Uchaguzi Uganda 2021:Bobi Wine ni nani na nguvu yake ni ipi?

Bobi

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Ezekiel Kamwaga
    • Nafasi, Mchambuzi

Nilimuona Bobi Wine ambaye jina lake asili ni Robert Kyagulanyi Ssentamu kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2008.

Nilikuwa nafanya kazi nchini Uganda na ndiyo kwanza wimbo wake maarufu wa 'Kiwani' ulikuwa unatamba.

Marafiki zangu waandishi wa habari walikuwa wamekwenda kumwona katika ofisi zake zilizokuwa katika eneo la Kamwokya Kaskazini Mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala, nami nilijiunga katika msafara huo kwa lengo la walau kumtia machoni.

Wakati huo, hakukuwa na aliyekuwa na mawazo kwamba mbunge huyu wa sasa Jimbo la Kyadondo Mashariki, angekuja kuwa mwanasiasa mashuhuri achilia mbali mshindani namba moja wa Rais Yoweri Museveni na chama chake cha NRM katika Uchaguzi Mkuu wa Januari mwakani.

Wakati huo, miaka 12 iliyopita, Bobi alikuwa akijulikana kwa kuimba nyimbo zinazoeleza maisha ya watu masikini - yeye mwenyewe akiwa amezaliwa na kukulia katika mazingira ya kimasikini huko Kamwokya, na hilo ndilo jambo lililompa umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi wa taifa hilo ambao wengi wao ni masikini.

bobi

Chanzo cha picha, AFP

Nilipigwa na butwaa nilipoanza kusikia habari za Bobi Wine zikianza kupamba moto.

Nikashangaa zaidi niliposikia amefanikiwa kuwa mbunge mwaka 2017; akiwa mgombea binafsi huku akiwabwaga wagombea wa vyama vikuu vya NRM na FDC vilivyokuwa na wagombea maarufu kwenye jimbo hilo.

Nini hasa kimemfanya mwanamuziki huyu mashuhuri aliyekuwa akisifika kwa kuimba nyimbo za kimapinduzi nakujiita ''Rais wa ghetto' kubadilika na kuwa mshindani wa kipekee dhidi ya utawala wa takribani miongo minne wa NRM?

Kijana, Mkristo na kutoka kabila la Baganda.

Wagombea wa urais nchini Uganda

  • Taaluma: Mhandisi, Mwanasiasa
  • Umri: 57
  • Mwaka 1994, Patrick Oboi Amuriat aliwania ubunge. Kati ya 2001 na 2016, alikuwa mbunge wa alikuwa mkosoaji mkubwa kuhusu kuondolewa kwa ukomo wa muhula wa urais.
  • Amuriat amesoma Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alipata shahada yake ya kwanza na ya pili katika Uhandisi wa Ujenzi. Amefanya kazi na makampuni kadhaa ya uhandisi nyumbani na ugenini, mashirika ya maenedeleo ya kijamii pamoja na kuwa mtumishi wa umma kama mhandisi wa wilaya.
  • Alikuwa miongoni mwa jopo la bunge ambalo liliunda chama cha Forum for Democray (FDC). Ni rais wa tatu wa chama cha FDC.
  • Taaluma: Mwandishi wa michezo, mchungaji
  • Umri: 48
  • Joseph Kiza Kabuleta ni kiongozi wa vuguvugu la Kupigania taifa na raia (ROCK)
  • Ukosoaji wake wa utawala wa chama tawala cha NRM ulimfanya kufungwa jela 2019. Alisema kwamba mateso aliopitia katika mikono ya vyombo vya usalama akiwa jela yalimfanya kumpinga rais Museveni katika kinyang’anyiro cha urais mwaka huu.
  • Kabuleta alifanya kazi kwa muda mfupi kama msimamizi katika majengo mjini kampala na ana cheti cha diploma katika uhandisi alichokipata baadaye miaka ya tisini, kisha alibadilisha taaluma na kuanza kuwa mwandishi wa michezo na alifanya kazi kama mwandishi katika kampunu ya The Crusader, kabla ya kujiunga na gazeti la The New Vision ambapo alikuwa mwandishi maarufu wa safu.
  • Baada ya kuondoka katika chumba cha habari 2016, alikuwa mchungaji kiongozi katika kanisa la watchman Ministries.
  • Taaluma: Mwandishi wa habari, Mtaalamu wa masuala ya fedha
  • Umri: 40
  • Nancy Linda Kalembe ndiye mwanamke wa pekee anayewania urais katika uchaguzi wa mwaka 202.
  • Ahadi yake kuu ya kampeni ni kuimarisha maisha ya wanawake, uchukuzi, miundo mbinu na biashara za jamii.
  • Nancy kalembe ana Shahada ya Sayansi katika masuala ya Idadi ya Watu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere.
  • Taaluma: Hana ajira
  • Umri: 24
  • John Katumba ni mgombea mwenye umri mdogo zaidi katika kinyang'anyiro cha urais nchini Uganda. Ameweza kugombea baada ya kuondolewa kwa umri wa urais kufuatia marekebisho ya kikatiba yaliofanywa mwaka 2017.
  • Alifuzu kutoka chuo kikuu cha Makerere kitivo cha biashara mwezi Januari 2020 akipata shahada ya uchukuzi na mipangilio.
  • Ijapokuwa bado hajatoa ilani ya uchaguzi, Katumba ameahidi kuangazia ukosefu wa ajira na kuwawezesha wanawake.
  • Taaluma: Wakili, Mwanasiasa
  • Umri: 53
  • Norbert Mao amehudumu kama mbunge aliyechaguliwa katika jimbo la Gulu kwa awamu mbili kati ya 1996 na 2006.
  • Baadaye, alikua mwenyekiti wa mojawapo ya mabaraza katika wilaya ya Gulu ambapo ni wakati alipohusishwa kuwa mpatanishi kati ya waasi wa kundi la wapiganaji wa LRA na serikali ya Uganda. Alipigania sheria ya kutoa msamaha kama sheria muhimu ambayo ingesaidia katika kusitisha vita hivyo kwa amani kaskazini mwa Uganda.
  • Mwaka 2010, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa rais wa chama cha Democratic Party, Mao alipigania urais wa Uganda katika uchaguzi wa 2011.
  • Mao ana shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alihudumu kama rais wa chama cha wanafunzi.
  • Taaluma: Mhandisi, Mtaalamu wa kilimo
  • Umri: 33
  • Mwaka 2016, Willy Mayambala alipigania kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama cha Forum for Democratic Change na kupoteza.
  • Ana Shahada ya Sayansi na Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kyambogo aliyoipata 2010. Baada ya kupata shahada, Mayambala alijiunga na mmoja ya wanafunzi wenzake kuanzisha kampuni ya Kamol Engineering Services Ltd na baadaye kuondoka miaka michache baadaye ambapo aliunda kamapuni yake binfasi JohnSemp Ltd.
  • Baba yake ambaye ni marehemu John Ssempala alikuwa alikuwa ni moja ya wapiganaji wa vita vya msituni vya 1980 hadi 1985 ambavyo vilimpatia madaraka rais Museveni.
  • Taaluma: Meja Jenerali Mstaafu , Mwanasiasa
  • Umri: 62
  • Meja Jenerali mstaafu Gregory Mugisha ndio rais na mgombea wa urais wa chama cha Alliance for National Transformation.
  • Muntu alikuwa mwanachama wa zamani wa kundi la waasi la NRA na alihusika pakubwa katika ufanisi wake kutokana na sifa yake ya kujitolea , utiifu na uwajibikaji.
  • Kufuatia ushindi wao 1996, Muntu alianza kwa kuongoza kitengo cha ujasusi wa kijeshi. Alikuwa kamanda wa kitengo maalumu cha jeshi 1989. Alishikilia wadhfa huo kwa miaka tisa hadi alipotofautiana na mkuu wa majeshi yote rais Yoweri Museveni 1989.
  • Ijapokuwa alimpatia wadhifa wa uwaziri Muntu alikataa wadhifa huo.
  • Alikuwa mbunge katika Bunge la Katiba la 1994-1995 ambalo lilijadili katiba ya Uganda. Mwaka 2021 Muntu alichaguliwa kuwa kamammoja ya wawakilishi wa Uganda katika bunge la Afrika Mashariki.
  • Taaluma: Rais wa Uganda
  • Umri: 76
  • Yoweri Kaguta Tubuhrburwa Museveni amekuwa rais wa Uganda tangu 1986 kufuatia uasi wa miaka mitano alioongoza dhidi ya uatawala wa awamu ya pili wa Apollo Milton Obote.
  • Aliahidi kuongoza kwa miaka minne pekee lakini sasa amefanya mabadiliko ya kikatiba mara mbili ili kumsaidia kusalia madarakani. Mara ya kwanza alihusika katika kubadilisha katiba 2005 ili kuondoa kikomo cha urais ili kumwezesha kuwania tena urais 2006 licha ya kuahidi hadharani 2001 kwamba hangewania urais tena.
  • Harakati zake za kuwania urais 2021 ziliwezeshwa kupitia marekebisho ya kikatiba mwaka 2017 kuondoa umri wa kikomo cha kuwania urais ambapo maafisa kutoka kikosi chake cha ulinzi walivamia bunge na kuwatoa nje viongozi waliokuwa wakipinga marekebisho hayo hadi pale yalipopitishwa.
  • Kabla ya sheria hiyo kupitishwa raia wa Uganda walio chini ya umri wa miaka 18 ama wale walio na zaidi ya umri wa miaka 75 walikuwa hawawezi kuwania urais.
  • Taaluma: Mchungaji
  • Umri: 38
  • Fred Mwesigye ameshikilia wadhifa wa mchungaji na mchungaji mshiriki katika kanisa la House of God Worship Ministry International, kanisa la God World Missions huko Kamwokya, Kampala na mchungaji kiongozi katika eneo la Kitoro mjini Entebe ambalo alilianzisha 2017.
  • Mwaka 2019, aliamua kujiunga na siasa ili kuitikia 'wito wa Mungu' kuiokoa Uganda kutoka kwa matatizo kwa kile ambacho anakiita enzi mpya ya mapenzi.
  • Ahadi yake kuu ni kuongeza mishahara ya walimu na madaktari pamoja na kuzuia kuparaganyika kwa taifa hilo 'kunakosababishwa' na chama tawala cha NRM, mathalan anataka kupunguza wilaya kutoka 135 hadi 62.
  • Taaluma: Mwanamuziki, mjasiriamali
  • Umri: 38
  • Robert Kyagulani Ssentamu, kwa jina maarufu Bobi Wine, ni mwanamuziki maarufu, msanii na mjasiriamali. Alianza kufanya muziki mapema miaka ya 2000 na kujitofautisha katika muziki wake aina ya dance hall kwa kuuchanganya na jumbe za masuala yanayokumba jamii.
  • Juni 2017, alipigania ubunge katika uchaguzi mdogo na kushinda kwa wingi wa kura dhidi ya chama tawala cha NRA na chama cha Forum for Democratic Change FDC.
  • Ijapokuwa kwa sasa anaongoza chama cha National Unity Platform (NUP), Kyagulani bado ni maarufu na na kundi la Nguvu ya Umma, vuguvugu aliloanzisha kupitia kampeni ya kutoondolewa kwa sheria ya ukomo wa umri wa kuwania urais.
  • Kyagulani katika siku za hivi karibuni amepata umaarufu mkubwa akionekana kuwa mpinzani mkuu wa rais Museveni katika uchaguzi wa urais wa 2021.
  • Taaluma: Wakili, Luteni Jenerali mstaafu
  • Umri: 61
  • Luteni Jenerali mstaafu Henry Tumukunde ni wakili ambaye aliipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Makerere 1981. Pia ana stashahada katika usimamizi wa mafuta na gesi kutoka Chuo cha Geneva.
  • Ni mbunge wa zamani wa chama tawala cha NRA tangu mwaka 1996, amehudumu kama katibu na mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Uganda nchini Uingereza , mkurugenzi wa mipango na usimamizi katika jeshi, mkuu wa idara ya ujasusi jeshini, kamanda wa kitengo cha nne cha jeshi kaskazini mwa Uganda na mkurugenzi mkuu wa shirika la usalama wa ndani.
  • Mwaka 2015, Tumukunde alistafaishwa kutoka jeshini akiwa katika wadhifa wa Luteni Jenerali na akarudishwa kuhudumu kama waziri wa masuala ya usalama kati ya 2016 na 2018.

Kwa mujibu wa mwandishi mashuhuri wa Uganda, Andrew Mwenda, Bobi Wine ana sifa tatu zinazomfanya kuwa mgombea wa aina yake dhidi ya Museveni.

Taifa la Uganda lina sifa kubwa tatu zenye mashiko kisiasa; lina wananchi wengi vijana, dini inayoongoza kwa watu wengi ni Wakristo wa madhehebu ya Wakatoliki na kabila lenye watu wengi zaidi ni la Baganda ambalo watu wake wanapatikana katikati ya taifa hilo.

Mke wake ameonekana akimuunga mkono katika harakati zake za kisiasa licha ya ghasia zinazotokea

Chanzo cha picha, Instagram

Maelezo ya picha, Mke wake ameonekana akimuunga mkono katika harakati zake za kisiasa licha ya ghasia zinazotokea

Bobi Wine ni kijana mwenye umri wa miaka 38, anatoka katika kabila la Baganda na dini yake ni Mkristo wa madhehebu ya kikatoliki.

Katika maboksi hayo matatu muhimu, kijana huyu anatia alama ya tiki kote.

Katika miaka yote tangu serikali ya Rais Museveni ilipoamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi, mshindani wake mkuu alikuwa ni Kizza Besigye wa chama cha FDC ambaye ingawa kiumri ni mdogo kwake; wana historia inayoshabihiana kisiasa.

Suala la umri si dogo katika muktadha wa uchaguzi wa Uganda mwakani.

Katika taifa lenye watu milioni 43 - kutokana na makadirio ya sensa ya mwaka 2014 iliyoonyesha taifa hilo lina watu milioni 34.9, zaidi ya nusu ya watu wake wana umri chini ya miaka 40.

Kimsingi, kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Uchaguzi ya Uganda, asilimia 80 ya wapiga kura wa taifa hilo katika uchaguzi huo wana umri wa kati ya miaka 18 hadi 40; umri ambao Bobi Wine anaangukia.

Ni asilimia 1.7 tu ya wapiga kura wa Uganda wana umri wa zaidi ya miaka 70.

VBobi

Chanzo cha picha, Twitter-Bobi Wine

Takwimu hizo zinaonyesha pia kwamba watu wenye umri wa kuanzia miaka 50 na kuendelea - ambao angalau wameona mafanikio ya utawala wa Museveni katika maisha yao, wanafikia asilimia 13 ya wapiga kura wote.

Linapokuja suala kabila, lina maana kubwa pia kwa sababu ukiondoa idadi yao kubwa, Wine ni mtu aliye karibu na utawala wa kifalme wa kabila lake.

Kuna wakati alikuwa akijulikana kwa jina la Omubanda wa Kabaka (Mpambanaji wa Kabaka - yaani Mfalme wa watu wa kabila la Baganda).

Katika miaka yake 20 ya kwanza madarakani, Rais Museveni alikuwa akiungwa mkono kwa kiasi kikubwa na watu wa kabila hilo kwa sababu alipindua serikali iliyokuwa ikiongozwa na watu kutoka Kaskazini mwa Uganda ambao hawakuutendea kwa heshima utawala huo.

Baada ya miaka 35 ya madarakani, Ufalme na watu wa kabila hilo wanaweza kuwa sasa wanafikiri kuwa na mtu wao katika Ikulu ya Entebbe.

Hii ni kete kubwa kwa Bobi.

Matumizi ya mitandao ya kijamii

Maelezo ya video, Kura za vijana zinaweza kumpa ushindi Bobi Wine?

Takwimu rasmi za Mamlaka ya Mawasiliano ya Uganda zinaonyesha kwamba taifa hilo sasa lina watu takribani milioni 20 wanaotumia mtandao wa intaneti.

Kwa sababu wengi wa watumiaji wa mitandao ni vijana na watu wa umri huo ndiyo wengi zaidi nchini humo, inadaiwa kwamba Bobi na chama chake cha NUP kinatawala dunia ya mitandao ya kijamii kwa asilimia takribani 80.

Kila anachofanya Bobi Wine katika siasa zake anahakikisha kuna namna kinawafikia wananchi wa Uganda kwa haraka.

Hii ndiyo namna aliweza kuwateka watu kwa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba mwaka 2017 ambapo alihakikisha picha mnato na video zinasambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa faida yake.

Ingawa mwanasiasa kukubalika katika mitandao ya kijamii si kigezo pekee cha kumwezesha kushinda uchaguzi, lakini tofauti hii ya asilimia 20 kwa 80 ni kubwa kiasi kwamba inatakiwa iingie katika hesabu kali za uchaguzi.

'Anatuelewa'

Marion Kirabo, mwanafunzi wa sheria aliye na umri wa miaka 23 na ambaye anagombea kiti cha udiwani ni mmoja wa wafuasi wake.

"hata kabla iingilie siasa alikuwa mtu ambaye aliwavutia vijana na walipenda sana kuwa karibu naye,"anasema.

"Hususan kupitia muziki wake, ungeona wazi kwamba anaelewa masuala ya kijamii ambayo yanawakumba vijana, hasa wale wanaoishi katika makazi duni."

Wakati Rais Museveni alipoingia madarakani mwaka 1986, Bobi Wine alikuw ana kama miaka minne, akiishi Kanoni.

Eneo la kati mwa Uganda lilikuwa ngome ya mapigano ya msituni ambayo ilileta madarakani kundi la waasi wa Bw. Museveni, National Resistance Army, na mrengo wao wa siasa, National Resistance Movement (NRM).

Babu yake Bobi Wine, Yozefu Walakira, alikuwa katika kundi lingine la waasi lakini mara kwa mara wakati wa mzozo alikuwa akimkaribisha Museveni nyumbani kwake.

Walakira alifariki wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na majeraha aliyopata baada ya nyumba yake kulipuliwa katika shambulio ambalo pia liliwaua jamaa zake watatu. .

Ujasiri

nn

Chanzo cha picha, Twitter-Bobi Wine

Kwa sababu ya historia ya miaka ya nyuma ambako Waganda wamewahi kutawaliwa kijeshi na madikteta, wananchi wameanza kuamini kwa viongozi wanaoonekana ngangari na wanaoweza kuvumilia shubiri za kisiasa.

Kwa kujua kwamba Museveni anapenda kutumia mabavu katika siasa zake, Bobi amekuwa wakati mwingine akifanya matukio ya akichokozi dhidi ya vyombo vya dola, ili nguvu zisizo za kawaida zitumike dhidi yake na kumjengea huruma kwa wananchi.

Mojawapo ya vitendo ni kukutana na wafuasi wake katika mikusanyiko mikubwa ya watu ingawa serikali imeipiga marufuku kwa sababu ya ugonjwa wa Corona.