Mguu uliokatwa, sasa wapata akaunti ya Instagram

Mfupa wa mguu wa Kristi Loyall

Chanzo cha picha, BBC Sport

Maelezo ya picha, Mfupa wa mguu wa Kristi Loyall

Mwanamke mmoja ambaye aliyewashawishi madaktari kumkubalia kuhifadhi mguu wake uliokatwa, ameanzisha akaunti ya Instagram ya mguu huo.

Kristi Loyall mwenye umri wa miaka 25 alipatikana na aina nadra sana ya saratani katika mguu wake wa kuume, na akaambiwa kuwa njia pekee ya kushughulikia tatizo hilo ni kuukata.

"Majibu yangu ya kwanza yalikuwa ni kuufanyia utani," Ameiambia BBC. "Nikasema, 'Hei naweza kuubeba mguu wangu?

Na hapo ndipo nilipofahamu kwa hakika nauhitaji mguu wangu."

Awali mguu huo ulipofanyiwa upasuaji, lakini sasa umesababisha gumzo mtandaoni
Maelezo ya picha, Awali mguu huo ulipofanyiwa upasuaji, lakini sasa umesababisha gumzo mtandaoni

Hata ingawa daktari wake aliona maombi hayo kuwa yasiyo ya "kawaida," alikabidhiwa kiungo hicho cha mwili wake mwezi mmoja baadaye ndani ya mfuko.

Kristi, anayetokea Yukon huko Oklahoma, anaeleza: "Ni jambo la kushangaza. Vidole vyangu vilianza kusogea na mama yangu kwa hakika aliudhika mno, hasa kwamba naweza kusongeza vidole."

Licha ya upasuaji huo, Kristi aliweza kuona sehemu nyingine ya ucheshi, ambayo amekuwa akipitia.

"Kufikia hapo nilitenganishwa kabisa na hali halisi ya hisia," anasema.

"Nilikuwa na muda mrefu kukabiliana nalo hasa nyumbani, na kwa wakati huo huo, nilijawa na furaha na nikaanza kuufanyia mguu wangu mzaha."

Kristi, akifurahia fupa la mguu wake huko Oklahoma, Marekani
Maelezo ya picha, Kristi, akifurahia fupa la mguu wake huko Oklahoma, Marekani

Wazo la kuanzisha akaunti ya Instagram kwa mguu wake, lilitoka kwa rafiki wake, lakini Kristi alilipenda wazo hilo.

Alituma mifupa huo ili usafishwe na wataalamu, kufanywa mweupe na kuunganishwa pamoja.

Ameipa akaunti hiyo jina la One Foot Wander na picha yake ya kwanza ilikuwa mguu wake uliokatwa na mifupa chini yake, huku akiandika maandishi "Reunited".

Kwa sasa, anaweka picha kadhaa mara kwa mara katika maeneo yasiyo ya kawaida- ukiwa ufukweni, makaburini na hata kwenye mti wa Krismasi.

Kristi, akipiga picha mlimani Silent Hill huku akiandika karibu Mlimani
Maelezo ya picha, Kristi, akipiga picha mlimani Silent Hill huku akiandika karibu Mlimani
Picha kwenye mti wa Krismasi
Maelezo ya picha, Picha kwenye mti wa Krismasi
Mara hii ameufikia mchangani katika uwanja wa Golf
Maelezo ya picha, Mara hii ameufikia mchangani katika uwanja wa Golf

"Sina pesa za kusafiri kwingi, lakini huwa naubeba daima niendako, na nikiona kitu cha kunifurahisha au kuwa na wazo na jambo fulani nzuri ama ya kushangaza, napiga picha nao."

"Mara nyingi nauweka ndani ya kasha la kubebea viatu na kuutia ndani ya begi langu la mgongoni.

Nadhani watu wengi wanionapo, nikipiga picha wa mfupa wa mguu wangu, sifikirii kama wananiona niko timamu."

Picha anayoipenda na kuihusudu mno ni ile ya mguu wake pamoja na mbwa wake- ni picha nzuri mno kupiga hasa mbwa wanaopenda kutafuta mifupa.

"Anapendezwa sana nayo, " Kristi alisema. "Tukiiacha mezani, mbwa anajaribu kuutwaa na kwenda nao."