Kwa nini tunafaa kuwathamini wanyama wanaokula mizoga?

Wawindaji daima wanadharauliwa na hata kuogopwa. Duniani kote,viumbe hawa wakiwemo Tai,Fisi na wadudu ambao wanategemea Wanyama kujipatia chakula chao kutokana na mizoga wanachukuliwa kama vile ni wachafu, hatari na wasiostahili kukaribiana nao.
Katika kitabu chake kijulikanacho kama The Green Hills of Africa, Mwandishi Ernest Hemingway amemuelezea Fisi kama "mteketezaji wa mizoga, msafisha mizoga ya ng’ombe inayozagaa, pia anaonekana kama ishara ya mkosi na kitu cha kutisha,pale unapoweza kuota ana kukung’ata usoni,na hivyo kuonekana kwamba tai ni alama ya mkosi na bahati mbaya.
Hata hivyo wanasayansi walio wengi wamebaini kuhusiana na Wanyama hawa wala mizoga,jambo ambalo linaonesha wazi kwamba ni lazima tuwajali na kuwalinda zaidi ya vile tunavyofanya sasa.Wanajukumu kubwa katika kuhifadhi Ikolojia kwani wanaleta faida kiafya na manufaa ya kiuchumi pia.Kutokana na kula mizoga wanazuia bakteria wa maradhi kushindwa kuwafikia binadamu na Wanyama katika mazingira yao.
Utafiti mpya umebaini kwamba faida za kiafya na kimazingira na kiuchumi kutokana na tai,Fisi na Wanyama wengine wala mizoga inasaidia kuzuaia gharama kubwa ya kupoteza uhalisia wa uumbaaji wa mazingira.
Tai wao wanasifa ya kipekee ya kusafisha kabisa uwepo wa mizoga,na hivyo kuwafanya kuwa muhimu Zaidi kuliko Wanyama wengine wala mizoga duniani,kama ambavyo anabainisha mwanasayansi Vibhu Prakash, kutoka taasisi ya kisayansi ya Bombay Natural History Society,ambaye alitafiti mazuingira ya tai katika programu maalumu ya uhifadhi wa mazingira. "Wanaweza kula takribani asilimia 40 ya mwili wa mzoga,wakati Wanyama wengine wanaweza kula asilimia tano tu,’’ anasema Vibhu Prakash .

Jambo la kusikitisha ni kwamba ndege hawa Tai wanaendeea kutoweka kwa kasi kusini mwa Asia na Afrika..
Kupungua kwa idadi ya tai wa India kulianzia katika miaka ya 1990 na kulitokea haraka sana.
Mapema miaka ya 1990, kulikuwa na tai kati ya milioni 100 na 160 nchini humo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Walikuwa kila mahali nchini India," anasema Bowden. "Walikuwa wakifanya kazi ya ajabu ya kusafisha mizoga kwa kiwango kikubwa."
Lakini kufikia mwanzoni mwa karne hiyo, makumi ya mamilioni ya ndege walikuwa wakifa kwa njia ya ajabu. Idadi ya aina tatu za tai nchini India kwa pamoja ilipungua kwa zaidi ya 97% kati ya 1992 na 2007.
Tai hao walifanyiwa majaribio ya vyuma vizito, dawa za kuulia wadudu na vichafuzi vingine lakini hakuna sababu moja ya kifo iliyoweza kutambuliwa. Hatimaye, uchunguzi wa maiti ulionesha kwamba tai wengi waliokufa walikuwa na aina ya ‘gout’ iliyosababishwa na kushindwa kwa figo.
Watafiti waligundua kwamba tai walikuwa wakitiwa sumu na dawa ya kutuliza maumivu ya diclofenac - inayotumiwa sana kama dawa ya mifugo kutibu ng'ombe - walipokuwa wakila mizoga ya mifugo.
"Kuna jambo lisilo la kawaida kuhusu kimetaboliki ya tai...hawawezi [kushughulikia] diclofenac na hiyo husababisha kushindwa kwa figo," anasema Bowden.
Mbwa mwitu wa India hivi karibuni walifaidika kutokana na kupungua kwa tai, anasema. Kwa sababu ya kupungua kwa idadi ya tai, mizoga ya ng'ombe ilirundikana na idadi ya mbwa mwitu iliongezeka na kuwa wawindaji wakuu.
Hii ilikuwa na athari kubwa kwa afya ya binadamu kwani ilisababisha kuongezeka kwa vifo vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, anasema Prakash. "Kumekuwa na ongezeko la kichaa cha mbwa nchini India katika kipindi cha miaka 20 iliyopita," anasema.

Kulingana na utafiti wa wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Bath, kupungua kwa tai kulichukua nafasi kwa mbwa mwitu zaidi ya milioni 5.5 nchini India, na waliwauma watu zaidi ya milioni 38.5 kati ya mwaka 1992 na 2006.
Kwa kutumia uchunguzi wa kitaifa ambao ulionesha kuwa watu 123 kati ya 100,000 ambao wanaumwa na mbwa walikufa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa, wanasayansi walihesabu kuwa takribani watu 47,395 walikufa kutokana na mbwa mwitu kuwa wawindaji wakuu nchini India.
"Tai hutoa faida kadhaa kwa jamii ya IndiA, kutoka kwa utupaji taka hadi maadili ya kiroho," anasema Tim Taylor, mwandishi wa utafiti huo na mhadhiri mkuu wa uchumi wa mazingira na afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Exeter. "Utupaji taka ni muhimu sana, kwani wanaweza kupunguza chakula kinachopatikana kwa mbwa wanaopotea na hivyo kusaidia kudhibiti idadi ya mbwa."
Kwa kuzingatia wastani wa gharama ya kutibu wagonjwa wa kichaa cha mbwa na kukabiliana na vifo vya ziada, Taylor na wenzake walihitimisha kwamba kupungua kwa tai kulikosababishwa na diclofenac kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuligharimu India $34bn (£28bn) kati ya 1993 na 2006, sawa na 3.6% ya pesa zote za nchi hiyo, Pato la Taifa mwaka 2006.
"Ni muhimu kwamba tai warejeshwe, kwani ni rasilimali muhimu kwa India na wanashikilia nafasi muhimu katika mfumo wa ikolojia," anasema Taylor.
Katika bara la Afrika, tai pia wanakufa kwa kasi, lakini kwa sababu tofauti.
Katika bara zima, idadi ya tai imepungua kwa hadi 97%. Saba kati ya spishi 11 za tai wa Afrika-Eurasia wako katika hatari ya kutoweka.
Hapa, tai ndio waathiriwa licha ya kuwa sumu inayolenga kuua wanyama wanaowinda wanyama wengine wakubwa, kama vile simba, anasema Darcy Ogada, mkurugenzi wa Afrika wa Mfuko wa Peregrine, shirika lisilo la faida ambalo hulinda ndege walio hatarini kutoweka ulimwenguni kote.
Wakulima wanaopoteza ng’ombe husambaza dawa zenye sumu kali kuwauwa wanyama wanaowinda wanyama wengine kama vile simba, na mara nyingi simba huwa hawarudi tena ila tai ndio huteseka Zaidi baada ya kula mizoga, anasema.
Wawindaji haramu pia hunyunyizia dawa za kuua wadudu kwenye tembo waliokufa ili kuua tai na kuwazuia kuwajulisha walinzi wa mbuga kwa kuwazunguka juu, anaongeza.
Tai wengi pia wanauawa kwa sababu ya imani za kidini. Vichwa vya tai vinatumika kwa dawa za jadi na katika "uchawi ", hasa kusini mwa Afrika, anasema Ogada.
Kupungua kwa tai barani Afrika pia kumezua hatari ya kiafya, kulingana na utafiti wa Ogada. Katika utafiti wa mwaka wa 2012 uliofanywa nchini Kenya, Ogada na wenzake waligundua kuwa mamalia wengi wanaotafuna wanyama walikusanyika karibu na mizoga wakati tai hawakuwepo, hasa fisi na mbweha.

"Wakati hakuna tai, kuna vitu vingine kwenye mandhari ambavyo vinataka kula mzoga," anasema Ogada. "Lakini hakuna aliye na uwezo wa kusafisha mifupa jinsi tai wanavyofanya, ili kusiwepo hata na nzi juu yake."
Mzoga unaooza ambao haujasafishwa hufanya kama "kitovu cha maambukizi ya magonjwa", ambapo wanyama walioambukizwa hukusanyika na kueneza vimelea vya magonjwa, anasema Ogada. "Kulikuwa na mara tatu zaidi ya [muda] wa kuwasiliana [kati ya wanyama mbalimbali] kwenye mizoga ambayo haikuwa na tai."
Fisi na mbweha pia wana uwezekano mkubwa wa kugusana na wanadamu kuliko tai na hufanya kama kienezaji cha magonjwa.

Ingawa faida za kiafya za tai mara nyingi hubakia kutothaminiwa, labda haijulikani hata kidogo kwamba tabia zisizopendeza za tai pia zinaweza kuwa na manufaa kwa hali ya hewa. Kwa kweli kunaweza kuwa na hatari kubwa za kimazingira zinazohusiana na kupungua kwa tai duniani kote.
Nchini India, mbwa mwitu hawawezi kuendana na ufanisi na kasi ya tai linapokuja suala la kutupa mizoga, anasema Bowden. Hii ina maana kwamba mizoga mingi huachwa ioze kiasili au, katika baadhi ya matukio, huchomwa moto.
Mizoga hutoa gesi chafu inapooza, ikiwa ni pamoja na kabon lakini hewa hizo huzuiliwa ikiwa tai watazitoa, kulingana na utafiti uliotolewa mapema mwaka huu na wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Comahue nchini Argentina.
"Huduma hii ya mfumo wa ikolojia inayochangiwa na tai kwa binadamu na mazingira haiwezi kubadilishwa kwa urahisi na viumbe vingine, ikiwa ni pamoja na binadamu," utafiti unabainisha.
Hata hivyo, kutokana na kukosekana kwa tai, mizoga inayooza nchini India sasa mara nyingi huzikwa, hutupwa kwenye maeneo ya kutupia taka, au hutupwa mtoni, ambapo huhatarisha kuchafua maji na kusababisha harufu kuzunguka miji, anasema Prakash.
Mnamo 2004, baada ya wanasayansi kugundua kwamba diclofenac ilisababisha kupungua kwa kasi kwa tai, walizindua programu za kuzaliana ili kusaidia kuongeza idadi kote nchini India, na ndege wa kwanza waliofugwa kutolewa mnamo 2021. Lakini ni maendeleo ya polepole - tai hukomaa wakiwa na takriban watano. na kutoa yai moja tu kwa mwaka, asema Prakash, na nusu tu ya ndege hufikia utu uzima.
Licha ya huduma wanazotoa, tai na fisi hawathaminiwi duniani kote, wanasayansi wanasema.
"Fisi wanachukuliwa kuwa wawindaji waliofanikiwa zaidi barani Afrika…Kwa hiyo hilo pia linasababisha migogoro mingi na pengine kuongeza katika masimulizi hasi," anasema mtafiti Sonawane. "Filamu kama Lion King labda hazisaidii,"anaongeza .
"Tai wanahusishwa na kifo na kuna ushirikina na imani kuwahusu katika nchi nyingi," anasema Bowden. "Nchini Nepal, kama tai akikaa juu ya nyumba yako, inachukuliwa kuwa bahati mbaya na inamaanisha mtu atakufa. Tunapambana kuangazia jukumu muhimu na chanya ambalo tai wanacheza."
Kwa kuongeza ufahamu wa uwezo wa wawindaji taka kuondoa sumu hatari kutoka kwa mazingira na kuzuia kuenea kwa magonjwa hatari kwa wanadamu, hata hivyo, wahifadhi wanatumai kuongeza uokoaji wa spishi hizi muhimu. Kwa kufanya hivyo, pengine wanaweza kuwasaidia wanadamu kukomesha kashfa zetu za waharibifu mara moja na kwa wote, na badala yake kuwathamini kwa manufaa mengi wanayotupatia.












