Saratani Nigeria:'Mke wangu angekuwa hai angepata tiba ya saratani'

Chanzo cha picha, Andrew Gift
Safari yangu ya ujane ilianza miaka mitatu iliyopita katika ofisi ya daktari wa saratani katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.
Mke wangu Garace, alifuata ushauri wa daktari badala ya kutafuta ushauri wa waponyaji wa kidini, ninaamini kuwa angepona saratani ya matiti na angekuwa bado na mimi na binti yetu mwenye umri wa miaka mitatu.
Alikwenda kufanyiwa vipimo vya uvimbe mkubwa na daktari akasema kuwa walikuwa wamebaini kuwa ulikuwa na "uvamizi wa carcinoma ".
Sikufahamu kile ambacho alimaanisha na akanifafanulia kuwa "uvimbe aliokuwa nao una saratani na tunahitaji kuanza mchakato wa kuidhibiti mara moja ili isisambae ".
Grace alionekana mwenye hofu na mdhoofu, na ninakumbuka nikimchukua mtoto wetu ambaye wakati huo alikuwa wa mwezi mmoja tu kutokla mikononi mwake kwa sababu nilikuwa ninaogopa ni nini angelikifanya baada ya kupata taarifa hiyo.
Kulikuwa na suluhu
Lakini mtaalamu wa saratani alituhakikishia kuwa kwa tiba atakayoipata angeweza kupona. Alitushauri kuwa afanyiwe tiba ya kuchoma seli za saratani -chemotherapy na labda afanyiwe upasuaji wa kuondoa matititi au mastectomy.
Kutokana na kile nilichoambiwa siku ile nilijaribu kuwa na matumaini kwamba suluhu ipo na kwamba bado nitaendelea kuishi na Grace, ambaye ndio kwanza nilikua nimeanza uhusiano nayeye mwaka mmoja tu kabla.

Chanzo cha picha, Andrew Gift
Andrew alikutana na Grace baada ya kusaidia kutatua mzozo baina yake na kondakta wa basi
Tulikutana mara ya kwanza katika mazingira ambayo hayakuwa mazuri kimapenzi ya kituo cha mabasi ya abiria mjini Abuja.
Alikuwa na mzozo na kondakta wa basi ambaye alikuwa amemtoza pesa zaidi za mzigo wake na nikaingilia kati kutuliza hali.
Tuliishia kuwa na mazungumzo katika safari na baadaye tukabadilishana namba zetu za simu.
Nilikuwa na umri wa miaka 33 wakati huo nikijihisi mpweke sana. Kama mtoto wa kwanza mkubwa wa kiume katika familia , nilikuwa nakumbushwa kila mara ninakotoka mashariki mwa Nigeria , utamaduni ni kuoa mapema na tayari waogo zangu wa kiume walikuwa tayari wameona.
Hatahivyo, nilisubiri miezi kadhaa kabla ya kuwasiliana na Grace na nikagudua kuwa tulikuwa hatuishi mbali.
Tulikiwa marafiki wa karibu sana halafu tukakubaliana kuoana.
Lakini miezi 13 tu baada ya harusi alipatikana na saratani.
Hapakuwa na tiba ya bure ya saratani na bima ya matibabu ya Grace haikuweza kugarimia matibabu, kwa hiyo ilibidi nifanye mipango ya kukopa fedha .
Kwa ujumla garama ilifika hadi naira 600,000 au dola 1,500; nilipata mkopo wa kulipia awamu ya kwanza ya matibabu.
Uamuzi mbaya zaidi nilioufanya
Lakini njiani nilipokuwa nikielekea kwenye duka la dawa kununua dawa za chemotherapy, Grace aliniita kuniambia kuwa hataendelea na matibabu.
Badala yake alikuwa na imani Mungu atamponya.
Aliniambia kuwa hiyo chemotherapy itaua seli zenye afya katika mwili wake pamoja n anile za saratani, na angependa kuweka imani yake katika dini.
Ni kweli kwamba madawa yanaweza kuharibu seli zenye afya, lakini wataalamu wanasema hii kwa kawaida huwa haidumu.
Nilijaribu kumshawishi Grace kubadili mawazo yake, lakini tayari alikuwa ameamua na nilihisi ninapaswa kukubali kutafuta suluhu nyingine-uamuzi mbaya zaidi niliowahi kuufanya.
Wanaigeria wengi ni waamini wa dini na inapokuja katika suala la afya wengi wanapendelea kupata usaidizi kutoka maeneo ya ibada kuliko hospitali.
Uamuzi wa Grace wa kukataa tiba ya chemotherapy aliupata kutokana ushauri alioupata kutoka kwa marafiki na familia. Wengi Nigeria wanaamini kuwa ugonjwa huo unaweza kuua na Grace aliogopa.
Alikubali kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe lakini hii ilikuwa ni suluhu ya muda kwani saratani ilirejea haraka na kwa hatari kubwa.
Mke wangu alikuwa imara sana na aliweza kuvumilia maumivu kwa miaka miwili bila kumuona daktari.
Hata hivyo tulitembelea makanisa na vituo vya maombi ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na nabii TB Joshua, lakini bado hatukupata suluhu.
Wengi miongoni mwa waponyaji hawa walichukua pesa na kutuahidi miujiza. Baadhi walimwambia kuwa siku atakayokwenda hospitalini ndio siku atakayokufa.
Tulipata dawa za kienyeji, ambazo tulishauriwa kuzitumia marafiki na ndugu.
Kutoruhusiwa kutaja saratani
Tuliomba pamoja na tukafanya mazoezi ya mwili pamoja mara kwa mara, alikunywa dawa za mitishamba na matunda, na akajinyima vyakula kadhaalakini maumivu hayakuisha.
Nilijaribu kumshawishi azungungumze na daktari, lakini alikataa.
Hata alipokwenda kupata matibabu ya malaria katika hospitali, alisisitiza kuwa nisitaje saratani.
Ilipofika mwezi Juni mwaka jana , ilikuwa ni dhahiri kuwa alikuwa amepoteza uzito wa mwili na alikuwa amekuwa dhaifu sana.
Halafu mwezi Julai, hali yake ya kiafya ikawa imezorota sana, kiasi kwamba sikuwa na chaguo jingine ila kumpeleka hospitalini kwasababu alikuwa anahangaika hata kupumua na hakuweza kusimama.
Hospitali mbili za kwanza ambako nilijaribu kuomba alazwe hawakutaka kumpokea, lakini ya tatu ilikubali kumshugulikia.
Unawezaje kutambua saratani ya matiti?
Dalili ambazo huonekana mara nyingi za saratani ya matiti ni uvimbe au kuongezeka kwa unene wa titi kusiko kwa kawaida-lakini kuna dalili nyingine pia:
· Kubadilika kwa umbo la titi na hisia zake
· Kubadilika kwa rangi ya titi, kama vile kuwa na upele au wekundu
· Kimiminika kinachotoka kwenye chuchu, tofauti na vinavyotoka unapokuwa mjamzito au unaponyonyesha.
Dalili hizi hata hivyo zinaweza kusababishwa na hali nyingine, kwahiyo ni muhimu kufanyiwa uchunguzi na daktari wa uvimbe wowote unaojitokeza kwenye matiti .

Chanzo cha picha, Andrew Gift
Nilikuwa ninaona kwamba bintio yetu , Princess Gold MmesomaChukwu, ambaye alikuwa naishi katika nyumba ya rafiki yetu alikuwa anaemia na alikosa joto la kukumbatiwa na mama yake.
Nilimpeleka hospitalini mara moja, lakini niliona kabisa kuwa alisikitika na hakuwa na uhakika afanye nini juu ya hali ya mama yake.
Hatimae, Mwezi Novemba Grace alipata maumivu ya kichwa yaliyoonesha kuwa saratani ilikuwa imesambaa hadi kwenye ubongo na akaingia katika hali mahututi na hakuweza kuamka tena kamwe.
Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 33.
Kuonja utamu wa ndoa na halafu kuupoteza yalikuwa maumivu makali.
Sasa niko mpweke, mwenye mawazo na huwa ninashindwa kumakinika. Kuna machozi kila siku.












