Wafilipino wakataa aliyekuwa rais kuzikwa katika makaburi ya mashujaa

Zaidi ya wafilipino 1000 wameandamana mjini Manila dhidi ya mpango wa kuuzika mwili wa Rais wa zamani aliyefedheheshwa , Ferdinand Marcos, kwenye eneo la mashujaa wa taifa hilo.

Waandamanaji hao walihimili mvua kubwa iliokuwa ikinyesha, na kumuomba rais wa sasa , Rodrigo Duterte, kufuta mpango huo.

Mwaandamanaji mmoja, seneta Risa Hontiveros, amemtaja rais Duterte kuwa adui wa mashujaa wa Ufilipino.

Rais huyo wa awali anatuhumiwa kuhusika katika ufisadi , na ukiukaji wa haki za binaadamu.

Serikali yake ilipinduliwa mwaka wa 1986, na aliaga dunia akiwa uhamishoni miaka mitatu baadaye.