Waziri Mkuu asiyepeana mikono na wanawake

Chanzo cha picha, ABDISHUKRI HAYBE
Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia, Hamse Abdi Barre, alitoa taarifa kwenye mtandao wa kijamii, baada ya kuchapishwa video akisalimiana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Catriona Laing bila kumpa mkono.
Baadhi ya watu wanaamini Laing kama kuonyesha kuudhika na hilo. Wengine wamekosoa uamuzi wa Barre, huku wengine wakiunga mkono kwa sababu za kidini.
Baadhi ya Waislamu hawapeani mikono na wanawake ambao si wake zao, wanaamini ni dhambi kuwagusa wanawake wasio wake zao.
Yapo matukio mengine ya Waziri Mkuu huyo akiwasalimia wanawake bila ya kuwapa mkono - katika maeneo anayotembelea au viwanja vya ndege akiwakaribisha wanadiplomasia, viongozi na wageni wengine.

Chanzo cha picha, OPM/SOMALIA
Aprili 29, 2023, Waziri Mkuu Barre, alirejea Mogadishu, Somalia kutoka ziara nchini Saudi Arabia, na kupokelewa na baadhi ya wanawake ambao hakuwapa mikono wakati wa kusalimiana nao.

Chanzo cha picha, OPM/SOMALIA
24, Agosti 2023, Barre hakupeana mikono na mwanadiplomasia wa Uturuki katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha TurkSom wakati wa ziara katika kituo hicho, kinachotoa mafunzo kwa Wanajeshi wa Somalia.

Chanzo cha picha, OPM/SOMALIA
30 Novemba 2023 akiwa katika ziara ya kutembelea wilaya ya Afmadow mkoa wa Lower Jubba, anaonekana anasalimiana na wanawake kwa kugusa kifua chake bila kuwapa mikono.
Akijibu kuhusu jambo hilo, alisema hiyo ni "sera ya peponi." Waziri Mkuu Barre aliviambia vyombo vya habari wakati akifanya mahojiano, “nataka kwenda peponi kupitia siasa."

Chanzo cha picha, OPM/SOMALIA
Tarehe 10 Oktoba 2022, Barre aliwasalimia wanawake waliokuwa wamesimama wakimshangilia na kumkaribisha katika mkoa wa Benadir huko Mogadishu, wakati wa ziara yake ya kiserikali na hakuwapa mkono wanawake hao.

Chanzo cha picha, SOCIAL MEDIA
Tukio ambalo limezua mjadala, ni lile linalomuonyesha mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Catriona Laing ambaye aliinua mkono wake kwa Waziri Mkuu lakini Waziri Mkuu alimsalimia kwa kuweka mkono kifuani bila kumpa mkno.
Wakati akizungumza katika kongamano la hadhara, Waziri Mkuu Barre alisema yeye ni muumini wa dini ya Kiislamu, vilevile anafuata Quran Tukufu.
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Dinah Gahamanyi












