Shah Rukh Khan: Kwa nini haiba na umaarufu wake vimedumu mpaka sasa?

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wiki iliyopita, Shah Rukh Khan alitimiza miaka 30 katika tasnia ya filamu za Kihindi

Mwezi uliopita, mwigizaji wa India Shah Rukh Khan alisherehekea miaka 30 ya kuwa katika tasnia ya filamu za Kihindi.

Shrayana Bhattacharya, mwandishi wa kitabu kuhusu kudumu kwa umaarufu wa mwigizaji huyo wa Bollywood, anaeleza kwa nini bado ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa filamu duniani.

 Pengine ni rahisi kutoa sababu zenye mantiki kuelezea kumudu kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu.

Mamilioni ya watu wanampenda muigizaji huyo bila ubishi kiasi kwamba sifa za hadharani kwake mara nyingi huchukuliwa kama anabudiwa.

Lakini kwa nini Khan anapendwa sana?

Sawa na filamu zake, jibu ni kuwa ‘mapenzi na hisia’ Khan daima ameonesha na kuiwakilisha vyema zaidi India na bara dogo la Asia Kusini. Anatuonyesha mtazamo wa eneo lenye ustawi, wingi na ubinadamu.

Kwa mamilioni ya Wahindi, yeye pia anabaki kuwa zao la ukuaji wa uchumi wa nchi.

Katika miaka ya 1990, Khan alionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye televisheni wakati huo ambao India ikiingia katika nyanja ya uchumi wa dunia. Na hadhi yake iliendana na uchumi unaokua.

Unaweza pia kusoma

Kama sehemu ya mfululizo wa mageuzi ya soko, nchi ilifungua sekta ya mawasiliano kwa uwekezaji wa kigeni ambao uliruhusu mitandao mipya ya vyombo vya habari kutangaza nchini India. Njia hizi zilihakikisha filamu, nyimbo na mahojiano ya Khan yanafikia nyumba nyingi zaidi kuliko mtu yeyote mashuhuri wa filamu kabla yake. India ilipoweka uchumi wake huria zaidi, soda na magari mapya yaliingia sokoni ghafla na kushirikiana na Khan kama balozi wa chapa zao.

 Kwa maana hiyo, kupanda kwa Khan kutoka katika familia duni huko Delhi hadi mtu mashuhuri wa kimataifa ni hadithi ya mwisho ya mafanikio ya uchumi mamboleo nchini India, kielelezo cha jinsi ya "kufika" kileleni bila ukoo wowote wa filamu au kuunganishiwa ili kusaidia kufika juu. Ukubwa wa Khan ulikua kwa pamoja na uchumi unaokua.

Kuimarisha haki za kidini, Khan pia amekuwa ishara ya kuunganisha Wahindi wengi.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shah Rukh Khan ana mamilioni ya mashabiki duniani kote
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakosoaji wanasema hali ya kutovumiliana imekuwa ikiongezeka chini ya serikali ya Wahindu ya Waziri Mkuu Narendra Modi, ambayo inashutumiwa pakubwa kwa kuwatenga Waislamu wa India.

Mtoto wa kiume wa Khan, Aryan Khan, alikamatwa mwaka jana katika kesi ya dawa za kulevya na baadae kuachiliwa huru katika kesi ambayo wengi walihisi ilikuwa ikimlenga Muislamu aliyefanikiwa zaidi nchini India.

Daima ametoa maoni ya kufikiria juu ya wingi wa Wahindi na kucheza uhusika mwingi wa Kiislamu kuliko wa enzi zake.

Walakini, mashabiki wake wanakataa kumshusha kwa utambulisho wake wa kidini badala yake, wanamwona kuwa mwenye busara, hekima na mwenye mafanikio.

Tukijadili mashambulizi mabaya ya mrengo wa kulia dhidi ya Khan na familia yake ya watu wenye imani tofauti kama mke wake ambaye ni Mhindu, shabiki mdogo niliyemhoji alikiri "Yeye hana dini, lakini pia ni mtanashati sana."

Muhimu zaidi ni kuwa mwigizaji huyo amekuwa akionesha udhaifu ambao sisi sote tunaufanya kama binadamu.

Khan kawaida huonyesha taswira ya udhaifu; mpenzi dhaifu, shujaa dhaifu, mume dhaifu, Mwislamu dhaifu na hata mhalifu dhaifu.

Wasiwasi ambao unasumbua uhusika wake katika televisheni umeibuka kupitia maendeleo ya kazi yake kwa miongo mitatu. Mara nyingi ni mtu mwenye hisia na mcheshi hasa anapozungumza na umma.

Khan pia ni shujaa wa kimapenzi wa bara la Asia Kusini , filamu zake ndizo kiwango ambacho wapenzi wote hujaribu kuendana nazo.

Takwimu zinaonyesha kuwa wahusika anaowacheza hujihusisha na wanawake zaidi kuliko nafasi zinazochezwa na nyota wengine wa kiume wa Bollywood. Lakini upendo ambao uhusika wa Khan wanatafuta sio tu upendo wa jadi wa mwanamke, wanatafuta sana upendo na idhini ya baba, marafiki na watu wangine wa nchini humo.

ggg

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Khan anajulikana kama mfalme wa mapenzi

Wahusika anaowacheza katika filamu hupata hisia za ndani, huwa katika mazingira magumu na kumwaga machozi mengi, mengi (mengi). Waandishi wa filamu mara nyingi wanatoa maoni kuhusu jinsi Khan anavyoweza kulia kuliko waigizaji wengi duniani. Kutoa huko machozi kunakoonesha ubinadamu kumemfanya kupendwa na mashabiki wengi.

 Zaidi ya sinema, mahojiano yake ya televisheni na mihadhara ya umma imeongeza ucheshi wake na unyenyekevu.

Kuna mashabiki wengi wasomi wa mjini ambao wanafuatilia mahojiano ya Khan zaidi kuliko filamu zake. Mazungumzo haya ya vyombo vya habari yanaashiria uigizaji bora zaidi wa mwigizaji huyo hadi sasa.

Kuvuta sigara, ushupavu, kujitambua na kufurahisha, Khan hachoshi kamwe. Anatoka kuwa mtoa ushauri mzuri juu ya kushughulika na ukosefu wa usalama wa kifedha na urafiki wenye shida hadi kwa utani unaochekesha kuhusu kuzeeka katika tasnia ya filamu na jinsia yake mwenyewe.

Katika nukuu zake zote na utani wake kwake mwenyewe na ulimwengu, kila wakati kuna maoni ya mtu anayefanya kazi kwa bidii, anajali sana ufundi wake na anafurahia kucheka mwenyewe.

Katika ulimwengu wa mashaka usio na uhakika, picha za kupendeza za Khan zimesalia kuwa chanzo cha kushangaza na burudani.

 Baada ya mapumziko, mwigizaji huyo anakuja na filamu tatu kubwa zinazotarajiwa kutoka 2023. Mashabiki wake wamejawa na msisimko, lakini pia wanahofia kampeni za mitandao ya kijamii za mrengo wa kulia zinazotetea kususiwa kwa wasanii wa Kiislamu na filamu za Bollywood.

Huku siasa zikizidi kuleta mgawanyiko, nguvu ya mwigizaji huyo ipo katika namna anavyoweza kutuunganisha wengi kwa tabasamu na hadithi.

Katika miaka 30 ijayo ya mkongwe huyu, tamaduni zilivovunjika nchini India zinahitaji vichekesho vya utani wake kwa mikono miwili.