Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Cristiano Ronaldo hakulipa kodi
Inaripotiwa kuwa mcheza mpira wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, na wachezaji wengine wa kandanda, wamekwepa kodi ya mapato yao ya mamilioni ya dola, kwa kupitisha fedha hizo kwenye njia za kuzighushi hadi nchi za n'gambo kusikotozwa kodi.
Habari hizo zimechapishwa na gazeti moja la Ujerumani, Der Spiegel, na inasemekana zinatokana na data ya maelezo pamoja na kandarasi, makubaliano ya siri na barua pepe.
Mawakili wa Ronaldo wanasema, wakuu wa kodi wa Uspania wamekagua mapato yake na hawakuona kasoro yoyote.
Watu wengine maarufu wanaosemekana kutajwa katika ufichuzi huo, ni pamoja na Jose Mourinho, meneja wa Manchester United, ambaye kama Ronaldo, anawakilishwa na wakala Jorge Mendes.
Kampuni ya Bwana Mendes, Gestifute, inasema Bwana Mourinho amelipa kodi kamili kwa wakuu wa Uingereza na Uspania.