Haya ndio matetemeko matano makubwa zaidi kuwahi kutokea duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Tetemeko la mwishoni mwa wiki hii nchini Morocco limeua watu zaidi ya 2,000 na kuwa miongoni mwa matetemeko yaliyoua watu wengi duniani.
Februari 2023, matetemeko mawili ya ukubwa wa 7.8 na 7.5 richter yalizikumba nchi za Uturuki na Syria. Tetemeko la Uturuki linatajwa kuwa tetemeko kubwa zaidi katika siku za hivi karibuni, likiua watu zaidi ya 50,000 lakini ulimwengu umewahihi kushuhudia matetemeko yenye nguvu zaidi.
Kulingana na data kutoka kwa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani, tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi katika historia ilitokea kusini mwa Valdivia, Chile mwaka wa 1960. Ukubwa wa tetemeko hilo lilikuwa 9.5 kwenye kipimo cha Richter.
Watu 2000 walifariki na wengine milioni mbili waliachwa bila makao kufuatia tetemeko la hilo la ardhi lilisababisha volcano zilizo karibu kulipuka na mitikiso yake kusika hadibaharini. Mitetemeko ya baadaye ilisababisha uharibifu mkubwa katika miji ya pwani

Chanzo cha picha, ANADULU AGENCY
Matetemeko ya ardhi yenye nguvu zaidi ya karne ya 21 yalilitokea mwaka 2004 huko Indonesia na 2011 huko Japan. Matetemeko yote mawili yalifikia 9.1 kwenye kipimo cha Richter.
Athari za tetemeko hilo la ardhi lililokumba pwani ya magharibi ya kisiwa cha Indonesia cha Sumatra ilikuwa kubwa zaidi.
Tsunami iliyofuata tetemeko la ardhi iliathiri nchi 14 za Asia Kusini na Afrika Mashariki. Takriban watu 2,30,000 walikufa au kutoweka kutokana na tsunami hiyo. Watu elfu 17 walipoteza makazi yao.
Tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki na Syria siku ya Jumatatu ni mojawapo ya matetemeko 20 yenye nguvu zaidi yaliyorekodiwa katika karne iliyopita. Mnamo 2015, tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lilipiga Nepal huko Alaska, Marekani, na kuua watu wapatao 9,000.
Ikiwa tunazungumza juu ya idadi ya vifo, tetemeko la ardhi lililotokea Haiti mnamo 2010 ndio mbaya zaidi. Ingawa tetemeko hilo halikuwa kubwa zaidi, liliua watu 3,16,000.
Kulingana na data kutoka kwa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani, matetemeko matano makubwa zaidi kuwahi kurekodiwa ni:
1. Chile

Chanzo cha picha, AFP
Tarehe: 05/22/1960
Ukubwa: 9.5
Usiku wa Mei 22, 1960, Chile ilikumbwa na mojawapo ya matetemeko ya ardhi yenye nguvu zaidi kuwahi kushuhudiwa, yaliyosababisha uharibifu mkubwa nchini humo.
Takriban watu 1600 walikufa na watu 3000 walijeruhiwa katika mkasa huo wa asili. Zaidi ya watu laki 20 walipoteza makazi yao kutokana na tetemeko hilo la ardhi. Tetemeko hilo la ardhi liligharimu Chile uharibifu wa takriban dola milioni 550.
Tetemeko hilo la ardhi lilifuatiwa na tsunami, iliyoua watu 61 huko Hawaii, 138 huko Japan, na 32 nchini Ufilipino.
2. Alaska (Marekani)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe: 03/28/1964
Ukubwa: 9.2
Tetemeko la ardhi lililofuatiwa tsunami liliua watu 131 na kusababisha uharibifu unaokadiriwa kuwa dola bilioni 2.3. Athari ya tetemeko la ardhi ilishuhudiwa sana katika miji kadhaa ya Marekani.
3. Sumatra (Indonesia)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe: 12/26/2004
Ukubwa: 9.1
Usiku wa saa Sita na dakika hamsini na nane ( 12.58am) asubuhi mnamo Desemba 26, 2004, tetemeko kubwa la ardhi lilitokea kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia.
Tsunami iliyofuatia tetemeko la ardhi iliathiri nchi 14 za Asia Kusini na Afrika Mashariki.
Kwa jumla, watu wapatao 2,30,000 walikufa au kutoweka katika janga hilo. Watu elfu 17 walipoteza makazi yao kutokana na tetemeko hilo la ardhi.
4. Honshu (Japan)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe: 03/11/2011
Ukubwa: 9.0
Takriban watu 15,700 waliuawa wakati tsunami ilipopiga pwani ya mashariki ya Honshu, kisiwa kikubwa kinachokaliwa na watu wengi zaidi nchini Japan, baada ya tetemeko la ardhi. Watu 4600 walifariki na wengine 5300 walijeruhiwa katika tetemeko hili la ardhi.
Tetemeko la ardhi na tsunami iliacha zaidi ya watu 1,30,000 bila makazi na kuharibu vibaya nyumba na majengo 3,00,000. Vifo vingi zaidi viliripotiwa katika miji ya Iwate, Miyagi na Fukushima.
Tsunami hiyo ilisababisha mawimbi ya bahari ya urefu wa mita 38 katika eneo hilo. Janga hilo la asilia lililigharimu Japan hasara ya takriban dola bilioni 309.
5. Kamchatka (Urusi)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tarehe: 11/04/1952
Ukubwa: 9.0
Mnamo 1952, tsunami ilitokea baada ya tetemeko la ardhi kukumba rasi ya Kamchatka eneo la Mashariki ya Mbali ya Urusi. Ni watu wachache waliripotiwa kujeruhiwa kwa sababu eneo hilo lilikuwa na wakazi wachache.
Hata hivyo, tsunami ilipiga Hawaii nchini Marekani, na kusababisha uharibifu wa karibu dola milioni moja. Mawimbi makubwa yaliharibu boti, nyumba, nguzo na barabara.














