Kwa nini alama hii imeorodheshwa kuwa alama ya chuki

The OK hand emoji

Chanzo cha picha, Getty Images

Alama hii imeorodheshwa kwenye alama zisizokubalika na kuashiria chuki.

Alama hiyo amabayo ni maarufu hutumika kama kiashiria cha "Msimamo wa dhabiti wa utawala wa watu weupe" kwa mujibu wa Anti-Defamation League (ADL).

Lakini kundi la kupambana na chuki nchiniMarekani, kinasema matumizi makubwa ya alama hiyo ya mkono ni kuonyesha idhini au kukubaliana jambo au mtu yuko poa.

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba utambuzi wa matumizi ya alama hii sio tu kwa kuangalia jinsi mtu alivyoitumia.

Alama inayounganisha kidole gumba na cha pili inayoorodheshwa kumaanisha kauli mbiu ya ubaguzi na kukubali mauaji ya kimbali.

Protester holds up OK sign

Chanzo cha picha, Getty Images

Orodha ya alama za chuki ziliorodheshwa mwaka 2000 kwa lengo la kusaidia kutambua alama za makundi ya msimamo mkali.

Kwa sasa kuna zaidi ya alama 200 .

Hata kama makundi ya msimamo mkali yataendelea kutumia alama hizi kwa miaka mingi ,wataunda alama mpya , kauli mbiu kuelezea mitazamo yao ya chuki", Jonathan Greenblatt, kiongozi wa ADL alisema.

"Tunaamani kuwa usimamizi wa sheria na matakwa ya umma ni kupewa taarifa kamili kuhusiana na maana ya taswira hizi, ambazo zitasimama kama onyo kutokana na uwepo wa jamii ya upingamizi.

The OK sign

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alama hii ilianza kutumika muongo wa 17 nchini Uingereza

ADL inasema alama hiyo ya Poa imekuwa mbinu maarufu ya kugandamiza kutokana na watu wenye mlengo wa kulia, ambao mara nyingi kuweka picha kwenye mitandao yao ya kijamii, ikiwa kama alama ya mzaha mtandaoni.

Hutumia alama hii kumaanisha kama kuna maana iliyojificha, ikiwa kama njia ya kuwalaghai wale wa mlengo wa kushoto.

Brenton Tarrant flashed a hand sign as he appeared in court on Saturday charged with murder

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtuhumiwa huyu alitumia alama hiyo wakati amehukumiwa kunyongwa

Dkt Paul Stocker, ambaye ni mtaalamu wa historia anasema kuwa harakati hizo za kupinga alama hiyo kumaanisha kukubali wakati ni alama ambayo watu wanaweza kuwasiliana kufanya uovu.

"Alama hiyo inaashiria kuwa hao ni miongoni mwao."

Utaratibu wa kutafuta vielelezo vya kudhibitisha kuwa alama hiyo inamaanisha bado haujakubalika.

Kutumia vidole kwa namna hiyo licha ya kwamba utamaduni wa siku hizi unamaanisha kuwa ni kuonesha kukubaliana na kuwa kila kitu kiko sawa .

Matokeo yake mtu anaweza kutumia alama hiyo huku akiwa anamaanisha jambo lingine kabisa.

line