Kim Jong-un aonekana hadharani, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimeripoti

North Korea's leader Kim Jong-un pictured by state media opening a fertiliser factory on 1 May 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vyombo vya habari vilionyesha picha hiiiliyoonyesha Kim Jong-un akizindua kiwanda cha mbolea Ijumaa

Kim Jong-un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya siku 20, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema.

Shirika la habari la KCNA limeripoti kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskanzini alikata utepe katika ufunguzi wa kiwanda cha mbolea.

Liliongeza kuwa watu katika kiwanda hicho '' walimshangilia shangwe kubwa" alipojitokeza siku ya Ijumaa.

Taarifa za kuonekana kwake-mara ya kwanza tangu alipoonekana katika tukio kwenye vyombo vya habari vya taifa hilo tarehe 12 Aprili- zinakuja huku kukiwa na tetesi kote duniani kuhusu afya yake.

Taarifa za hivi punde kutokavyombo vya habari vya taifa la Korea Kaskazini hazikuweza kuthibitishwa.

Vyombo vya habari baadae vilitangaza picha ambazo zilionyesha Bwana Kim akikata utepe nje ya kiwanda.

Alipoulizwa kuhusu taariofa za kuonekana kwa Kim, rais wa Marekanai Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa asingetaka bado kuzungumzia lolote juu ya taarifa hizo.

Je rip[oti ya vyombo vya habari vya taifa inasemaje?

Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa- Korean Central News Agency (KCNA), Bwana Kim aliambatana na maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, mkiwemo dada yake Kim Yo Jong.

Kiongozi wa Korea Kaskazini akakata utepe katika sherehe iliyofanyika katika kiwanda, katika jimbo la kaskazini mwa nchi la Pyongyang, na watu waliohudhuria tukio hilo " walimshangilia kwa shangwe kubwa ' kiongozi huyo wa ngazi ya juu ambaye anawaamuru watu wote kwa ujumla kutimiza jukumu zuri la mafanikio ", KCNA ilisema.

Kim Jong-un pictured by state media opening a fertiliser factory 1 May 2020

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, "Kelele za shangwe kubwa '" zilisikika wakati kiwanda kilipofunguliwa, kwa mujibu wa KCNA

Bwana Kim alisema kuwa ameridhishwa na mfum wa uzalishaji wa kiwanda, na akakisifu kwa kuchangia katika maendeleo ya viwanda vya kemikali na uzalishaji wa chakula, liliongeza shirika hilo

Ni nini kilichoibua tetesi kuhusu afya yake?

Tetesi kuhusu afya ya Kim zilianza baada ya kukosa katika sherehe za maadhimisho ya sikuuu ya kuzaliwa ya babu yake, muasisi wa taifa Kim Il Sung tarehe 15 Aprili.

Kumbukumbu hiyo ni moja ya matukio makubwa katika kalenda ya Korea Kaskazini, na Bwana Kim kwa kawaida huadhimisha siku hii kwa kutembelea katika eneo la makumbusho yenye mnara ambako babu yake amezikwa. Bwana Kim hajawahi kukosa kuhudhuria tukio hili.

Madai kuhusu kuugua kwa Bwana Kim, yaliandikwa katika tovuti ya muasi wa Korea Kaskazini.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kufahamika kiliiambia Daily NK kuwa "wana taarifa kuhusu matatizo yake ya kiafya langu mwaka jana mwezi Agosti, lakini tatizo limezidi kuwa kubwa baada ya kurudia kutembelea mlima Paektu".

Hii imevifanya vyombo vingine vya habari vya kimataifa kuripoti kwa kutegemea chanzo kimoja.

Wakala wapya wa habari wakaanza kuja na madai kuwa ndio hicho walichokuwa nacho mpaka ripoti kutoka kikosi cha ujasusi kilichopo Korea Kusini na Marekani kufuatilia madai hayo.

Lakini wakaja na kichwa cha habari cha taharuki zaidi kutoka vyobo vya habari vya Marekani kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini yuko kwenye hali ya mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Celebration of Kim Il-sung's birth anniversary on 15 April

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kim Jong-un hajawahi kukosa kuhudhuria kumbukumbu za siku ya kuzaliwa ya babu yake awali

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alikuja kuongeza chumvi tetesi hizo kwa kusema hadharani tarehe 29 Aprili kuwa hawajamuona Bwana Kim hivi karibuni.

Ingawa taarifa kutoka serikali ya South Korea na taarifa kutoka wana intelijensia wa China alizungumza na wakala wa habari- Reuters - kusema kuwa hakuna ukweli wowote katika hilo.

Je Kim Jong-un aliwahi kutoonekana kwa muda hapo awali?

Ndio bwana Kim aliwahi kupotea kwa muda wa siku 40 mnamo Septemba 2014, baada ya kuhudhuria tamasha. Na akaonekana tena katikati ya mwezi Oktoba akiwa anatumia fimbo.

Chombo cha habari cha taifa hilo hakikuwahi kuelezea alikuwa wapi. Lakini kikosi cha ujasusi cha South Korea kilisema kuwa labda walikuwa anafanyiwa operesheni ya goti lake ambalo lilipata shida.

Bwana Kim Jong-akiwa anapanda mlima Paektu

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bwana Kim Jong-akiwa anapanda mlima Paektu

Uchambuzi

Na Laura Bicker

Mwandishi wa BBC Seoul

Tahadhari huwa inawekwa katika kuripoti taarifa kuhusu North Korea. Chanzo cha habari ni kidogo, na tetesi ndio zinakuwa zinavuma zaidi na kusababisha vichwa vya habari kuhusu Kim Jong-un kuwavutia watu wengi. Ni ngumu sana kupata ripoti sahihi kutokana na usiri wa taifa hilo.

Ukweli na vyanzo vya habari ni ngumu kupatikana haswa tangu taifa hilo kuwa limefungwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Serikali ya South Korea ilikuwa wazi kusema kuwa imebaini kuwa Nort Korea haifanyi shughuli zake kama kawaida.

Seoul huwa ina kitengo cha majasusi wazuri kutoka Pyongyang. Lakini hata wao wamekuwa wakikosea hapo nyuma.Tuwe wazi kuwa Kim Jong-un alikuwa anaugua au alifanyiwa upasuaji wiki mbili zilizopita.

Au alikuwa mapumzikoni akiicheka dunia kwa utabiri wao mbaya.

Kutoonekana kwake kwa siku 20 bila maelezo yoyote bado kuna maswali mengi kuhulizwa kuhusu mridhi wake na mipango yake ni ipi kama chochote kikitokea kwake.

Lakini kuna jambo moja ambalo halipo katika haya yote, North Korea ni zaidi ya mwanaume mmoja .Ni taifa ambalo lina watu milioni 25 ambao wamekuwa wamefungiwa.

Leo Bwana Kim kutoonekana ilikuwa kama mmea ambao uliorutubishwa kunyauka. Vichwa vya habari vikasababisha kurejea kwake lakini alikuwa wapi na je vita vitaweza kusaidia taifa lake kukomboka katika uhaba mkubwa wa chakula. Ninawahakikishia kuwa watu wa North Korea sasa hivi, kuwa hilo ni jambo muhimu zaidi ya kujua kiongozi wao alikuwa wapi.