Mabadiliko ya tabia nchi: Vyakula vya kila siku vitaadimika na kuwa na thamani ya juu

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuagiza samaki aina ya kambamti katika migahawa au kupikwa kwenye sherehe inachukuliwa kama moja ya vyakula vya gharama kubwa.Ila wengi wana mtazamo tofauti kuhusu samaki huyu-kambamti ni kitoweo kilichotokea kupendwa zaidi kutokana na ladha yake tamu sanjari na harufu.Katika Karne ya 18, chakula cha kambamti hakikuzingatiwa kama chakula kisichofaa sana na dhana hii ilitokana na matajiri wengi kuacha kutumia kwenye milo yao ya siku.
Mnyama kama Gegereka wanaopatikana kwa wingi kando ya pwani ya mashariki ya Marekani, jambo hili lilifanya wataalamu kumtumia kama mbolea kwenye magereza. Mwanasiasa wa Kentucky John Rowan alidadisi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka ya awali wakati inaanzishwa reli nchini Marekani ndipo samaki aina ya kamba alianza kutumika na pia ustaarabu wa kuwapa wahudumu ulipoanzia na hapo ndipo akaanza kutambulika.Wengi walipeleka vyakula majumbani mwao na ndipo upishi wake ukaanza kuonekana kwenye migahawa ghali zaidi nchini humo.
Mwisho wa Karne ya 19, Kambamti akawa anajulikana kama chakula cha kifahari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vyakula vingine ka kamba, chaza kwa muda mrefu wamekuwa wakipikwa kwenye hafla maalum, haswa kwa sababu ya bei yao ya juu. Chaza walikuwa wakiliwa na maskini zaidi katika jamii katikati ya Karne ya 19. "Walikuwa wengi na bei rahisi ziliongezwa kwenye kitoweo na mikate ili kuziongeza ladha," anasema mwanahistoria wa chakula Polly Russell.
Kufikia mwanzoni mwa Karne ya 20, chaza nchini Uingereza walianza kupungua kwa sababu ya uvuvi kupita kiasi na uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye taka za viwandani. Kadiri walivyozidi kuwa adimu, hadhi yao iliongezeka na walionekana kama kitu maalum, anasema Russell.
Ni tofauti zaidi na bidhaa kama sukari, ambayo zamani ilikuwa ngumu kupatikana na inapatikana tu kwa matajiri.
Vyakula hivi vilipoteza "sura ya anasa" baada ya muda wakati watu walianza kuzilima na, kama matokeo, zikawa chache, anasema Richard Wilk, profesa aliyeibuka wa anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Indiana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matunda na mboga nyingi zilikuwa chache sana kuliko ilivyo leo. Matunda kama vile jordgubbar na raspberries yalikuwa yanapatikana tu wakati wa kiangazi, lakini sasa tunaweza kununua msimu wote wa mwaka. "Hiyo inabadilisha maoni ya kuwa chakula cha watu wenye ukwasi pekee," anasema Peter Alexander, mtafiti mwandamizi katika kilimo cha ulimwengu na usalama wa chakula katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.
Uzito wetu na uhaba wa upatikanaji wa chakula, mara nyingi bei ya vyakula vya hupanda. Aina fulani ya samaki au dagaa inapozidi kuwa adimu, bei hupanda. Thamani iliyoongezeka inawapa watu motisha wa kuvua samaki hii inakuwa ngumu zaidi kuwapata samaki waliobaki ambayo inaweza kusababisha kutoweka kabisa, anasema Wilk.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kumbukumbu za kushiriki chakula cha pamoja majira ya jioni pia huongeza jinsi watu wanavyothamini vyakula, anasema Papies. Mara nyingi vyakula vya anasa husheherekewa na marafiki na familia, kwa mfano wakati wa Krismasi. Kipindi Covid-19 imeingia, kupata chakula na watu wengi likawa jambo la kukimbiwa, anasema Russell.
"Watu walikuwa wakitamani kupika pamoja na kula meza moja," anasema. "Katika ulimwengu ambao rasilimali ni chache na upatikanaji wa chakula ni hatari, uzoefu wa kula chakula pamoja unaweza kuwa anasa."
Vyakula vifuatavyo vya kifahari
Ingawa kihistoria vyakula fulani kama kahawa, Chokoleti na viungo vilikuwa vitu vya kifahari, leo vyakula hivi bado vipo kwenye hadhi ile ile katika nchi nyingi zilizoendelea. Walakini, kuongezeka kwa joto na mvua isiyoaminika inaweza kugeuza hali hii tena kwa miongo michache ijayo.
Mwaka 1828, duka la dawa la Uholanzi Coenraad Johannes van Houten iliweza kugundua mchakato wa maharagwe ya kakao na chumvi za alkali na kutoa chokoleti ya unga ambayo inaweza kuchanganywa na maji.
Utaratibu huu ulibadilisha chokoleti kuwa bidhaa inayonunuliwa ambayo inaweza kuzalishwa kwa wingi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kahawa iliwahi kujulikana kidogo kama utamaduni wa kidini wa Ethiopia, kabla ya wafanyakazi wa ulaya hawajaingia katika biashara hiyo mnamo karne ya 17 na kuanza kuweka utaratibu wa watu kunywa kahawa nyumbani. Baada ya waholanzi kuchukua mbegu ya kahawa, kilimo cha kahawa kikawa maarufu duniani na kuwa kinywaji cha kila siku. Leo hii Chokoleti na kahawa ziko hatarini kuwa ghali na kutopatikana.
"Chokoleti na kahawa zinaweza zisipatikane zote, na kuwa chakula cha kifahari tena kwasababu ya mabadiliko ya tabia nchi," anasema Monika Zurek, mkuu wa utafiti wa mabadiliko ya mazingira katika chuo kikuu cha Oxford.
Maeneo makubwa ya ardhi nchini Ghana na Ivory Coast yanaweza yasiwe mazuri katika uzalishaji wa kokoa tena kama joto litafika kiwango cha nyuzi joto 2C, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2013. "Kakao ilikuwa kwa ajili ya wafalme tu. Mabadiliko ya tabia nchi yameathiri uzalishaji na zao hilo linaweza kuwa la kifahari zaidi ," anasema Zurek.
Mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kuathiri nusu ya ardhi iliyotumika katika uzalishaji wa kahawa duniani ifikapo mwaka 2050, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2015. Utafiti mwingine ulisema maeneo ambayo yalikuwa mazuri kwa uzalishaji wa kahawa huko Latin America yanaweza kupunguza uzalishaji kwa 88% ifikapo 2050 kutokana na ongezeko la joto.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzalishaji wa Vanilla nchini Madagascar umeathirika sana na mabadiliko ya hali ya hewa na kufanya bidhaa hiyo kuwa ya juu.
Kilogramu moja kuuzwa kwa $600 (£434) kiufupi, kiungo hicho kimekuwa ghali na bidhaa nyingi ziko hatarini kuonekana za kifahari kutokana na ugumu wa kuwafikia watu wengi.
Kuacha kula nyama
Si suala la athari za mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa chakula unaweza kutokea kwa kila chakula kuonekana kuwa bidhaa ya kifahari. Watu wanabadili mitazamo yao na hata ladha zinaweza kuathiri aina ya chakula.
"Namna Nyingine ya kufikiria kuhusu chakula cha kifahari , ni kile chakula ambacho huwezi kukila mara kwa mara, " Raats anasema, akitolea mfano wa nyama. Nyama ni sehemu ya chakula cha kawaida kwa watu wengi , kinaweza kuwa chakula cha kifahari kwa miongo michache ijayo wakati mlo huo sasa tayari kuna watu wameanza kula mbogamboga zaidi, alisema.
Watu wanaweza kuchukua hatua pia kwa sababu ya eneo la kulimia limechukuliwa na uzalishaj wa nyama, ambapo linaweza lisitoshe kadiri idadi ya watu inavyoongezeka duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kula nyama kunaweza kupigwa marufuku na kuwa sawa na kuvuta sigara , anasema Alexander. "Itafikia wakati ambao kula burger sio kitu kizuri kufanya hivyo na marafiki zako."
"Kula nyama ni kawaida , imekuwa kama kitambulisho cha taifa ," aliongeza kusema kuwa watu wengi wanaokula mbogamboga kuna wakati wanapata wakati mgumu kwa kuhojiwa kwanini hawali nyama.
Gharama halisi za vyakula vyetu
Katika nia ya kupunguza uzalishaji , nchi zinaweza kuchagua kuongeza kodi katika nyama kwa siku zijazo kama ilivyofanywa na nchi nyingi katika sukari, anasema Alexander.
Jambo ambalo litaongeza bei ya nyama na kufanya bidhaa hiyo kuwa ya kifahari.

Chanzo cha picha, Getty Images













