Makao ya Jean Ping yavamiwa nchini Gabon

Vikosi vya usalama vimevamia makao makuu ya chama cha mgombea urais aliyeshindwa Jean Ping.
Bwana Ping amekiambia kituo kimoja cha redio kutoka Ufaransa RMC kwamba amekimbia mafichoni kufuatia uvamizi wa makao makuu ya chama chake usiku kucha
Msemaji wa serikali alisema kuwa oparesheni hiyo kwenye mji mkuu Libreville ililenga kuwafurusha wahalifu.

Alisema wao ndio walihusika katika kuchomwa kwa majengo ya bunge siku ya Jumatano.
Bwana Ping alisema kuwa watu 2 waliuawa wakati wa uvamizi katika makao makuu ya chama.

Chanzo cha picha, EPA
Mapema wafuasi wake waliinga barabarani kupinga tangazo kuwa rais Ali Bongo alishinda uchaguzi kwa chini ya kura 6000.
Kwa sasa kiongozi huyo wa upinzani amedai kuwa anahofia usalama wake na kwamba huenda akakamatwa muda wowote.








