Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matokeo ya Uchaguzi Marekani 2020: Maafisa wa usalama wa uchaguzi wapinga madai ya wizi ya Trump
Maafisa wa uchaguzi nchini Marekani wamesema kuwa kura za mwaka huu zilikuwa "mojawapo ya kura zilizolindwa zaidi katika historia ya Marekani ", na kupinga madai ya wizi wa kura.yaliyotolewa na Rais Donald Trump.
"Hakuna ushahidi kwamba mfumo wowote wa kupigia kura ulifutwa au kupotea kwa kura, kubadilishwa kwa kura, au ulifanyiwa mizengwe yoyote ile," kamati ilitangaza.
Walizungumza baada ya Bw Trump kudai bila ushahidi kwamba kura zake milioni 2.7 zilikuwa "zimefutwa".
Bado hajakubali kushindwa na rais mteule, Mdemocrat Joe Biden.
Matokeo ya uchaguzi wa tarehe 3 Novemba yalibashiriwa na karibu televisheni zote za Marekani TV mwishoni mwa juma lililopita.
Ubashiri wa BBC sasa kwamba Biden ameshinda Arizona, uliongeza ushindi wake kwa kura 11 wajumbe-ameshinda sasa 290, huku Trump akiwa na 217.
Bw Trump alianzisha upinzani wa kisheria taratibu dhidi ya makadirio ya kura katika majimbo muhimuna kutioa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa katika uchaguzi.
Wakati huo huo, China hatimaye imetoa pongezi zake kwa Bw Biden na mgombea mwenza Kamala Harris baada ya kimya cha siku kadhaa.
"Tunaheshimu chaguo la watu wa Marekani," alisema msemaji wa izara ya mambo ya nje. Urusi imesema kuwa inataka kusubiri "matokeo rasmi".
Ni kwanini tangazo ni muhimu?
Tangazo hilo ni la moja kwa moja la kutoka kwa maafisa wa serikali kuu na serikali za majimbo la kupinga madai yasiyo na ushahidi ya wizi katika uchaguzi.
Taarifa ya pamoja ya Alhamisi ilitolewa na baraza la uratibu wa miundombinu ya uchaguzi la serikali - ambalo linawajumuisha maafisa wa ngazi ya usalama wa ndani ya nchi na tume ya usaidizi ya uchaguzi ya Marekani pamoja na maafisa wa ngazi ya jimbo ambao husiamania uchaguzi na wawakilishi wa sekta ya mashine za kupigia kura.
" Uchaguzi wa Novemba 3 ulikuwa ni uchaguzi uliolindwa zaidi katika historia ya Marekani .
Sasa hivi, kote nchini, maafisa wa uchaguzi wanatathmini na kuchunguza mara mbili mchakato wote wa uchaguzi kabla ya kukamilisha matokeo ," kikundi hicho kilisema.
"Huku tukifahamu kuwa kuna madai yasiyo na msingi na uwezekano wa taarifa upotoshaji kuhusu mchakato wa uchaguzi wetu , tunaweza kukuhakikishia kwamba tuna imani kabisa katika na usalama na uadilifu wa uchaguzi wetu, na unapaswa kuwa na imani hiyo pia ,"iliongeza taarifa hiyo, bila kumtaja Bw Trump moja kwa moja.
"Unapokuwa na maswali, waulize maafisa wa uchaguzi ambao ni sauti za kuaminika kwani ndio wanaoongoza ."
Taarifa hiyo ilitumwa kwenye wavuti wa shirika la miundo mbinu ya usalama wa Kimtandao (Cisa), ambalo ni sehemu ya Wizara ya usalama wa ndani ya nchi.
Mkuu wa Cisa, Christopher Krebs,ameripotiwa kupata taarifa zaIkulu ya White House kuhusu kutofurahishwa kwake na hatua ya Cisa kuiita kampuni ya udhibiti wa taarifa za uvumi, Rumor Control , ambalo hukanusha taarifa potofu kuhusu uchaguzi.
Alhamisi Bw Krebs alishirikisha umma kauli ya mtaalamu wa sheria za uchaguzi ambayo ilisema: "tafadhali usishirikishe Twitter za unyama ambazo hazina msingi kuhusu mashine za uchaguzi, hata kama zimetumwa na rais ."
Mkurugenzi msaidizi wa Cisa Bryan Ware alijiuzulu Alhamisi .
White House ilikuwa imemtaka ajiuzulu mapema wiki hii, kulingana na taarifa za Reuters . Bw Krebs anatarajia kufutwa kazi, shirika hilo la habari lilisema.
Saa kadhaa kabla ya taarifa hiyo ya maafisa wa uchaguzi kutolewa, Bw Trum alikuwa ametwee kwamba mfumo wa mtandao wa kupigia kura uliotumiwa katika majimbo 28 ulikuwa umefuta kura zake , lakini hakutoa ushahidi kwa shutuma hizo kali.
Madai hayo yalihusiana na kutohesabiwa kwa kura katika moja wapo ya kaunti za Michigan . Matokeo rasmi awali yalionesha kuwa Bw Biden anashinda lakini baadaye yalirekebishwa na kuonesha kuwa Trump anaongoza.
Maafisa wa uchaguzi wa jimbo hilo walikubali juu ya kile kilichotokea, wakasema kosa la kibinadamu ndilo lililotokea, na sio kuingiliwa kwa mfumo wa kompyuta wa uchaguzi.
Je Warepublican wanamuunga mkono Trump?
Idadi ndogo lakini inayoongezeka ya Warepublican wanaunga mkono miito ya kupewa kwa taarifa za kiintelijensia za kila siku kwa rais mteule.
Senata Lindsey Graham, mshirika muhimu wa Trump, alikuw ani miongoni mwa wale ambao walisema Bw Biden anapaswa kuanza kupokea taarifa za siri za rais, kama ilivyo kwa kawaida kwa rais anayeingia madarakani.
Maseneta Warepublican Chuck Grassley, John Cornyn na John Thune walikubali, ingawa kiongozi wa Warepublican walio wachache katika bunge la wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy alisema Bw Biden "sio rais sasa" na anapaswa kusubiri.
Kati ya wabunge 10 na 20 Warepublican katika bunge la Congress hadi sasa ima wamempongeza Bw Biden au wamekubali kuwa lazima hatua zichukuliwe kuelekea kipindi cha mpito. Lakini wengi bado hawajakubali ushindi wa rais mteule.
- Rais wa zamani wa Barack Obama alisema maafisa wa ngazi ya juu wa Republican wanadhoofisha demokrasia kwa kuunga mkono madai ya Trump ya wizi.
- Spika wa bunge la wawakilishi Nancy Pelosi wakati huo huo alisema kuwa "upuuzi usioisha " unamaanisha kuwa janga la corona linapuuzwa.
- Senata Chris Coons aliiambia CNN kuwa baadhi ya Warepublican wamekuwa wakimuomba ampongeze Bw Biden kwa niaba yao kwasababu hawahisi kufanya hivyo wazi .
- Kiongozi wa wa walio wachache katika Seneti Chuck Schumer alisema kuwa Wanasiasa wa Republican "wanahoji uchaguzi wetu bila sababu lakini wanamuogopa Trump
Watu muhimu katika Chama pia wanasemekana kuwa wana matimaini kuwa Bw Trump atasaidia kampeni ya mabunge mawili katika kuendeshwa upya kwa uchaguzi mwezi Januari katika Georgia ambayo itaamua iwapo Warepublican watabakia na udhibiti wa seneti au la .
Bw Biden yuko mbele ya Bw Trump kwa kura milioni 5.3 - ambazo ni sawa na 3.4%, ambaye pia yuko nyuma katika kura za wajumbe 270 za urais. Rais Trump hajaonekana hadharani tangu uchaguzi ulipofanyika.
Taarifa zinasema amewaambia marafiki zake kuwa anatanga kuanzisha kampuni ya habari ya kidigitali itakayochukua kampuni ya kihafidhina ya mtandao wa habari-Fox News,ambao anahisi haummungi mkono kikamilifu.
Kwa mujibu wa televisheni ya CBS News, Bw Trump pia anazungumzia wazi uwezekano wake wa kuwania urais mwaka 2024 ili achukue tena kiti cha urais.
Biden amekuwa akifanya nini?
Alhamisi alizungumza na Papa Francis ambaye alimpa "baraka na pongezi ". Bw Biden atakuwa ndiye rais wa pili muumini wa Kanisa Katoliki la Roma kuiongoza Marekani.
Pia amezungumza na uongozi wa baraza la congress juu ya haja ya kutolewa kwa pesa za kuchochoa vita dhidi ya virusi vya corona huku maambukizi yakizidi ya watu 150,000.
Alitumia siku yake na timu yake ya mpito katika mji wa Wilmington, Delaware, ambako amekuwa akipanga uteuzi wa baraza lake la mawaziri.
Jumatano alimteua Mdemokrati mkongwe Ron Klain kuwa mkuu wa wafanyakazi wa White House