Usafiri wa Anga: 'Ghostflights' ni nini? kwanini ndege hizi huzunguka tupu?

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ghostflights ni ndege tupu zinazozunguka

Je, ndege inaweza kuruka tupu bila hata mtu mmoja ndani?

Ili kuendesha ndege, rubani na wahudumu wengine wanapaswa kulipwa na mafuta lazima yanunuliwe. Inagharimu sana.

Na licha ya hali hiyo, kwa nini baadhi ya ndege husafiri bila mizigo au bila abiria?

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ndege tupu

Je, hii inafanyika kweli?

Hakika hutokea. Mamia ya ndege huruka tupu huko Ulaya kila mwezi. Hizi zinaitwa ndege tupo au ghost flights

Takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na 'safari nyingi kama hizi za ndege' huko Amerika Kusini au Caribbean katika miaka michache iliyopita. Pamoja na ujio wa janga la Corona na kuongezeka kwa vikwazo vya usafiri, tatizo hili limezidi katika kanda hiyo.

Viwanja vingi vya ndege vinapaswa kuweka 80% ya safari za ndege zilizopangwa ili kudumisha nafasi zao za kupaa na kutua. Kuna kiasi cha kughairiwa cha 20% ya safari za ndege.

Ikiwa safari za ndege hazipatikani ndani ya asilimia hizi, mashirika ya ndege yatalazimika kutumia ndege tupu ili kudhibiti viwanja vyao vya ndege bila kughairi safari zilizopangwa. Vinginevyo, wanaweza kuhatarisha 'saa bora zaidi za kibiashara' kwenye viwanja hivyo vya ndege mwaka unaofuata.

Kuondoka saa kumi na mbili asubuhi huko London kamwe sio sawa na kupaa saa mbili au tatu asubuhi.

Pia, kutua Madrid saa 1 asubuhi na kutua saa 5 usiku havifanani. Wasafiri watateseka ikiwa hakuna muunganisho wa katikati mwa jiji wakati vituo vya usafiri wa chini vimefungwa.

Pia bei sio sawa wakati huu.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwanja wa ndege

"Uitumie au uiache"

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tume ya Ulaya na Shirikisho la Usafiri wa Anga (FAA) ya Marekani hutumia sheria ya "kutumia nafasi au iache'' ili kudhibiti kasi ya safari zote za ndege kwenye viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi.

Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI) linafafanua kama "Ndege tupu ni safari za ndege zinazoendeshwa kwa hiari na mashirika ya ndege ili kuhifadhi haki zao za maeneo yanayopangwa."

Kuhusiana na serikali na viwanja vya ndege, kampuni hii inasema, “Ndege hizo haziuzi tikiti. Hazibebi abiria wala mizigo. Hakutakuwa na mapato kutoka kwa ndege hizo, "alifichua.

Watu wengi wanasema kwamba ndege hizo hazimnufaishi mtu yeyote na ni utaratibu usiohitajika na usio na maana.

Badala yake, wataalam wanasema ugawaji ulioratibiwa wa maeneo ya viwanja vya ndege unaweza kuongeza ushindani kati ya mashirika ya ndege, na hivyo kuwanufaisha abiria.

Diego R. González, rais wa Chama cha Wanasheria wa Viwanja vya Ndege Duniani, alisema, "Hakuna matumizi ya kiuchumi ya ndege hizi. Zaidi ya hayo, pia kuna uharibifu mkubwa wa mazingira. Mafuta mengi yanaharibika. Ina hatari kubwa ya uharibifu wa mazingira."

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Treni za chini na huduma za anga zinapaswa kushirikiana na kila mmoja

Mashirika ya Ndege ya Kawaida - Mashirika ya ndege ya gharama nafuu

Ni muhimu sana kuona safari ya ndege kama ya kibiashara.

"Nafasi hizo zimepangwa kulingana na muda na zamu. Kushindwa kuzitumia husababisha kutozwa faini. Mamlaka ya uwanja wa ndege itakabidhi kwa kampuni nyingine mwaka ujao. Hii inaweka mashirika ya ndege katika hatari ya kupoteza sehemu yao ya soko," Gonzalez alisema.

Chama cha Wanasheria wa Viwanja vya Ndege Duniani kilisema kuwa kuna ushindani kati ya mashirika ya ndege wa zamani na wapya, lakini wanawahimiza kuzingatia sheria hata kama watalazimika kuruka bila kitu.

"Mashirika ya ndege ambayo yanatawala soko yanaendesha ratiba bora zaidi kwa sababu ndio ghali zaidi. Wanafika katika viwanja vya ndege wakati muhimu na kwa urahisi," Gonzalez alisema.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya mashirika ya ndege hutumia safari za ndege tupu ili kuokoa ratiba

"Ikiwa mtoa huduma mkuu hana ushindani kwa wakati fulani, haitapunguza bei," Gonzalez alisema.

Mkurugenzi wa Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga Willie Walsh alisema baadhi ya ndege hulazimika kufanya kazi na abiria wachache au bila ili zisipoteze nafasi iliyopangwa kwa ajili ya kuruka.

"Mtoa huduma anayeendesha safari za ndege kati ya viwanja viwili vya ndege ataomba ruhusa kutoka kwa viwanja vyote viwili vya ndege wakati hana uwezo wa kuendesha huduma hiyo. Vinginevyo tutalazimika kurusha ndege," alisema Walsh.

Mashirika ya ndege yanataka yasibughuziwe na sheria hizi.

Hata hivyo, watu kutoka sekta hiyo wanasema kuwa badala ya kuendesha safari hizo za ndege zikiwa tupu, ni bora kuchukua abiria kwa nauli ndogo na kuendesha huduma hizo. Kwa kweli ni jambo la kuzingatia.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uwanja wa ndege

Kusaidia mazingira

Kanuni kama hizo katika sekta ya anga pia zinaathiri mazingira. Sekta ya usafiri wa anga inachangia takriban asilimia 2 ya uzalishaji wa kaboni duniani. Sekta hii inachangia asilimia 3.5 ya ongezeko la joto duniani kutokana na shughuli za binadamu.

Aidha, ni sekta inayokua. Ikiwa hali itaendelea hivi, kuna hatari kwamba asilimia hizi zitaongezeka zaidi katika siku zijazo.

Kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA), tangu 2000, uzalishaji huu umeongezeka kwa 50%. Sekta hiyo inatarajiwa kukua kwa zaidi ya 4% kila mwaka kwa miongo miwili ijayo.

Kulingana na Greenpeace "uzalishaji wa kaboni kila mwaka kutoka kwa ndege hizi tupu huko Ulaya ni sawa na uzalishaji wa kaboni kutoka katika magari milioni 1.4.

Sekta ya usafiri wa anga imetangaza dhamira ya kutotoa hewa chafu ya kaboni ifikapo mwaka wa 2050. Katika hali kama hizi, hitaji la kupunguza safari hizi za anga inaonekana kuwa kubwa zaidi.