Je, FW de Klerk alikuwa shujaa aliyemaliza ubaguzi wa rangi au alipaswa kushtakiwa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa baadhi ya raia wa Afrika Kusini , FW de Klerk alikuwa kiongozi mzuri ambaye alipewa tuzo ya amani ya Nobel, kwa kusaidia kusitisha mfumo wa ubaguzi wa rangi ambao ulikuwa umehalalishwa na ambao aliurithi.
Kwa wengine wanaona alistahili kufunguliwa mashtaka kwa kuwa alikuwa na makosa wengi.
Kiukweli alikuwa mtu aliyekuwa sehemu nyingi.
Klerk ambaye amekufa akiwa na miaka 85-alikuwa rais wa mwisho wa ubaguzi wa rangi. Wakati alipokuwa madarakani , vikosi vya usalama vilikuwa vinakabiliana na raia weusi wa Afrika kusini ambao walitaka kukomesha utawala wa wazungu ambao walikuwa wachache katika taifa hilo-huku wakipigania kuachiwa huru kwa Nelson Mandela na viongozi wengine ambao walikuwa wamefungwa gerezani.
Ubaguzi wa rangi haujaisha muda mrefu na bado upo sana Afrika Kusini , si kwasababu hakuna mtu ambaye ameshitakiwa kwa sababu ya mashtaka ya uhalifu wa jinai ambao ulifanyika wakati ule.
Uhalifu ulifanyika , na waliofanya uhalifu walikuwa wanaweza kufuatiliwa lakini hakukuwa na uhalifu , naona.
Raia wengi wa Afrika Kusini walifanya kampeni za muda mrefu dhidi ya mfumo wa utawala wa watu weupe walio wachache.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Wengine wakiamini kuwa De Klerk angeweza kufanya maamuzi mazuri zaidi kuleta mabadiliko na kuhakikisha kuwa mfumo wa ubaguzi wa rangi unawajibika kwa kile walichokifanya dhidi ya watu weusi na ghasia zilizosababishwa na serikali yake, na hata alipaswa kufikishwa kwa vyombo vya sheria.
Alihusika kwa miongo mingi, kwa kuwa madarakani katika mfumo wa rangi na amejinufaisha kwa miaka mingi.
'Wakati wa mabadiliko'
Mwanasheria ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Chama cha taifa tangu mwaka 1972, De Klerk alikuwa na uelewa thabiti wa chama kilichounda ubaguzi wa rangi, na alipata fursa ya kufanya kazi ndani ya muundo huo katika ngazi ya juu, ingawa alikuwa na msimamo tofauti kidogo na watangulizi wake.
Labda ndio maana aliweza kuwaelekeza kwa umakini hata watu waliokuwa wanatetea mfumo wa ubaguzi wa rangi ndani ya chama chake katika meza ya mazungumzo ambapo Mandela alikuwa akitoa nafasi ya kusaidia kuijenga upya nchi - njia ya majadiliano ambayo wengi waliamini ingesababisha umwagaji damu.
Taasisi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu ilitambua mchango wake katika kipindi cha mpito cha demokrasia:
"Hayati FW De Klerk alikuwa na jukumu muhimu katika historia ya Afrika Kusini. Wakati ambao si wenzake wote waliona hali ya baadaye ya nchi ikitokea kwa njia ile ile, alitambua wakati wa mabadiliko na akaonesha nia ya kuchukua hatua katika hilo."
Heshima aliyopata Nelson Mandela, ambapo De Klerk alishiriki naye kupata Tuzo ya Amani ya Nobel, walimweleza waziwazi kama mtu mwenye "heshima kubwa" lakini pia "usio sawa".

Chanzo cha picha, Getty Images
De Klerk alichagua kufanya mazungumzo na African National Congress (ANC) wakati ambapo nchi nyingi duniani na washirika wa zamani walikuwa wamekipinga Chama cha Taifa na serikali yao ilikuwa imefilisika.
Wakosoaji wanasema alikuwa mtaalamu zaidi wa ushawishi na hakuwa na chaguo lingine.
Katika kitabu chake , Long Walk to Freedom, Mandela alikuwa wazi kabisa: "Licha ya kwamba alionekana kuchukua hatua, lakini bwana de Klerk hakuwa mkombozi wao.
"Hakufanya mageuzi yake yoyote kwa nia ya kujiondoa madarakani. Alifanya mambo kinyume kabisa kuhakikisha anaukandamiza utawala mpya wa mwafrika.
Alikuwa muoga na msaliti
Hata hivyo, uamuzi wake ulimtenga na wengi katika chama chake na miaka baadaye baadhi ya jamii yake ya Kiafrika bado walimwona De Klerk kama msaliti.
Miaka michache iliyopita nilitembelea mji wanaoishi wazungu pekee - nyumbani kwa watu waliochukizwa na ndoto kama "taifa la upinde wa mvua", wakichagua kuishi peke yao.
Huko kwenye kilima, katika mji mdogo ambapo bendera iliyopeperushwa ilikuwa ya zamani ya wakati wa ubaguzi wa rangi na sanamu za shaba za viongozi wa zamani wa serikali ya ubaguzi wa rangi zilionyeshwa kwa fahari, ingawa De Klerk alikosekana - ilifutwa katika orodha yao ya "mashujaa".
Watu niliozungumza nao walimwona kuwa muoga, na waliamini kuwa amewasaliti.
Hata hadi mwisho, De Klerk alionekana kutoridhika na nafasi yake nchini Afrika Kusini alipokuwa akipambana na ugonjwa.
Katika ujumbe wa video uliotolewa na taasisi yake mara baada ya kifo chake, De Klerk mwenye sura dhaifu alisema kwamba, wakati aliwahi kuunga mkono mradi wa "maendeleo tofauti" kama alivyouita ubaguzi wa rangi, katika miaka ya 1980 "amebadilika kabisa".

Chanzo cha picha, Getty Images
Alieleza mabadiliko hayo yalimpa moyo safi ambao ulimfanya aweze kukubali kukubali kufanya mazungumzo na Mandela na viongozi wengine wa kisiasa.
Aliongeza kuwa tangu amalize utawala wake amefanya kila awezalo kuendelea kuukemea, hata kukiwa na mashaka.
"Niruhusu leo katika ujumbe huu wa mwisho nirudie: Mimi, bila sifa, naomba radhi kwa maumivu na maudhi na fedheha na uharibifu ambao ubaguzi wa rangi umefanya kwa weusi na Wahindi nchini Afrika Kusini," De Klerk alisema katika video iliyopewa jina. "ujumbe wake wa mwisho".
Kwa waafrika kusini wengi, utawala wa ubaguzi umesababisha mamilioni ya watu nchini Afrik akusini kuishi katika umasikini na kutokuepo kwa usawa.
Baadhi wanaamini kuwa hakufanya jitihada za kutosho kwa sababu hakusema kuwa ubaguzi bado unaendelea bila kupata hukumu yake - kufariki kwa bwana De Klerk kunaacha maswali mengi bila majibu .
"De Klerk alikaa katika mkutano wa baraza la usalama la taifa hatima ya Matthew Goniwe and Fort Calata ya mwaka 1984 na 1985," salisema Lukhanyo Calata wa taasisi ya Fort Calata.
Baba yake Fort Calata, alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na polisi wa ubaguzi wa rangi alimuua yeye pamoja na Matthew Goniwe na wanaume wengine wawili mnamo 1985 .
Amefuatilia kwa miaka mingi , kuwapatia haki na mwezi Juni mwaka huu mahakama ilitaka mauaji ya ubaguzi kuchunguzwa.
Hukumu bado haijatolewa.
"Inaumiza sana muhalifu mwingine wa ubaguzi wa rangi amekufa bila kuwajibishwa kwa uhalifu alioufanya " anasema bwana Calata.















