Miaka 10 ya Kim Jong-un madarakani, Korea Kaskazini imetengwa zaidi

Kim Jong-un

Sauti ya vilio inafurika mitaa ya Pyongyang.

Vikundi vya wanafunzi waliovaa sare wanapiga magoti. Picha zinaonyesha wanawake mikono vifuani mwao wakiwa wamekata tama.

Vyombo vya habari vya serikali ambavyo kawaida viko chini ya udhibiti wa serikali, vimetangaza kifo cha kiongozi mpendwa mwenye miaka 69 Kim Jong-il. Tarehe ni Desemba 19, 2011.

Akiwa na miaka 27 alikuwa ametambuliwa kama mrithi mkuu. Lakini itakuwaje nchi yenye inaangalia sana umri na ujuzi ikatawaliwe na mtu ambaye hana yote hayo? Wengi walitabiri mapinduzi ya kijeshi na hatua kutoka kwa wasomi wa Korea Kaskazini

Lakini dunia ilimdharau dikiteta huyo mchanga. Hadi sasa Kim Jong-un hajafanikiwa tu kuimariaha nafasi yake Lakini pia ameongaza nchi kwenda kipindi kipya kinachotajwa kama cha Kim Jong-unism.

Alianza kwa kuwaondoa washindani wake na kulikuwa na mamia ya mauaji na kisha akgeukiwa masuala ya kimataifa. Majaribio manne ya zana za nukulia, maajaribio 100 ya makombora ya masafa marefu na mazungumzo yake na aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump.

Lakini mbio zake za kumilikiz zana za nuklia zimekuja na gharama zake na Korea Kaskania sasa iko kwenye matatizo, maskini zaidi na imetengwa zaidi kuliko ilivyokuwa wakati aliingia madarakani.

Raia kumi waliokimbia Korea Kaskazini akiwemo mmoja aliyekuwa mwakilishi wa kidiplomsia wa ngazi ya juu wanazungumza jinsi hali imekuwa katika kipindi cha miaka 10 ya Kim Jon-un.

Mwanzo mpya

Siku baba yake Kim Jong-un alifariki, mwanafunzi Kim Geum-hyok alifanya kitu ambacho kingeweza kumgharimu maisha yake. Aliandaa karamu.

"Iliwa hatari sana, Lakini tulikuwa na furaha kubwa wakati huo…,"anasema

Kwake, kiongozi mpya na mchanga, anayejulikana kwa kupenda kuteleza kwenye theluji na mpira wa kikapu, kilichochea matumaini kuwa mabadiliko yalikuwa njiani.

"Tulikuwa na matumaini kwa Kim Jong-un. Alisomea Ulaya, kwa hivyo huenda alifikiri kama sisi," alisema.

Kim Jong-il y su hijo Kim Jong-un

Geum-hyok anatoka familia ya wasomi na alikuwa akisomea Beijing wakati huo, fursa ambayo watu wachache nchini Korea Kaskazini wanaweza kuipata.

Kuishi kwake China kulifungua machao yake kuhusu maendeleo yaliyo duniani na alitafuta mitandaoni kwa habari kuhusu nchi yake.

"Kwanza sikuamini. Niliamini kuwa nchi za magharibi zilikuwa zinadanganya kuhusu Korea Kaskazini. Ubongo wangu uliniambia auhitaji kutazana habari zaidi lakini roho yangu ilitaka kutazama zaidi."

Korea Kaskazinia ina watu milioni 25 walio chini ya vizuizi vikali ambapo watu wengine hawajui ni kipi kinaendelea duniani au vile nchi yao inazungumziwa huko nje,.

Pia waliamini kuwa kiongozi wao ni kiumbe safi aliyestahili zawadi safi na utiifu wa hali ya juu.

Wenye shaka

Ryu Hyun-woo balozi wa zamani wa Korea Kaskazini nchini Kuwait aliiambia BBC kuwa wafanyakazi wenzake walikasirishwa na kuhamishwa madaraka kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto.

Raia wa Korea Kaskazini walikuwa wanachoshwa na uongozi wa urithi, hata miongoni mwa wasomi. Tulitaka kitu kimpya. "Tulifikiri, Nitaweza kuanza kitu tofauti?"

Familia ya Kim imeitawala Korea Kaskazini tangu nchi hiyo iundwe mwaka 1948. Watu wanafikiri kuwa damu yao ni takatifu. Ni kama njia ya kuhalalisha nasaba.

Ahadi

Kwenye hotuba ya mwaka 2012 kiongozi huyo mpya aliahidi kuwa raia wa korea Kaskania "hawatakaza mikanda yao tena."

Kwa watu wa nchi ambayo ilikuwa na njaa iligharimu maisha ya maelfu ya watu miaka ya tisini, ilionekana kuwa kiongozi huyo mpya alitaka kumaliza uhaba wa chakula a mateso.

Mujeres haciendo cola para recibir comida en Corea del Norte.

Maafisa waliamrishwa kufanikisha uwekezaji zaidi wa kimataifa. Na baadhi ndani ya nchi wakaanza kuona mabadiliko.

Dereva Yoo Seong-ju, kutoka mkoa ulio pwani ya mashariki, anasema walianza kuona bidhaa zaidi za Korea Kaskazini kwenye maduka ya jumla.

Kusafisha

Mambo mazuri kutoka kwake Kim hayakuwafikia watu aliowaona kama tisho.

Mjomba wake Jang Song Thaek alikua amejenga washirika wenye nguvu.

Kilomita mamia kadhaa kutoka Pyongyang, kaskazini mwa nchi na karibu na mpaka na China, mfanyabiashara Choi Na-rae alijiuliza iwapo Jang Song-thaek angeweza kuwa kiongozi mpya wa nchi.

"Wengi wetu tulikuwa na matumaini kuwa nchi ingefunguka kwa China na tuweza kusafiri bila tatizo kwenda ng'ambo," anakumbuka

"Tulifikiri kuwa iwapo Jang angerithi , ingeleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini Korea Kaskazini"

Jang Song-thaek alibandikwa jina "takataka ya mwanadamu" na "mbaya zaidi kuliko mbwa" na baadaye akanyongwa kwa madai kuwa alidhoofisha umoja wa chama.

Kiongozi mchanga akaonyesha ukatili wa hali ya juu.

kuchukua udhibiti

Watu kadhaa walivuka mpaka na kuingia china kutafuta usalama.

Kiongozi akaamua kuzuia watu kuvuka na ulinzi ukaongezwa mpakani kuliko awali.

Ha Jin-woo alifanikiwa kuwavusha watu 100 kutoka Korea Kaskazini.

Frontera de Corea del Norte

Mtu maarufu

Licha ya kuwawekea shinikizo watoro na wale waliohama nchi, Kim Jon-un alijaribu kuonekana mwenye urafiki kuliko baba yake.

Akamuo Ri Sol-ju na kuzuru miji na majiji akiwakumbatia na kuwasalimia wenyeji.

Wanandoa hao walizuru maduka ya urembo na kuonyesha bidhaa za ufahari.

Lakini raia wa kawaida kujaribu kuishi maisha ya kisasa ni "haramu."

Yoon Mi-so alitaka kufuata mienendo aliyogundua kwenye santuri zilizoingizwa kisiri kutoka Korea Kusini. Aliota kuvaa pete, mkufu au jeans

Serikali inazuia haya kwa sababu inaogopa ushawishi wa nchi za kigeni. Sheria za kuzuia ni ishara kuwa hawana imani na utawala wao.

Misiles.

Mwaka 2016 kwenye wizara ya mashauri ya nchi za kigeni, Balozi Ryu alipata amri mpya. Msisitizo haungekuwa kwenye biashara tu.

"Tungeeleza ni kwa nini Korea Kaskani ilihitaji zana za nuklia."

Matumaini yalikuwa ni iwapo wanadiplomasia wangezungumza kuhusu hilo, wazo hatimaye lingekuja kuwa suala la kawaida katika jamii ya kimataifa.

Haikuwa hivyo.

Mchezo mkubwa wa "mtu wa roketi"

Vitisho kati ya Donald Trump na Kim Jong-un viliishia kwa maonyesho ya kidiplomasia

Kim y Trump

Magazeti ya Korea Kaskazini yakachapisha salamu za mkono kati ya Trump na Kim huko Singapore kwenye kurasa za mbele

Lakini vikwazo vya kuzuia mpango wa nyuklia ya nchi hiyi vikaanza kuumiza. Na malalamiko vijijni nje ya pyongyang yakazimwa.

Mwishowe hakukuwa na makubaliano. Balozi Ryu anaamini kuwa ilikuwa mikatai ya kupata unafuu kutoka kwa vikwazo.

"Korea Kaskani haiwezi kuachilia hizi silaha kwa sababu inaziona kama muhimu kwa kuendeleza utawala."

Mapinduzi ya covid

Lakini wakati mbaya zaidi kwa Kim ulikuwa njiani.

Wakati janga la Covid lilizuka kwa jirani wake China Januari 2020, Korea Kaskazini ilifunga milango yake kwa watu na bidhaa.

Chakula na madawa vilikuwa vinarundika kwenye kituo cha Dandong. Zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa huingia kutoka China.

Tangu COVID iwasili mambo mengi yamebadilika, anasema Ju Seong aliyekuwa akifanya kazi kama dereva nchini Korea Kaskazini. Amefanikiwa kuongea kwa muda mfupi na mama yake karibu na mpaka wa China.

Uchumi unadorora na bei zinapanda. Maisha yamekuwa magumu zaidi.

Kuna ripoti za baadhi ya watu kufariki kutokana na njaa

Kim Jong-un mwenyewe ameieleza hali kuwa mbaya sana, na akaja kulia akitoa hotuba, kitu kisichotarajiwa kutoka kiongozi wa Korea Kaskazini.

Dr Kim Sung-hui anakumbuka kutoka nyakati zake huko kuwa madawa mengi hayapatikani.

Viumba vya upasuaji wakati mwingine havikuwa na mwangaza na madaktari walifanya kazi mikono mitupu bila glovu.

Mahehebu ya Kim

Baadhi ya wale walihama nchi wanasema wana wasiwasi na hali iliyopa na wanatarajia mapinduzi kufanyika karibuni. Lakini haku dalili kuwa hilo linaweza kutokea.

Desertores que prestaron su testimonio a la BBC.

Madhehebu ya familia ya Kim yamefichuliwa na yamebaki. Utabiri wote wa awali wa kuporomoka kwa utawala umefeli.

Wengi wa wale waliohojiwa wangependa kuona mipaka ikifunguliwa kuruhusu watu wake kutembea bila tatizo baada ya miaka 70 ya kufungiwa. Wengi wanataka tena kuona familia zao.