Kwa nini ni vigumu kupata mpenzi wa kweli nyakati hizi?

fdc

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, David Robson
    • Nafasi, BBC

Teknolojia inatupa fursa nyingi mpya za kukutana na wapenzi. Mwandishi David Robson alizungumza na Paul C Brunson, mkuu wa utafiti wa mtandao wa Tinder - ambaye ameandika kitabu kipya cha Find Love: How to Navigate Modern Love and Discover the Right Partner for You.

Kupata mpenzi daima imekuwa uamuzi muhimu sana, lakini kulingana na utafiti wa kitabu hiki, Brunson anaamini kutafuta na kudumu na mpenzi katika zama hizi ni vigumu zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya binadamu.

Sababu moja ni kwamba, kuna aina nyingi za mahusiano kwa sasa. Unaweza kuwa na mke mmoja au mume mmoja au kuna uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja au uhusiano wa kuishi pamoja au kuishi mbali mbali.

Kuwepo kwa namna nyingi za mahusiano kunafanya kupata mshirika wa kuendana na lengo lako katika mapenzi kuwa changamoto zaidi.

Pili, kutaka mambo mengi kutoka kwa wenza wetu. Hapo awali, watu walihitaji mtu wa kusaidia kulinda au kulea mtoto, au kutunza shamba.

Lakini sasa - tumefikia hatua ambapo tunataka mpenzi awe amekamilika kitu kitu. Tunataka awe sawa kiakili, awe Mkurugenzi Mtendaji, tunataka awe mzazi bora, tunataka awe hodari kitandani.

Kwa kweli, watu wengi wamekata tamaa. Lakini watu wengine wanatumia changamoto hizo kwa faida yao. Wanajaribu kubaini kasoro katika uhusiano wao, ili waweze kuuboresha.

Pia unaweza kusoma

Kutafuta mpenzi mtandaoni

fdxc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtafiti wa Tinder Paul C Brunson anasema watu wana vigezo vingi

Kwa kuzingatia kazi yako katika Tinder, ni aina gani ya makosa ambayo watu hufanya katika mbinu zao za kuchumbiana mtandaoni?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuna makosa kadhaa. Mtu hafanyi maamuzi mapema kutambua lengo la uhusiano autakao. Kwa sababu kuna aina nyingi za mahusiano.

Sasa tumeunda kipengele kwenye Tinder kinachokuruhusu kuchagua lengo lako la uhusiano. Kwa sababu, ikiwa wewe unatafuta mpenzi wa muda mrefu, lakini mimi natafuta mpenzi wa muda mfupi, na tukiingia kwenye uhusiano, italeta shida.

Tatizo jingine kubwa ni picha. Watu hawaweki picha zao za karibuni, kwa hivyo wanapoonekana siku ya kukutana, picha zao hazifanani na wao walivyo.

Nilipojiunga na Tinder miaka miwili iliyopita, ilibidi nifungue akaunti ili kuona hali ikoje, na niliweka picha ambayo nilipiga miaka 12 nyuma.

Mtu niyekuwa nikifanya kazi naye huko Tinder alisema Paul, huonekani hivyo. Sote tunafikiri tunaonekana kama tulivyokuwa miaka 10 iliyopita, lakini hatuko hivyo.

Unapaswa kuwa na picha tatu hadi tano - moja inayoonyesha tabasamu la kweli, moja inayoonyesha mwili wako mzima, na baadhi ya picha zako ukifanya kitu ambacho unakipenda.

Tofauti ya vizazi

sdx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna njia nzuri na mbaya za kujionyesha kwenye Tinder, kulingana na utafiti

Tunapaswa kuelewa kwamba kizazi cha Z (waliozaliwa kuanzia miaka ya 90), katika jiji au nchi yako kinaweza kuwa tofauti na kizazi cha Z katika jiji au nchi nyingine.

Katika utafiti wetu katika Tinder, tuligundua kuwa kigezo nambari moja cha iwapo anataka kukutana nawe kwa mara ya pili au la, ni jinsi alivyoliwazika alipokuwa na wewe kwa mara ya kwanza.

Ilhali katika vizazi vyote vilivyotangulia, mvuto wa kimwili ulikuwa jambo la kwanza. Katika zama hizi, mvuto wa kimwili ni jambo namba mbili kwa kizazi cha Z.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah