Ni kwanini Trump ''ameyaua'' mazungumzo siri aliyoyayaandaa mwenyewe na Taliban?

Rais wa Marekani Donald Trump anasema mazungumzo na Taleban yaliyolenga kumaliza vita vya miaka 18 nchini "yamekufa ".
" Kulingana na mimi , yamekufa , na yamekufa ," aliwaambia waandishi wa habari wa White House Jumatatu.
Mnamo wikendi Bwana Trump alifuta mipango yake ya siri ya kuupokea ujumbe wa aliban nchini Marekani baada ya kikundi hicho kumuua mwanajeshi wa Marekani.
Pande mbili zilionekana kuwa na mkataba wa siri na Taleban inasema kuwa Marekani ndiyo "itapata hasara kubwa zaidi "kwa kufuta mazungumzo hayo.

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani ameufanya mpango wa kukondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghastan kuwa lengo muhimu la sera ya kigeni , lakini alipoombwa wanajeshi 14,000 waendelee kuwepo huko alisema : " Tungependa kutoka nje ya Afghanstan lakini tutaondoka katika wakati sahihi."
Bwana Trump alikuwa amekaribia kuwapokea viongozi wa Taliban pamoja na rais wa Afghanstan Ashraf Ghani katika ikulu ndogo ya Camp David kabla ya kuyafuta mazungumzo hayo ghafla.
"Walifikiri kuwa lazima wangewauwa watu ili kujiweka katika hali nzuri kidogo ya mazungumzo ", aliwaambia maripota , akiataja shambulio hilo kama "kosa kubwa ".
Ni nini alichokisemaBwana Trump?

" Mkutano wetu ulikuwa umepangwa . Lilikuwa ni wazo langu kuuitisha na lilikuwa ni wazo langu kuuvunja. Wala sikujadili swala hili na mtu yeyote ," Bwana Trump alisema Trump wakati alipokuwa akiondoka White House kwa ajili ya mkutano wa kisiasa katika jimbo la North Carolina.
" Nilifuta mkutano wa Camp David kwa misingi kwamba Taliban walifanya kitu ambacho kusema ukweli kisingepaswa kufanyika ," alisema , akilaani shambulio lililowauwa watu 12 nchini Afghanstan akiwemo askari mmoja wa Marekani.
Bwana Trump amekosolewa kwa kukubali uwezekano kuwapokea Taliban kwa mkutano siku chache tu kabla ya maadhimisho ya mashambulio ya kigaidi dhidi ya Marekani ya Septemba 11
Lakini Bwana Trump alitetea wazo lake , akisema "kuwa na mkutano ni kitu kizuri, sio kitu kibaya".
Taliban hawakuwahi kukubali kumaliza mashambulio yao dhidi ya Afghanstan na vikozi vya usalama huku mazungumzo yakifanyika. Wanajeshi 16 wa Marekani wamekwishauawa mwaka huu.
Mnamo mwaka 2001, vikosi vinavyoongozwa na Marekani viling'oa serikali ya Taliban nchini Afghanistan kwasababu wanamgambo hao waliupatia mtandao wa al-Qaeda fursa ya kuandaa mpango w amashambulio dhidi ya Marekani tarehe 11 Septemba.












