Kutoka kuwa rais hadi mfungwa mtarajiwa: Hukumu ya Sarkozy inaigawa Ufaransa

d

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela
    • Author, Hugh Schofield
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Nicolas Sarkozy, miaka 13 baada ya kuondoka madarakani, anakaribia kuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kufungwa jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kula njama za uhalifu.

Baada ya kuhukumiwa katika kesi ya "fedha za Libya" siku ya Alhamisi, alizungumza kwa hasira kuhusu "chuki" ambayo alisema yeye ni mwathirika.

Tangu alipoibuka kama rais wa mrengo wa kulia, Sarkozy ameshawishika kuwa analengwa na watu wa mrengo wa kushoto ndani ya mahakama na vyombo vya habari vya Ufaransa.

Na kwa sentensi hii - anadhani - ni ushahidi usio na shaka wa hilo.

Pia unaweza kusoma

Wafuasi wake wanauliza

Wafuasi wake wanauliza, kwa nini mahakama ilimfutia mashtaka matatu kati ya manne yaliyokuwa yakimkabili: ufadhili haramu wa chama, ubadhirifu wa fedha za Libya na ufisadi?

Pia wanauliza, kwa nini mahakama ilimtia hatiani kwa shtaka la mwisho - lile la kula njama ya uhalifu? (Kosa ambalo mara nyingi hushitakiwa washiriki wa magenge ya dawa za kulevya wakati wapelelezi hawana kingine cha kuwashitaki.)

Na kwa nini - baada ya kumtia hatiani kwa shtaka hili dogo - mahakama imempa adhabu ya kufedhehesha na kali namna hiyo? Wamempa mzee wa miaka 70 miaka mitano jela, kwa kosa hilo.

Pia wanaeleza kuwa hukumu hiyo haina "kusitishwa" - kwa maneno mengine ni lazima atakwenda jela hata kama atakata rufaa. Ingawa katika sheria ya Ufaransa, kusubiria rufaa unahesabiwa bado huna hatia kinadharia.

Wengi watamuone huruma Sarkozy - sio kwa sababu hana hatia katika suala hili la kutafuta pesa za kampeni kutoka Libya, lakini ni vile kuona kuna ukweli fulani katika madai yake ya kudhulumiwa:

Kwamba kuna baadhi ya watu katika taasisi za Paris za "kisiasa, vyombo vya habari- na mahakama" ambao wanamchukia na kufurahia kumwangusha.

Mtazamo mwingine

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hata hivyo, angalia jambo hili kwa mtazamo mwingine. Sarkozy ni kiongozi wa zamani wa nchi – ambaye mara kwa mara amekiuka sheria ili kupata analotaka.

Tayari kuna mfululizo wa kesi dhidi yake. Sarkozy alipatikana na hatia kwa mashtaka mengine mawili ya rushwa - moja kwa kujaribu kumuhonga jaji, na kesi nyingine nyingine kwa ufadhili haramu wa kampeni.

Na kama mahakama sasa imeamua kumtia hatiani kwa suala la Libya, labda ni kwa sababu shtaka la kujaribu kutafuta fedha za uchaguzi kutoka kwa dikteta wa kigeni ni kubwa sana.

Ingawa Sarkozy hana ushawishi tena kama wa zamani, lakini mabishano kuhusu kesi hii yanaibuka kupitia siasa za Ufaransa.

Wakati mrengo wa kulia na mrengo mkali wa kulia wakilia kuhusu mahakama kuwa za mrengo wa kushoto. Mfano, Marine Le Pen aliyepigwa marufuku kugombea urais baada ya hukumu dhidi yake mwenyewe mapema mwaka huu - alikuwa wa kwanza kushutumu "ukosefu wa haki.”

Na upande wa watu wa mrengo wa kushoto, wanaona haya yote ni ushahidi kwamba watu wenye nguvu hawana fursa ya kupuuza sheria.

Nicolas Sarkozy ameondoka madarakani muda mrefu, na hakuna matarajio ya kurudi. Sisa zake ni historia. Lakini kesi yake inaweka wazi migawanyiko katika nchi iliyogawanyika.