Amnesty : Qatar inawadhulumu wahamiaji

Chanzo cha picha, .
Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limesema kuwa serikali ya Qatar halijafanya lolote kumaliza unyanyasaji wa wahamiaji.
Amnesty inasema kuwa licha ya shinikizo kwa Qatar kufanya mageuzi katika sera zake za ufanyikazi hakuna lolote lililobadilika.

Maelfu ya wahamiaji wanadaiwa kupokonywa vyeti vya kusafiria na kunyimwa haki ya mapato yao katika mpango ambao ulidhaniwa utamalizwa tangu ilipoteuliwa kuwa mwenye wa kombe la dunia mwaka wa 2022.
Shirika hilo limesema dhuluma hizo zinaiharibia taifa hilo la ghuba na shirikisho la soka duniani FIFA hadhi zao.

Chanzo cha picha, Getty
Amnesty International limeishutumu Qatar kwa kushindwa kufanya mabadiliko muhimu katika sehemu kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa wafanyakazi wenye uhuru wa kubadilisha kazi, kuondoka nchini humo na pia kujiunga na chama cha wafanyakazi.
Hata hivyo Qatar imekanusha madai ya kuwadhulumu wafanyikazi na kusema kuwa inafanya mageuzi kadhaa katika sheria za leba.








