Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni kwanini baadhi ya dawa hazipaswi kutumiwa na vinywaji vyenye kahawa
Kwa wengi wetu, kuanza siku bila kikombe cha kahawa ni jambo lisiloweza kufikirika.
Lakini, katika baadhi ya nyakati, wakati tunapomeza au kutumia dawa fulani asubuhi, ni bora kusubiri kwa muda mrefu kabla ya kunywa kinywaji hiki.
Baadhi ya dawa zinaweza kumezwa katika nyakati tofauti za siku, lakini pia inashauriwa kutozimeza pamoja na vinywaji vyenye kahawa.
Kuna takriban dawa 60 ambayo yanaweza kuwa na mwingiliano na kahawa ," Antonio Javier Carcas Sansuán, anasema mtaalamu wa madawa na profesa katika chuo kikuu cha Madrid, aktika mazungumzo na BBC Mundo, ingawa mwingiliano kati ya mengi kati ya madawa haya haya ni wa kadri.
Tunapotumia dawa, inasafiri katika mwili wetu wote, inapokuwa tumboni au katika utumbo , hupita ndani yad amu na halafu husambaa kote mwilini.
"Dawa hizi zinapaswa kupita katika eneo ambapo itatekeleza kitendo cha uponyaji wa ugonjwa zinazoutibu, ni lengo la kimatibabu ," Elena Puerta Ruiz de Azúa, profesa katika kitengo cha tiba ya dawa katika Chuo kikuu cha Navarra, aliiambia BBC Mundo.
Fikiria eneo lililolengwa kama kituo cha mkakati wa kutibu ugonjwa, protini katika miili yetu – ambayo hupokea dawa huiimarisha au kuizuia – ambapo itapunguza ufanisi.
Na kwa dawa kufanya kazi yake, inahitaji kufyonzwa na kusambazwa kwa ufanisi.
Halafu dawa hiyo inafaa kuzunguka kwa njia yake pekee, itengwe na mwili pamoja na viungo muhimu vya mwili katika mchakato huu ni ini, ambalo linakazi ya kusafisha mwili wetu. Lakini vipi iwapo kahawa na vinywaji vingine vyenye kafeini itaongezwa kwenye safari hii? Inategemea dawa na lengo lake
Iwapo tunazungumzia dawa yenye lengo la kumfanya mtu asinzie , ukiichanganya na kahawa au vinywaji vyenye kiungo cha kafeini , kama vile Coca cola itakuwa na madhara kwasababu italeta athari mbaya kwa dawa kwa kutenda kinyume na matarajio ya kile ambacho dawa ilitarajiwa kukifanya.
Madawa kadhaa ya aina hii ni kutoka familia ya benzodiazepines, ambayo hutumiwa katika matibabu, kwa mfano kutibu ukosefu wa usingizi na wasiwasi
"Kafeini itafika kwenye ubongo wakati huo huo sawa na dawa hii ," anasema Puerta.
"Halafu upande mmoja utapokea kichocheo cha kafeini na upande wa pili utapokea dawa ambayo nguvu yake ya tiba imepungua: athari ambayo ni kinyume ."
"Kwa baadhi ya madawa, labda ongezeko hili la utegili huenda lisiwe la maana kwasababu wana ukingo mpana salama, lakini kwa wengine ambao ndio wengi huhitaji kiwango kamili cha dawa, na kutopata dawa kamili kunaweza kusababisha hatari," wanaonya wataalamu
"Ni dawa ambayo haijalishi kata imekolea kidogo au zaidi. Inaweza kuwa hatari iwapo makali yake yataongezeka .
Kufyonzwa mwilini
Inashauriwa kwamba baadhi ya dawa, kama vile ile inayotumiwa kutibu kiwewe, kabla ya mlo wowote
Ni muhimu kwamba uwepo wa chakula tumboni na kwenye utumbo unaweza pia kuzuia ufyonzwaji wa aina fulani za dawa.
"Hata kama utameza dozi kama ilivyoshauriwa , iwapo sehemu yake haitaingia mwilini , haitakuwa na athari yoyote kwa tiba ."
Hatahivyo, kwa dawa, chakula ni kitu muhimu : baadhi yad awa zinazozuia majeraha zinaweza kuwa na uharibifu mkubwa kwa ute wa tumbo.
Kwa sababu hii "wakati mwigine kile tunachokishauri ni kumezadawa na chakula ili kuia athari za majeraha tumboni."
Tetracycline , ambayo ni aina ya antibiotic, haiendani na maziwa kwani yanaizuia kufyonzwa mwilini , anafafanua Puerta.
Iwapo utameza dawa ya antibiotic ya aina hiipamoja na maziwa , "ni sawa na kuitupa tu."
Na ni kwamba jamii hii ya antibiotics, inapoingizwa katika bidhaa za maziwa, hutengeneza mchanganyiko usioyeyuka wenye calcium, unaoitwa chelates, ambao hautafyonzwa katika utumbo, kwa hiyo haitakuwa na athari yoyote ya tiba, kulingana na malengo yake.
Soma maelezo
Kama madawa yanaathiri mfumo wa kati wa neva, kama vile antidepressants, zinamezwa, ni muhimu kufuata maagizo ya daktari, kwani kadini yenyewe huchochea sana mfumo huo.
Kulinangana na Puerta, ni muhimu kwamba dawa zitumiwe kama ilivyoelezwa na wataalamu wa afya.
"Sahau kutegemea dawa za nyumbani. Kama umeelezwa kwamba paketi moja ya dawa iwekwe kwenye maji iyeyuke ndio unywe, fanya hivyo, usiiweke kwenye juisi au soda wala kimiminika kingine chochote kile , kwasababu itabadili viungo vyake."
Zaidi ya hayo, anafafanua kuwa kuna dawa nyingi ambazo hazikinzani na kahawa.
"Umeona kila kisa " na njia bora zaidi ni kuhakikisha unamuuliza daktari au mtaalamu wa dawa katika maduka ya dawa.
Kwa ujumla ni muhimu kunywa kahawa kwa kadri,’’ anasema Carcas.