Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi ya kujua dalili za saratani kupitia kinyesi
Deborah James, mwanaharakati wa saratani kutoka Uingereza na mtengenezaji wa kipindi cha BBC cha "You, Me And The Big C," amefariki akiwa na umri wa miaka 40. Aliweza kukusanya maelfu ya pauni kwa ajili ya utafiti wa saratani ya utumbo.
Deborah alisisitiza umuhimu wa kuzingatia kinyesi katika kutambua ugonjwa wa saratani.
Philippa Roxby, mwandishi wa BBC wa masuala ya afya, ameandika kuhusu vidokezo vya kusaidia kugundua saratani ya utumbo mapema.
Inahitajika kuzingatia ishara hizi:
• Damu nyekundu au nyeusi kwenye kinyesi chako
• Unajisaidia mara nyingi zaidi, kinyesi kigumu au chepesi kuliko kawaida
• Unahisi maumivu huku tumbo limevimba na kuwa gumu
Dalili zingine zinaweza kujumuisha;
• Kupoteza uzito haraka
• Kujihisi tumbo zito hata baada ya kwenda chooni
• Kuhisi uchovu kuliko kawaida au kizunguzungu.
Wakati mwingine saratani ya utumbo huzuia kinyesi kupita kwenye matumbo. Hii inaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo na kuvimbiwa. Katika hali kama hizo, unapaswa kuwasiliana mara moja na mamlaka ya afya.
Jinsi ya kuchunguza kinyesi
Unapaswa kuzingatia kinyesi chako kila wakati unapokwenda chooni. Na hupaswi kuogopa kuzungumza. Mbali na damu kwenye kinyesi chako, unapaswa pia kuangalia kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa.
Kunaweza kuwa na mabadiliko katika tabia zako za choo - unaweza kuhisi kama unaenda mara nyingi zaidi au mara chache zaidi. British Bowel Cancer Foundation inapendekeza uweke shajara ili kurekodi dalili zako kabla ya kwenda kwa daktari.
Madaktari wanajua watu wengi wenye matatizo mbalimbali ya matumbo, wanajua dalili za ugonjwa huu. Kwa hiyo, usisite kuwajulisha kuhusu mabadiliko katika tabia yako ya choo na kutokwa damu.
Ni nini sababu za saratani ya utumbo? Haijulikani hasa ni nini husababisha saratani ya utumbo mpana. Lakini kuna mambo kadhaa ambayo huongeza uwezekano wa ugonjwa huu:
• Kadiri umri unavyoongezeka, hatari ya kupata saratani, pamoja na saratani ya utumbo, huongezeka. Kesi nyingi hutokea kwa watu zaidi ya miaka 50.
• Kula kiasi kikubwa cha nyama nyekundu na soseji, pamoja na nyama ya kusindika kama vile bakoni
• Kuvuta sigara
• kunywa pombe nyingi
• Uzito kupita kiasi
Je, ni ugonjwa wa kurithi? Katika hali nyingi, saratani ya utumbo sio ya urithi.
Jinsi ya kupunguza hatari ya kupata saratani
Wanasayansi wanasema kuishi maisha yenye afya kunaweza kuzuia zaidi ya nusu ya visa vya saratani ya matumbo. Unahitajika kufanya mazoezi zaidi, kula vyakula vingi vya nyuzi na mafuta kidogo, na kunywa glasi sita hadi nane za maji kwa siku.
Wanasayansi wanasema watu wa umri wa miaka 50 na 70 hupata saratani hiyo kila baada ya miaka 10. Ni muhimu kufanya uchunguzi wa MRI kuanzia umri wa miaka 40.
Hata kama wewe ni wa umri mdogo, unapaswa kumuona daktari unapoona dalili zozote, wala usinunue vifaa vya kujipima. Kwa sababu matokeo yanaweza kuchanganya.
Saratani ya matumbo inaweza kutibiwa, haswa ikiwa itagunduliwa mapema. Kulingana na matokeo ya vipimo, mbinu za matibabu ni za mtu binafsi.
Chaguzi tofauti hutumiwa katika matibabu ya saratani, kama vile upasuaji, tiba ya dawa na tiba ya mionzi.
Hatu za saratani
• Hatua ya kwanza - uvimbe wa saratani ni mdogo na haujasambaa.
• Hatua ya pili - uvimbe wa saratani ni mkubwa kiasi, lakini bado haujaenea.
• Hatua ya tatu - uvimbe wa saratani umeenea kwa katika baadhi ya tishu zinazozunguka, kama vile.
• Hatua ya nne - saratani imeenea katika kiungo kingine cha mwili.