya usafi. Ailikuwa akishabikia klabu ya soka ya eneo analotoka, San Lorenzo de Almagro, shauku aliyodumiu nayo kwa muda mrefu hata baada ya kuwa Kasisi mnamo 1969
Papa Fransis wakati wa uhao wake alifanya juhudi za kukuza amani ya dunia n alitafuta kuponya mpasuko wa miaka elfu moja na Kanisa la Othodoksi la Mashariki na kufanya kazi na Waanglikana, Walutheri na Wamethodisti