Watu 13 wafariki kwa ajali ya basi Kenya maeneo ya Kisumu

ajali

Chanzo cha picha, DAILY NATION

Watu 13 wameuwawa na wengine kujeruiwa katika ajali ya basi lililokuwa linatoka soko la Awasi Kisumu kuelekea Nairobi nchini Kenya majira ya saa tano na nusu usiku siku ya alhamisi, imeripotiwa na gazeti la nchini humo la Daily nation.

Kamanda polisi wa mjini Kisumu, Benson Maweu amethibitisha miila ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Eldoret Express alfajiri ya leo saa nane na nusu.

"Basi lililokuwa linasafiri kutoka mji wa Kericho kuelekea Kisumu, barabara ya kuelekea Nairobi lilipokuwa linalipita lori", shuhuda Maweu alinukuliwa na Daily nation.

ajali

Chanzo cha picha, DAILY NATION

Kamanda wa polisi amesema kuwa kati ya watu hao 13 kulikuwa na mtoto mmoja.

Watu 12 walikufa papo hapo kwenye basi na huyo mtu wa 13 ni dereva wa lori pia alikufa.

AJALI

Chanzo cha picha, DAILY NATION

Ripoti ya polisi nchini humo inasema kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 51, na ajali imesababisha abiria 11 na madereva wote wawili wa basi na lori wamefariki.