Mashabiki Kenya, Tanzania watambiana mitandaoni

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika mechi ya kufa kupona timu ya Tanzania Taifa Stars inakutana ana kwa ana leo na Harambee stars ya Kenya uwanjani kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kutafuta pointi tatu muhimu.
Taifa Stars ya Tanzania na Harambee Stars ya Kenya zimekuwa gumzo hii leo wakati macho na masikio vikielekezwa kwenye uwanjani kukutanisha timu hizi mbili za Afrika Mahariki.
Tanzania na Kenya zilianza na mkosi mashindano ya Afcon 2019.Tanzania iliangukia pua mechi yao kwanza kwa kushindwa na Senegal mabao 2-0 kisha Kenya nao wakaadhibiwa kwa mabao hayo hayo na Algeria.
Wakati kipute hicho kikisubiriwa kwa hamu kubwa ifikapo majira ya saa tano usiku saa za Afrika Mashariki. Mashabiki na wapenzi wa kandanda wa Tanzania na Kenya wamekuwa wakitupiana vigongo vya kejeli kila mmoja akimtambia mwenzie kuwa shughuli itakuwa moto na wataondoka na ushindi.
Kwenye mitandao ya kijamii kubwa lililotawala ni mchezo wa leo, mashabiki wakizipamba kurasa zao kwa tambo za hapa na pale, miongoni mwao ni mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idriss Sultan na mwenzake Eric Omondi wa Kenya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Wadadisi wanasema Kenya ina nafasi kubwa ya kupata pointi tatu wakizingatia takwimu za mechi kati ya mataifa haya mawili.Kwanini?
Kufikia sasa timu hizo mbili zimekutana mara tisa, na Tanzania ikashinda mechi mbili tu.Macho yote yanaangazia Cairo sasa kuona jinsi Mbwana Samatta atakavyoongoza kikosi chake dhidi ya nahodha mwenzake wa Kenya Victor Wanyama.
Lakini ni wazi kwa timu zote mbili kwamba mechi ya leo ni kibarua kipevu.
Mchezaji wa Harambee Stars Michael Olunga ameeleza, 'Tanzania ni jirani zetu na itakuwa mechi ngumu. Sote tulishindwa katika mechi zetu za ufunguzi. Kikombozi chetu sasa ni pointi tatu'.
'Tumejifunza kutokana na makosa yetu na tutajisahihisha katika mechi ijayo', ameongeza Olunga.
Hii ikiwa ni mara ya kwanza kufuzu tangu 1980, kocha raia wa Nigeria Emmanuel Amuneke ameleta matumaini kwa Tanzania baada ya kuisukuma timu hiyo kufuzu katika mashindnao hayo nchini Misri.
Matarajio sasa na swali kubwa ni je Taifa Stars italitingisa eneo la Afrika mashariki baada ya kurudi katika michuano hiyo?
Baadhi wanaitazama mechiya leo kama Derby ya Afrika mashariki.
Msisimko ni mkubwa kwa mashabiki wa kambi zote mbili, msema kweli akisubiriwa kujulikana.













