Sitakubali dhamana itolewe kwa washukiwa wa mauaji , asema Museveni

Rais Museveni amesema kuwa haki za washukiwa lakini haki za waathiriwa zinasahaulika

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Museveni amesema kuwa haki za washukiwa lakini haki za waathiriwa zinasahaulika
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameelezea kutofurahishwa kwake na hatua za polisi na mahakama za kutoa dhamana na hawala kwa washukiwa wa mauaji na makosa mengine makubwa.

"Tatizo lililobakia ni ni baadhi ya maafisa wa mahakama kufanya vitu ambavyo havina uhusiano na uhalisi. Katika ksi ya Masaka, watu wengi sana wamekufa na washukiwa wanapewa dhamana. Na tunaambiwa dhamana ni haki. Dhamana ya wahalifu ni haki. Vipi kuhusu haki za waathiriwa? Hawana haki? Hawana haki ," Museveni alisema.

Rais huyo wa Uganda alikuwa akizungumza katika hotuba yake ya televisheni ya moja kwa moja kwa taifa hilo ambapo alikuwa akizungumzia masuala muhimu ya kitaifa. State Lodge in Nakasero.

Akizungumza moja kwa moja kutoka Ikulu ya Nakasero Bw Museveni alielezea kukasirishwa kwake na jinsi haki za washukiwa zinavyolindwa na kupuuza haki za waathiriwa.

"Ni mshukiwa wa kosa kubwa. Angalia haki yake lakini pia angalia haki ya muathiriwa. Muathiriwa amekufa na mawazo yako yako kwa mshukiwa na hakuna lolote kwa muathiriwa! Hatukupigana kwa ajili ya watu wetu kuuawa na wahalifu na mfumo umeegamia upande wa washukiwa badala ya waathiriwa ," alisema Rais Museveni.

Hawala

Rais huyo wa Uganda pia ameonyesha kukasirishwa na hatua ya polisi wa nchi hiyo kuwapa hawala washukiwa wa mauaji baada ya kukamatwa.

Kulingana na Rais Museveni, sio haki kumuona mtu anayeshutumiwa mauaji akizurura huru katika jamii baada ya kuachiliwa kwa ya polisi.

"Kwa suala polisi, sitakubali suala la hawala. Nitajadili na Mwanasheria Mkuu wa serikali juu ya jinsi ya kuzuia huu upuuzi ," alinukuliwa akisema.

Kipengele cha 17(3) cha sheria ya uhalifu nchini Uganda inasema kuwa kwamba wakati mshukiwa anapopelekwa mahabusu na kuonekana na afisa mkuu wa kituo husika polisi ambaye amepokea kesi kwamba mashitaka hayajakamilia anaweza kumuachilia mshukiwa au kumpatia hawala.

Dhamana itolewe au isitolewe?

Hivi karibuni Rais Museveni amekuwa akishinikiza kuondolewa kwa dhamana kwa watu wanaotuhumiwa kufanya makosa ya jinai husan mauaji.

Kulingana na Bw Museveni, kutoa dhamana kwa watu wanaoshukiwa kufanya mauaji sio haki kwa waathiriwa. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bw Museveni amekuwa akionyesha kulalamikia suala la dhamana kwa washitakiwa na kuahidi kuchukua hatua kukomesha suala hilo:

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Rais Museveni hatahivyo alijipata akitofautiana vikali na Jaji mkuuu wan chi hiyo, Alphonse Owiny Dollo kuhusiana na suala hilo.

Mwanasheria Mkuu Jumatatu alisema kuwa katiba inampatia mamlaka afisa wa mahakama ya kutoa au kumnyima dhamana mshukiwa.

"Afisa wa mahakama haamkii tu upande mbaya wa kitanda na kumkatalia dhamana muombaji au aamkie upande mzuri wa kitanda na kutoa dhamana kwa kwa wote na wengi. Sheria za kutoa dhamana ziko wazi na kuna mambo mengi yanayoangaliwa ," Dollo alinukuliwa na gazeti la Nile Post nchini humo akisema.

Kumekuwa na maoni tofauti

Wengi hususan wakosoaji wa Rais Museveni wamemkosoa kwa kile walichosema kuwa anataka kutumia mbinu ya kuwanyima washitakiwa dhamana ili kuwalenga wapinzani wake kisiasa.

Kiongozi wa upinzani wa Uganda kutoka chama Forum for Democratic Change , Dkt Kizza Besigye hivi karibuni alisema kuwa Rais Museveni anataka kuwa mallamikaji, jaji na mtekelezaji wa hukumu kwa wakati mmoja.

"Anayeshutumu ni jaji na kutoa hukumu ; kama sheria inaingilia , atakuwa mtungaji wa sheria ," Alisema Besigye.

Kiongozi wa Muungao wa (ANT), Meja Jenerali Mugisha Muntu hivi karibuni alimuomba rais kuacha suala la kutoa au kumnyima mtu dhamana mikononi mwa mahakama.

Sheria ya inasemaje?

Haki ya dhamana ni haki ya kimsingi inayoainishwa katika kipengele cha 23 (6) cha Katiba ya 1995 ya Jamuhuri ya Uganda

Katiba inasema kuwa wakati mtu anapokamatwa kwa tuhuma za kosa la uhalifu , ana haki ya kuwasilisha maombi kwa mahakama ya kuachiliwa kwa dhamana na mahakama inaweza kumpatia dhamana mtu yule kwa masharti kulingana na jinsi sababu za mahakama zinazofaa.