Kimbunga Ian: Cuba yakumbwa na giza baada ya dhoruba

Chanzo cha picha, Getty Images
Cuba haina umeme kabisa baada ya kimbunga Ian kupiga magharibi mwa kisiwa hicho, serikali yake imetangaza.
Maafisa walisema mfumo wa umeme umeanguka kabisa baada ya moja ya mitambo mikubwa ya umeme kukushindwa kufanyakazi tena.
Watu wawili wameripotiwa kufariki na majengo kuharibiwa nchi nzima.
Vimbunga vya aina ya tatu, vyenye kasi ya upepo wa hadi 195km/h (120mph) sasa vinashuka kuelekea Florida.
Katika runinga ya taifa ya Cuba siku ya Jumanne, mkuu wa mamlaka ya nishati ya umeme alitangaza kwamba kukatika kwa umeme katika kisiwa chote kumetokea kutokana na kuharibika kwa mfumo wa kitaifa wa umeme, na kuwaacha watu milioni 11 gizani.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la serikali aliripoti kwamba 100% ya saketi za umeme nchini hazikuwa na huduma na kwamba "kinu cha umeme cha Antonio Guiteras ... hakikuweza kufanya kazi kwa wakati mmoja".
Katika makao yake huko Matanzas, kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu Havana, Antonio Guiteras ndio mtambo muhimu zaidi wa nishati nchini Cuba. Kuzimwa kwake kunamaanisha kuwa kwa sasa hakuna uzalishaji wa umeme popote kwenye kisiwa hicho.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmiliki wa kiwanda cha uzalishaji wa sigara maarufu Finca Robaina alichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii za uharibifu uliosababishwa na kimbunga hicho katika mashamba ya tumbaku.
Hirochi Robaina aliandika hivi: "Ilikuwa ni janga kweli"
Watabiri walikuwa wameonya kuwa baadhi ya mikoa ya Cuba inaweza kupata mvua ya hadi 30cm (12in) kutokana na Kimbunga Ian.
Mayelin Suarez, mkazi wa Pinar del Rio, alisema Jumatatu usiku, wakati dhoruba ilipopiga, ilikuwa "giza tete maishani mwake".
"Tulikaribia kupoteza paa katika nyumba yetu," aliiambia Reuters. "Binti yangu, mimi na mume wangu tulilifunga kwa kamba ili isiruke."
Rais wa Cuba Miguel Diaz Canel alitembelea jimbo hilo na kuapa kwamba litaleta "mateso ya juu", ofisi ya rais wa Cuba iliandika.












