Manchester City: Kwanini ushindi wa mataji matatu unazusha maswali na pongezi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ushindi wa Manchester City wa kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya huko Istanbul ulionekana kuwa ni ushindi muhimu katika mchezo wa soka kwa miaka mingi. Hatimaye kombe waliloliwinda kwa muda mrefu wamelipata.
Kwa kufanikisha ushindi wa makombe matatu katika msimu mmoja, klabu hiyo ya Uingereza imefanikiwa kuwahakikisha wachezaji na mkufunzi wao kwamba daima watafurahia ufahari huo.
Ongeza ukweli kwamba wapinzani wao Manchester United, wamefanikiwa kushinda mataji matatu mara moja tu katika msimu wa 1998-99, wakati huo City ikiwa daraja la chini, na mafanikio haya makubwa katika safari ya mchezo wa soka yamekuwa wazi.
City imeishinda mara kadhaa United kabla ya kwenda Istanbul, lakini ushindi huu umeongeza mtetemeko wa kuhama wa uwiano wa nguvu za mchezo huo katika jiji la Manchester na Ulaya yote, ambako wengi waliamini Pep Guardiola atatawala kama vile watu wa England wanavyoamini hivyo.
Ushindi wa Istanbul ni mafanikio makubwa kwa uwekezaji kutoka Mashariki ya kati katika soka. Kuna mambo mengi ya kuyahusudu, ikiwemo namna City ilivyocheza, ufundishaji wa Guardiola, na muundo wao wa uchezaji.
Timu ya Manchester City ya chini ya miaka 18 hivi karibuni iliandika historia ya kuwa timu ya mwanzo kushinda makombe mara tatu mfululizo. City chini ya miaka 21 wameshinda mara tatu mfululizo katika ligi yao.
Na mwaka 2016, City ilianzisha timu ya wanawake nao pia wameshinda kombe la FA mara tatu na kombe la wanawake la Super League mara moja.
Sheikh Mansour, utajiri wake umeleta neema kwa klabu hiyo, ikiwa ni mechi ya pili kuhudhuria tangu aichukue timu hiyo mwaka 2008 kupitia uwekezaji wa Abu Dhabi Investment Group, ulikuwa ni ukumbusho wa wazi wa baadhi ya maswali na mambo muhimu kuhusu washindi hao wapya wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ukweli kwamba Mansour, Naibu Waziri mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE), alihudhuria mechi hiyo kwa mara ya kwanza tangu kupita kipindi cha miaka 13, iliibua maswali mengi kuhusu msukumo wake wa uwekezaji.
Watetezi wa haki za binaadamu wanaamini klabu hiyo inatumiwa kusafisha kile ambacho Amnesty wamekiita ‘picha mbaya’ ya taifa hilo tajiri kwa mafuta.
Mwezi ulipita, zaidi ya mashirika arobaini yasiyo ya kiserikali, yaliituhumu UAE kwa kuendelea kukiuka haki za binaadamu na uhuru, ikiwemo kuwalenga wanaharakati wa haki za binaadamu, kuanzisha sheria kandamizi, kutumia mfumo wa kisheria kuondoa harakati za haki za binaadamu.
UAC pia ni msalishaji mkubwa wa hewa mkaa.
Lakini kuna ushahidi kuhusu uwekezaji wake kuongeza thamani kwa City. Takribani pauni bilioni 1.5 zimetumiwa kununua wachezaji wapya tangu 2008. Mansour aliinunua City kwa pauni milioni 200, na imepanda thamani ikikadiriwa kufikia pauni bilioni 4, na faida ya pauni milioni 42 ilitangazwa mwaka jana.
Pia kumekuwa na juhudi mpya za ushirikiano wa kimataifa wa UAE kuhusu uhusiano wa Abu Dhabi na utawala wa rais Vladimir Putin wa Urusi.
Machi, serikali ya Marekani ilisema ilikuwa na mashaka kampuni za UAE zimepeleka bidhaa za thamani ya mamilioni ya pauni kwa Urusi, kuisaidia nchi hiyo kupambana na vikwazo vya kimataifa.
Mwaka ulipotia, UAE ilijizuia kupiga kura iliyoongozwa na Marekani katika Umoja wa Mataifa, ya kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Na mwezi Oktoba, Putin alipongeza uhusiano wa Urusi na UAE katika mkutano na rais wa nchi hiyo, Sheikh Mohamed Bin Zayed Al Nahyan.
'MBZ' anajuulikana kuwa mtawala wa Abu Dhabi, ambaye alikuwa ameketi pembeni ya kaka yake, Sheikh Mansour wakati wa fainali ya klabu bingwa Ulaya.
UAE imekuwa mshirika muhimu miongoni mwa nchi za kiarabu, nchi hiyo ikifanya biashara ya mabilioni pauni na Uingereza. Lakini mwaka jana, serikali ya Uingereza ilimkosoa Mansour baada ya mkutano wake na rais wa Syria, Bashar Al Assad.
Msemaji wa ofisi ya mambo ya nje alisema, kulingana na nyakati, mkutano huo unahujumu ustawi na amani ya Syria. City haikujibu ombi la kuzungumzia jambo hilo. Bashar na utawala wake uko chini ya vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sio tu siasa za kimataifa zinazofanya umiliki wa Abu Dhabi wa klabu hiyo kuwa wa utata. Pia, ushindi wa mataji matatu, City inajulikana kwa zaidi ya tuhuma 100 za uvunjifu wa kanuni za kifedha kati ya 2009 na 2018, ambapo Ligi Kuu ya Uingereza ikiishutumu timu hiyo.
City pia ilituhumiwa kutotoa ushirikiano wakati wa uchunguzi. Kwa mujibu wa wataalamu, ligi hiyo ina malalamiko kuhusu mapato ya ufadhili ya wamiliki wa City. Ila City inakana kosa lolote, wanasema wana ushahidi usiopingika kwamba hawana hatia.
Mwaka 2020 walifanikiwa kuipindua marufuku ya UeFa ya kutoshiriki mashindano ya Ulaya kwa miaka miwili kwa kukiuka kanuni za matumizi ya pesa. Mahakama ya usuluhishi iliondoa katazo hilo baada ya kuikuta klabu haijavunja kanuni hizo. Ingawa City ilipigwa faini kwa kushindwa kushirikiana na UeFa.
Pia kuna kesi ya Ligi ya Uingereza inayo weza kuchukua miaka – inayohusu kwa namna gani City imefikia mafanikio yake.
Hayo yote yanaongeza maswali kwa wale wenye mashaka kutawala kwa City na utajiri ambao unaweza kuathiri ushindani katika soka – kwamba ligi kuu ya Uingereza inaanza kutabirika Manchester City ikishinda mara tano kati ya misimu sita iliyopita.
Mashabiki wa City ambao wanafurahia mafanikio yao ya Istanbul, na wale ambao huwepo Etihad kuangalia timu yao ikiichabanga timu kubwa kama Arsenal na Real Mdrid.
Wale waliopigwa na mvua kushuhudia gwaride la ushindi la City. Hasa wale ambao ni wazee kukumbuka miaka ambayo Manchester United ilikuwa ikitawala.
Wengi wao, ingawa sio wote wanaamini ukosoaji wa City unatokana na wivu, na kujenga hoja kwamba vilabu vingine pia vimepitia kutawala kama huko katika kipindi cha nyuma. Na vilabu vyengine vya soka vimetumia kiasi sawa cha pesa bila ya kupata mafanikio ambayo City imeyapata.
Wanaamini City inapaswa kushangiliwa. Lakini bado kuna mengi ya kupatiwa jawabu, na mengi ya kuyajadili kuhusu wale wanaomiliki timu hiyo.












